Askari Magereza wamsukuma Lissu kibabe

Askari Magereza wamsukuma Lissu kibabe

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
16,818
Reaction score
62,031
Katika hali inayoendelea kuitia dola aibu, Leo mahakamani Askari Magereza amemsukuma ndugu Lissu na kumsababishia sintofahamu kubwa.

Lissu ambaye ni kiongozi wa Umma, ambaye anastahili heshima katika jamii, inashangaza dola inamfanyia kitendo hiki. Dila isiyoheshimu viongozi wa umma hii ni dola ya namna gani?.

Hata kama ni kiongozi wa upinzani lakini ni kiongozi ambaye nyuma ana wananchi wengi, anastahili heshima.

Pamoja na hayo Ndugu Lissu anafahamika changamoto zake za ulemavu kutokana na Jaribio la kumuua kwa risasi 16. Kwa nini Askari wa jeshi Magereza nchini wamfanyie jambo kama hili?

Hii ni aibu kubwa, ni ukatili wa kiwango cha hali ya juu sana, ni unprofessionalism, na inaonyesha ni namna gani Askari wa Jeshi la Magereza wasivyoheshimu viongozi wa kitaifa. Hii haikubaliki hata kidogo!.

Jeshi la Magereza litoke na kulitolea kauli hiki kitendo, na wahusika wawajibishwe. Askari wasioheshimu viongozi wa kitaifa hata kama ni wapinzani au wako mahakamani hawafai.


View: https://youtu.be/ZnFQ-wYNfu4?si=mvOChVgwy3r-uLoa
 
Wamevaa joho la maaskari magereza lakini c wao.wamevaa kitambaa usoni ili wasitambulike.
 
Back
Top Bottom