Askari JWTZ waionya Dawasco | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari JWTZ waionya Dawasco

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, Mar 28, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa Dar es Salaam, wameeleza kukerwa na uongozi wa Kampuni ya Huduma za Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASCO) kwa kutangaza na kukata maji katika kambi zao. Sambamba na hilo, wamewaonya wakataji maji hao kuwa kitendo cha kukata maji na kuingia kambini bila kuutaarifu uongozi wa kambi husika, ni kukiuka sheria za uingiaji kambini na ipo siku watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali.

  Kwa mujibu wa taarifa ya onyo ya wanajeshi hao, Mkurugenzi Mkuu wa Dawasco, Alex Kaaya na watendaji wenzake, wanalaumiwa kuwa na ajenda ya siri yenye kutaka kulitikisa Jeshi na kuwakasirisha askari ili wafanye fujo. Wanajeshi hao walisema serikali ilikwishawaagiza Dawasco na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuacha kulikatia Jeshi huduma hizo kwa kisingizio cha madeni na kuongeza: “Hivi wanatangaza madeni hayo wanalitangazia Jeshi au serikali? Waelewe Jeshi halina vyanzo vya mapato ya kulipia ankara ya maji, ni serikali ndiyo yenye jukumu la kulipa.”

  Hata hivyo, taarifa ilisema wamefuatilia na kubaini kuwa fedha zinazotolewa na serikali kulipia huduma hizo, zinalipwa zote kwa taasisi hizo na wao ndio wanaolipa fedha nyingi zaidi kuliko wateja wote, na hata bili za kubambikizwa, hivyo waache kuwanyanyasa na kutamba. “Sisi tunapenda kumhakikishia Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Jakaya Kikwete na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, kuwa pamoja na vitendo hivyo vyote vya kulihujumu jeshi tuko imara na tutaendelea kutekeleza majukumu na wajibu wetu kwa uadilifu na nidhamu ya hali ya juu,” ilisema taarifa.

  Akitoa maelezo kuhusu malalamiko hayo, Mkuu wa Idara ya Operesheni wa Dawasco, Jackson Mibala, alisema wamekubaliana na uongozi wa JWTZ kuwa watamaliza kulipa deni lao lote. Kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita walikuwa wakidaiwa Sh milioni 860 na hadi sasa wamelipa Sh milioni 150. Alisema: “Rais hakusema wasikatiwe, ila alisema watulipe na wasiolipa wakatiwe maji nasi muda tuliokubaliana ukipita kabla hawajalipa kama tulivyokubaliana, tutakata maji, sisi tusipolipa umeme tunakatiwa, hivyo nasi tutawakatia wasipolipia huduma.” Alisema wao wanaingia kwenye kambi kwa utaratibu unaotakiwa na hakuna wa kuwazuia kukata maji iwapo watakuwa hawajalipa.
   
 2. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  This is stupid, if they are not paying why not? if not who actually ought to pay? why should they react against the one who is not paying for their bills. Rubbish!!!
   
 3. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Military junta mentality. Mkuu wa nchi na wengi tu wanaomzunguka ni wanajeshi - ni rahisi kwao kujisahau kwa sababu ni kama tu vile tuna a government ruled by a committee of military leaders.
   
 4. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Wakulaumiwa ni wao JWTZ. Hivi wanataka wawe wanatumia maji bila kulipia na kama watafanya fujo watakuwa wamedhamiria tu. Walipe bills na tuone kama DAWASCO watawakatia maji. Mimi nadhani JWTZ linataka kutumia mabavu kwa hili.
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ndio hivyo kama hawawezi kulipa wavunje jeshi
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kwa nini zisikatwe huku huko hazina..yaani mgawo wa pesa wa JW na Polisi ikawa minus pesa ya umeme na maji. Hazina ikalipa TANESCO na DAWASCO directly??

  This way kulumbana kungeisha..maana hii pesa wakipewa wanafanyia mambo mengine au zinaliwa!
   
 7. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Lakini si wanapewa hizo fedha? Swali ni je, pesa zinaenda wapi? Na ujue hizi ni pesa za walipa kodi na siyo zawadi kuwa watumie wanavyotaka. Sasa wanaposhindwa kuwajibika wanataka kutumia vitisho. Tuwe wastaarabu na tuwajibike kila mmoja sehemu yake.
   
 8. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  JWTZ sio wastaarabu naunga mkono hoja yako wapewe net of electricity and water bills
   
 9. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Hii ni kuwatafutia manundu hao wakata maji, Mkuu wa operesheni yeye atakuwa yuko ofisini anakenua tu wakati vijana wake wakitolewa baru!
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Waachieni DAWASCO wawakatie maji wanajeshi, wanajeshi wachukue nchi kama Madagascar.

  Labda tunaweza kuwa na afadhali.
   
 11. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakichukua nchi kwa sababu wamekatiwa maji hapatakuwa na afadhali yeyote,it will be a disaster!After all jeshi la Tanzania lina tofauti gani na mafisadi tunaowaona mitaani,mbona na wao wameshafisadishwa.

   
Loading...