Askari Magereza mbaroni kwa kukutwa na pembe za ndovu

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Askari Mageraza wa gereza la Msalato A.8070 SSGT Cosmas Ndasi (51) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukutwa na pembe za ndovu vipande sita vyenye thamani ya sh 103.5 milioni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto akiongea na waandishi wa habari leo jijini hapa amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa April mosi mwaka huu katika mtaa wa Kilimani akiwa na vipande hivyo vya pembe vyenye uzito wa kilogramu 13 sawa na tembo watatu.

“Tulitengeza mtego na Askari huyo akanasa na kumkamata akiwa ameficha kwenye mfuko vipande vya pembe za ndovu kwa ajili ya kumsubiri mteja ili kufanya mauzo,” amesema Muroto.

Katika tukio jingine Muroto amesema kuwa wanamshikilia Ambokile Mwampulo (32) kwa tuhuma za kujifanya afisa usalama wa Taifa na kudanganya watu ili kujipatia fedha.
 
Mzee hawatomfanya lolote waache amalizie miaka yake tisa ale mafao.
 
Hahahaha !!
Ila kweli aisee,,,ifike mahali serikali iliangalie hill.

Tena mi nahisi wataongezeka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
... labda makampuni yenye fedha nyingi ila mtanzania wa kawaida ukiruhusiwa kufuga tembo sijui utawalisha nini hadi wafikie umri wa kuvuna pembe? maana kula yao ni kwa tani sio mbuzi au kondoo wale! Utawatunza vipi na kwa banda la aina gani wasiishie zao au kuleta mtafaruku mtaani? In short ni biashara kichaa hailipi.
 
Back
Top Bottom