Askari JWTZ wafanya vurugu kituo cha polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari JWTZ wafanya vurugu kituo cha polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mgomba101, Oct 29, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Watu wanaosadikiwa kuwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wamefanya vurugu katika kituo cha polisi kilichopo Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani cha mjini hapa na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali kituoni hapo.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, askari hao walifika kituoni hapo juzi saa 12:00 jioni huku wakimkokota mwenzao aliyedaiwa kuonekana amelewa.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe, alipoulizwa kwa njia ya simu yake ya mkononi kuhusiana na tukio hilo, alithibisha kutokea.

  Hata hivyo, Kamanda Massawe hakutaka kuingia kwa undani zaidi bali alisisitiza kuwa taarifa za kina atazitoa leo pamoja na kutaja jina la askari huyo.

  Kwa upande wake, Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alijibu kuwa hajapata taarifa.
   
Loading...