Askari usalama barabarani Mbagala agongwa na daladala

Askari usalama barabarani Mbagala agongwa na daladala

Jerhy

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2013
Posts
3,135
Reaction score
1,000
Hivi punde kuna taarifa za kugongwa kwa askari Wa Usalama barabarani huko Mbagala akiwa katika jitihada za kulisimamisha dakadala hilo lenye safari za kutoka Temeke kwenda Mbagala chalambe. Askari walikuwa wanne , jitihada za kunasua abiria wanne wengine waliokuwa ndani zinaendelea.

Traffic Amegongwa na gari aina DCM leo akiwa kazini,point mbagala rangi 3,aliwahisha Temeke Hospital na baadae kuhamishiwa Muhimbili.

Aliyepata ajali ni WP 2806 Cpl Riziki, chanzo cha habari kinasema hali yake si mbaya sana.

---------------------------------

UPDATE:

Taarifa za kuaminika zinasema Trafiki huyo kapoteza maisha mapema leo (16/09/2014) akiwa bado hospitali.

Tumia lugha ya kibinadamu basi, hata kama jamaa wanatupiga faini za kuvizia bado haiwezi kujustfy wewe kushadadia binadamu mwenzako apatapo majanga. Povu limekutoka hata story tenyewe umeshindwa kutiririka. Pumua halafu rudi tena.
 
Hivi punde kuna taarifa za kufyekwa kwa askari Wa Usalama barabarani huko Mbagala akiwa katika jitihada za kulisimamisha dakadala hilo lenye safari za kutoka Temeke kwenda Mbagala chalambe. Askari walikuwa wanne , jitihada za kunasua abiria wanne wengine waliokuwa ndani zinaendelea.

Source: Clouds FM

Huu sio uandishi. when . where. who. what.
 
mleta mada unaonekana una jazba kupita kiasi na matrafik......tupe data zaidi ilikuwaje! pole sana trafik wa mbagala
 
Matraffic me nawachukulia ni maadui. Haki kwao imetendeka. Hakuna trafic msafi wa tabia
 
Utafyekaje mtu kwa daladala!
Kwani daladala lina makali kama upanga?
 
Unamatatizo ndugu, yule naye ni binadamu. Pamoja na madhaifu yao, nawaheshimu sana askari wa usalama barabarani kwani huwa wanasaidia sana ku harmonize hali ya barabara ikichafuka. Madereva wenyewe wazembe, magari mabovu, halafu hamjiamini, hata kama huna kosa, unatetemeka na kukimbilia kutoa rushwa!
 
Huu sio uandishi. when . where. who. what.

@when leo where-mbagala who-askari wa usalama barabarani what-ajali....sema tu ameshindwa kuipanga vizuri habari hata kama ameichukua toka chanzo kingine cha habari
 
@when leo where-mbagala who-askari wa usalama barabarani what-ajali....sema tu ameshindwa kuipanga vizuri habari hata kama ameichukua toka chanzo kingine cha habari

kuna kiunga kimoja (sitting room) pembezoni mwa dar kinatumia jina hili.. astalavista
 
Last edited by a moderator:
Unagombana au! tulia eleza taratibu utaeleweka.

Back
Top Bottom