Askari JWTZ tuhuma nzito

Askari JWTZ tuhuma nzito

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
KATIKA hali isiyo ya kawaida, askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanadaiwa kuwafanyia ukatili mkubwa vijana 11, wakazi wa eneo la Keko Magulumbasi B, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam kwa kuwapiga na kuwalazimisha wanywe maji machafu yenye kinyesi.

Tukio hilo ambalo limefananishwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, linadaiwa kutokea Septemba 12 mwaka huu, saa 11 jioni, katika eneo la Keko Magulumbasi B.

Inadaiwa kuwa, wanajeshi hao ambao walikuwa saba wakiwa na sare za jeshi hilo, walifika Keko Magulumbasi B wakiwa na kijana mmoja mwenye asili ya Kiarabu na kuwavamia vijana waliokuwa wakila chakula kwenye kibanda cha chipsi.

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa, wanajeshi hao waliwakamata vijana hao na kudai wanahusika kupora simu ya kijana mwenye asili ya Kiarabu aina ya Tecno yenye thamani ya sh. 25,000.

Pamoja na vijana hao kukataa kuhusika na tukio hilo, waliwekwa chini ya ulinzi, kufungwa mikono kwa kamba, kulazwa kifudifudi na kuanza kupigwa mikanda ya jeshi.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa, vijana hao walichukuliwa hadi kwenye bwawa la maji machafu yaliyochanganyika na kinyesi cha binadamu wakazamishwa vichwa vyao ndani ya bwawa hilo la kulazimishwa kunywa maji hayo.

Waliongeza kuwa, vijana hao wakiwa wameloana kwa maji machafu walichukuliwa na wanajeshi hao hadi Kituo Kidogo cha Polisi Keko na kuswekwa rumande na mmoja wao aliachiwa baada ya dakika 10.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo, walilazimika kuvamia kituo hicho na kufanya vurugu wakiwarushia mawe askari wa kituo hicho kwa lengo la kuwatoa vijana hao kwa nguvu wakidai wameonewa.

Hata hivyo, wananchi hao walitawanywa kwa risasi za moto zilizopigwa hewani na askari wa Kituo Kikuu cha Polisi Chang'ombe walioitwa kuongeza nguvu kituoni hapo.

Bw. Omary Abdu (30) ambaye ni mkazi wa eneo hilo ambaye alikuwepo kwenye eneo la tukio, alidai kutofurahishwa na kitendo kilichofanywa na wanajeshi hata kama vijana hao wameiba kwani walipaswa kufikishwa katika mamlaka husika ili hatua zichukuliwe.
"Walichokifanya wale wanajeshi ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu...naamini wanafahamika, itakuwa vizuri kama watachukuliwa hatua za kisheria," alisema.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, ambaye hakutaka jina lake litajwegazetini, aliwashutumu wakazi wenzake kwa kitendo cha kuvamia Kituo cha Polisi na kufanya fujo kwa kuwarushia mawe polisi.

Katika hatua nyingine, mkazi huyo alimtuhumu Mwenyekiti wa Mtaa wa Magulumbasi B, Bw. Mohamed Fundi ambaye alidai kupitia kikao chake na wananchi Agosti 29 mwaka huu, alihamasisha wagome kukamatwa na polisi.

Alidai kauli kama hiyo inaweza kuleta vurugu na uvunjifu wa amani hivyo zinatakiwa kukemewa na kila mkazi wa eneo hilo.
Majira lilimtafuta Bw. Fundi ambaye alikiri kufanya kikao na wananchi kwa tarehe hiyo ambacho kilikuwa na lengo la kuhamasisha maendeleo na kuwafahamisha wananchi haki zao si kuhamasisha vurugu au kuzuia wasikamatwe na polisi kama inavyoelezwa.
Alisema miongoni mwa haki hizo ni namna polisi anavyotakiwa kumkamata raia na asikamatwe usiku bila kuwepo kwa kiongozi wa eneo lake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Kihenya Kihenya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akidai taarifa alizonazo ni kwamba, vijana waliokamatwa wanajihusisha na wizi wa mifukoni.

Alisema wakiwa Kituo Kidogo cha Polisi Keko, wananchi walikivamia na kufanya vurugu hadi walipotawanywa na askari kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Chang'ombe kwa kupiga risasi hewani.

"Taarifa zinazosema vijana hao waliteswa na kunyweshwa maji machafu na wanajeshi bado sijazipata ila hawa vijana wanashikiliwa Kituo cha Polisi Chang'ombe wakisubiri kufikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika," alisema.


