Tuombe Mungu Uchaguzi 2015 ufanyike tuondoe misikule. Yule askari aliye muua Mwangosi kule Iringa kesi yake iliishia wapi? Make wale askari walio muua pamoja na kamanda Kamhanda bado wanakula kuku makazini.! Tumuulize nani kuhusu kisa hiki cha kuuwa mwandishi wa habari kwa bomu la machozi mchana kweupe?
Issue ya pili iliyo niacha mdomo wazi ni issue ya Rais wa nchi akitoa kauli ya kuwakaribisha chakula cha mchana Ikulu watu walio husika kuondoa miili ya watu waliokufa kwa kufunikwa na lile jengo la gorofa 16 hapa jijini Dar! bila kutaja walio jeruhiwa wanasaidiwa vipi au waliopoteza wazazi wao wanasaidiwa vipi! Sijui anamaliza lini uongozi! mi ananiboa sana!
Inabidi nitumie maneno makali kidogo, kwa kile ulichoongea kuwa askari kazi yake ni kutii tu, ndani ya jeshi hakuna kitu kinachoitwa HAPANA!
Sasa nimuulize huyo aliyecomment hivyo, hivi hajui kuwa hata ndani ya Jeshi, zipo amri halali na haramu?
Kwa mfano atokee kamanda kama RPC, kwa mfano wamemkamata mtuhumiwa ambaye ni dada yako uliyezaliwa naye tumbo moja, yaani mama yenu mmoja, sasa itokee kutokana na ubabe wa maaskari, wewe askari wa rank za chini ukaamrishwa na afande wako, umwingilie kimwili yule dada yako, utakubali?!
Hiyo haina tofauti sana na amri aliyotoa kamanda Kamuhanda, ya kuamrisha kuuawa Mwangosi, ile ni dhahiri ilikuwa ni amri haramu ambayo haikupaswa kutekelezwa na wale askari wa vyeo vya chini, hasa tukizingatia maelekezo aliyowahi kuyatoa JK wakati fulani kuwa ni lazima ufuate mfano wa mbayuwayu, wa kupima yale unayoambiwa kufanya na utumie common sense yako, kama kutekeleza hilo unaloamriwa, je hakuwezi kueta athari kwa jamii.
Ni dhahiri basi yule askari aliyetekeleza amri ya Kamuhanda hakufuata maelekezo ya JK.
Hata hivyo hayo mauaji ya Mwangosi bado yanaacha maswali mengi yanayokosa majibu.
Swali la kwanza, ni kwa nini hadi leo, kamanda Kamuhanda hajaunganishwa kwenye kesi hiyo ya mauaji ya Mwangosi, wakati upo ushahidi usio na mashaka yoyote kuwa yeye ndiye aliyeamrisha mauaji ya Mwangosi?!
Swali la pili, ni kwa nini tokea kesi ya askari huyo anayetuhuiwa kumwua Mwangosi, askari wenzake wamekuwa wakifanya juhudi za ziada kumziba uso ili wananchi wasiijue sura yake, je huo haujawa ushahidi usio na shaka yoyote kuwa huyo anayepelekwa mahakamani kama mtuhumiwa wa mauaji ya Mwangosi, akawa ni mtuhumiwa feki kabisa ambaye hata pengine hakuwepo hata siku ile ya tukio la mauaji ya Mwangosi, ambapo ianaweza kufanana sana na movie ya Kova kuhusu yule mkenya wake chizi, ambaye ndiye anadai aliyehusika na utekaji wa Dr Ulimboka, wakati mtuhumiwa no. 1 Ramadhan Ighondu wa Ikulu, akiachwa huru bila hata ya kuguswa?!
Kwa mazingira ya kesi ya Mwangosi na kesi ya Dr Ulimboka na tukio la hivi karibuni la kuteswa kwa Kibanda, bila watuhumiwa wakuu wa matukio hayo yote kukamatwa, tunapata ushahidi usio na shaka yoyote kuwa, matokeo yote haya ni lazima yana mkono wa mkuu wa nchi mwenyewe JK, kwa sababu kama si hivyo, isingewezekana aendelee kumkumbatia IGP Mwema aendelee kuwepo kazini bila ya kumfukuza kazi, wakati Jeshi lake la Polisi ni dhahiri, limeshindwa kabisa wajibu wao wa kazi no. 1 ambao ni KULINDA RAIA NA MALI ZAO, TAFAKARI KWA MAKINI SANA UJUMBE HUU!!!