Askari polisi waliopambana wazawadiwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na jumuiya ya wafanyabiashara wa jijini Mwanza imewazawadia zaidi ya Shilingi milioni 11 askari polisi tisa waliowaua majambazi watano waliovamia duka la Mfanyabiashara wa kiasia, Mukeshi Nonee Ganatira Novemba 11, mwaka huu kwa lengo la kuiba fedha taslimu kiasi cha dola 60,000 za Marekani.

Polisi hao (ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiusalama) walikabidhiwa vitita hivyo vya fedha mwishoni mwa wiki na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evaristi Ndikillo kwenye hafla iliyohudhuriwa na maofisa wa ngazi za juu za jeshi hilo na waandishi wa habari,

ambapo kila askari polisi alikabidhiwa kitita cha fedha cha zaidi ya shilingi milioni moja.
Awali akizungumza katika hafla hiyo, Kamanda wa Polisi wa mkoa, Liberatus Barlow, alisema kuwa polisi hao wamezawadiwa kiwango hicho

cha fedha, mara baada ya jumuiya ya wafanyabiashara wa mkoa wa Mwanza kuguswa kutokana na jinsi ambavyo walivyowaona maaskari hao wakipambana na majambazi hayo asubuhi ya Novemba 11 mwaka huu.

"Ndugu Mkuu wa mkoa fedha hizi zimetolewa kwa vijana hawa shupavu wa jeshi letu, hasa mara baada ya jumuiya ya wafanyabiashara wa mkoa wetu kuthamini na kuzikubali juhudi walizozionyesha wakati wa mpambano ule na majambazi na kwa hiari yao wenyewe waliamua

kuchangisha fedha ambazo leo hii tunawazawadia vijana hawa. Kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la polisi ninawapongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya," alisema Kamishina Barlow.

Alisema sanjari na utoaji wa zawadi hizo kwa maaskari wake, jeshi la polisi litaendelea kushirikiana na raia wema kwa mpango wake wa ulinzi shirikishi ili kuhakikisha kuwa wanatoa taaarifa katika jeshi hilo ili wahalifu waweze kudhibitiwa kikamilifu.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI



 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wakati tukio hili linatokea nilikuwepo maeneo hayo nikashuhudi police wanavyomimina risasi kwa hiyo mijambazi,!? Kwa kweli walistahili kupongezwa.
 
kumbe zoezi lao la kupiga mabomu ya machozi na kuua raia wema kwenye maandamano limesaidia eti?
 
Wengi wa hao majambazi ni wananchi, Polisi wetu pia ni wananchi wa nchi hii. Kazi waliyoifanya ni ya kutukuka
wanastahili pongezi. Hata kama wakati mwingine vitendo vyao hatuvipendi haimaanishi kuwachukia moja kwa moja
kwani ni hakika tunawahitaji sana kwa ajili ya usalama wetu na mali zetu. Tuwape ushirikiano ili wasife moyo. Bunduki
akiwa nayo jambazi ni hatari sana hakuna kati yetu atakayethubutu kuisogelea.
Hata hivyo siafiki namna zawadi zenyewe zilivyotolewa, kuanika sura zao kwenye TV ni hatari kwa maisha yao na ya
familia zao. Ndugu za majambazi na washirika wao wanaweza wakawatambua kirahisi na kulipa kisasi hapo baadaye.
 
kumbe kwenye tv wameonekana sasa kuna haja gani kuficha majina yao?
 
walistahili pongezi na zawadi ila c zawadi za kimcharuko namna hii, zawadi bora ni ile itolewayo na mkono wa kulia wa kushoto ikawa haujui kitu!
 
Back
Top Bottom