Askari usalama barabarani Mbagala agongwa na daladala

Askari usalama barabarani Mbagala agongwa na daladala

Ni busara kutoa taarifa kama hizi zinazogusa hisia za watu baada ya kupata taarifa kamili na sio kwa kukurupuka tu bila kujua kinachoendelea. Unatuchanganya hasa wale jamaa wa karibu na huyo unayetoa taarifa zake.
 
ASKARI wa usalama barabarani, aliyejulikana kwa jina moja la Riziki, WP 2806 CPL Riziki, aliyegongwa na daladala aina ya DCM wakati akiwa katika harakati za kutimiza majukumu ya kazi eneo la Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam jana asubuhi amefariki dunia leo.
Mpaka mauti yanamfika, marehemu alikiuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili

Source: Global Publishers
 
Nasikitika kuwataarifu amefariki leo ,mungu ampe pumziko la amani
 
Ni nini kifanyike ili kuzuia umwagikaji wa damu za Watanzania kwa kupitia ajali za barabarani? Hili nalo sasa ni tatizo kubwa kama lmahakama ya kadhi, rushwa, ufisadi na maradhi.
 
Ni busara kutoa taarifa kama hizi zinazogusa hisia za watu baada ya kupata taarifa kamili na sio kwa kukurupuka tu bila kujua kinachoendelea. Unatuchanganya hasa wale jamaa wa karibu na huyo unayetoa taarifa zake.

Ndio uzuri wa utandawazi. Mmezoea kuletewa habari zilizochakachuliwa
 
Nasikitika kuwataarifu amefariki leo ,mungu ampe pumziko la amani

RIP Askari wetu .... Pole kwa familia yake.

Hizi ndio habari za kumpigia kampeni kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari .... hili janga la ajali linamaliza sana watu ..... waache kujaza siasa tu front pages wakati watu wanakufa na hamna anayejali kuchukua hatua kali!
 
Pole sana kwa msiba huo Mungu ablaze mahali pema roho yake. Ni kitendo cha kinyama kuweka picha ya mtu aliyepata ajali kama mlivyoieweka.
 
All in all , inabidi tuwape credits hawa askari wetu , no matter what especial traffic police ,hawa watu nina wa envy mno wanafanya kazi kwenye mazingira magumu/ hatarishi mno ,kama wale mama zetu wanaofagia barabara .POLE MAMA TRAFIK KWA YALIYOKUPATA , I HOPE FOLENI ITAONGEZEKA SEHEMU KWANI JEMBE MOJA LIMEPUNGUA.
 
Poleni sana.

Nawahurumia watoto wake Mama asubuhi ametoka kuelekea kazini, pengine watoto nao shuleni, baadae wanaletewa taarifa Mama yao mpendwa amefariki, inasikitisha sana
 
Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kituo cha Mbagala, Koplo Riziki Mohamedi ambaye alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi) alifariki dunia jana saa 4 asubuhi alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

Askari huyo aligongwa juzi asubuhi eneo la Mbagala Rangitatu akiwa anaongoza magari, ghafla gari aina ya Toyota Hiace inayofanya safari zake kati ya Temeke na Kongowe, lilishindwa kushika breki na kumgonga.

Ofisa Uhusiano Msaidizi wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya fahamu, Moi, Patric Mvungi alithibitisha kufariki kwa askari huyo. "Huyu askari alilazwa Moi tangu jana (juzi) na amefariki leo (jana) saa 4 asubuhi," alisema Mvungi.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kienya Kienya, alisema utaratibu wa mazishi unafanywa."Tuko kwenye majonzi na tunafanya maandalizi ya maziko, kwa sasa tunawasiliana na ndugu wa marehemu ili kujua atazikwa wapi na siku gani hivyo utaratibu ukikamilika tutawajulisha," alisema Kienya.

Kienya alisema dereva wa gari lililomgonga askari huyo, liliyagonga magari mengine manne yaliyokuwa mbele yake na kusababisha watu sita kujeruhiwa."Majeruhi hao walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Aliyeumia zaidi ni huyu askari," alisema Kienya.

Alisema Polisi wanaendelea kumsaka dereva huyo ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria, kwani alikimbia baada ya ajali kutokea.

Chanzo: Mwananchi
 
Duuu imenisikitisha sana maana wakati anagogwa nilikuwa nashuhudia,yaani nilisikitika sana,kweli akuwa na makosa ila Ndio siku ilifika
 
Apumzike kwa amani, poleni sana wafiwa na jeshi la polisi kitengo cha barabarani.
 
Duuu imenisikitisha sana maana wakati anagogwa nilikuwa nashuhudia,yaani nilisikitika sana,kweli akuwa na makosa ila Ndio siku ilifika

Hivi wewe bwana mbona matukio mengi unakuwepo? Lile la juzi mkuu wa Wilaya Arumeru alipotangaza walimu wakatwe mshahara kuchangia maabara nawe ulikuepo.
 
Back
Top Bottom