Inaelezwa kuwa, wiki moja iliyopita kijana huyo mwenye asili ya Kiarabu mkazi wa Keko Toroli, alivamiwa na vijana eneo la Keko Magulumbasi B, ambao walimpora simu ya mkononi tukio ambalo liliripotiwa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi Keko.

CHANZO:
​Majira
 
Waje kwangu tuoneshane brown belt holder on aikido and muai thai!
 
Wanajeshi tena. Hawa watu wanatakiwa kuishi kwenye kambi tu. Uraiani ni shida tu.
 
Hao raia ni wajinga walishindwa kuwavamia hao wanajeshi kipindi wanawatesa haoo vijana wao ili kuwaokoa na wakati hao wanajeshi hawana siraha yeyote wanakwenda kuvamia kituo cha police kwenye silaha au walikua wanaogopa magwanda?
 
huyu mwanajeshi anatakiwa kuchukuliwa hatua kali ikiwezekana hata kumfukuza jeshini kwa amelidhalilisha jeshi lote ni aibu pia kwa taifa letu
 
Hongera wanajeshi wetu! Itakua vyema mngelienda na mle ndani bunge la katiba mukawanyweshe maji machafu akina Kingwala(rais mtarajiwa}
 
Mje mechi ya Simba na Yanga oct 13
kuongeza ulinzi
 
Hii habar nimeiskia asbui,imenishtua sana,wanajesh hao ndo tunaambiwa wana nidham,gharama ya sim elf 25 ukamnyweshe binadam mwenzio MAVI!
 
Ni ujinga mtupu. Habari hii nayo ya kuandika eti kashfa jwtz! Hiyo mitaa wamejaa vibaka wengi wa ajabu. Tena wazee wao ndio wanawafuga na kuwatetea. Ni vizuri majeshi yetu kusafisha mitaa jama hivyo!
 
Pamoja ni kwamba ni tendo la kinyama lakini vibaka bhana wanakera sana. Wapigwe tu. Walishaniliza home. Nmefuatilia polisi hadi leo 0/0.
 
Hao raia ni wajinga walishindwa kuwavamia hao wanajeshi kipindi wanawatesa haoo vijana wao ili kuwaokoa na wakati hao wanajeshi hawana siraha yeyote wanakwenda kuvamia kituo cha police kwenye silaha au walikua wanaogopa magwanda?
wagewavamia hao, wanajeshi kivipi? kwa hali ya kawaida hata kama ukuta ndugu yako anapigwa, na wanajeshi huwezi ukaingilia kesi moja kwa moja lazima utazame chanzo ni nini ndiyo uchukue hatua.
mimi naona walichokifanya wanainchi ni sawa.
 
Nani ana mamba za simu za hao wanajeshi, natamani wafike huku mitaa ya bom bom na kijiwe samli, hali bado si nzuri kivile
 
Naona jeshini kumeingia tatizo kubwa la watu kufanya kazi zisizo wahusu kwa ubabe na ujinga. Nadhani kiwango cha elimu kwa wanajeshi kiangaliwe maana watu waliokua wakorofi shuleni ndio wanafeli mitihani na kwa sababu wanakua na uwezo wa kuhonga na wengine wana ndugu huko jeshini wakishafanikiwa kupata nafasi jeshini wanahamishia ukorofi wao jeshini, tena wengine vyeti wananunua mwisho wa siku ndo wanakuja kusumbua raia kutokana uelewa wao kua mdogo maana wanadhani kazi yao ni kupamban na wananchi kwa kutumia mafunzo yao ya kijeshi.
 
Sidhani kama hawa askari wanafahamu ni kwa nini hilo jeshi linaitwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
 
Walichokif
anya kipo sawa kabisa naona mnaotetea hap
a hawajawahi kuibiwa kw
A sisi tuliokwisha
Ibiwa ni sawa tu tena hiyo mitaa ni balaa tupu
 
wagewavamia hao, wanajeshi kivipi? kwa hali ya kawaida hata kama ukuta ndugu yako anapigwa, na wanajeshi huwezi ukaingilia kesi moja kwa moja lazima utazame chanzo ni nini ndiyo uchukue hatua.
mimi naona walichokifanya wanainchi ni sawa.

Hivi kumbe karne ya sasa bado ina mabongolala wengi kama wewe wanaoamini kuwa mwanajeshi anaweza kumpa kipigo raia anapomkuta ametenda kosa!
 
Hawa hapa hawajaiba hata Nokia ya tochi,lakini wanakunywa maji machafu kwa hiari yao.
 

Attachments

  • 1410796639103.jpg
    1410796639103.jpg
    59.5 KB · Views: 131
Back
Top Bottom