Asiyoyajua Yericko Nyerere katika utafiti wa historia ya Mapinduzi ya Zanzibar

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
Hicho anachoita kitabu wala hakina publisher wala mswada haukusomwa na mhariri yeyote aijuae historia ya mapinduzi ni sawa na mtu aliyejifungia chumbani kwake anaandika katika mtandao wa kijamii.

Yericko hana moja alijualo katika historia ya mapinduzi. Ili kitabu kiwe ni kitabu kinatakiwa kiwe na habari mpya zisizo fahamika.

Huwezi kuungaunga habari walizoandika waandishi wengie ukasema umeandika kitabu.

Anachofanya Yericko ni kunakili yaliyoandikwa na wengine na kisha akayaleta kama fikra zake.

Hicho kichwa chake cha habari kwa haya aliyoandika ameyanakili kutoka kwangu kayabadilisha kidogo tu.

Mwenye maneno hayo ambayo mimi ndipo nilipoyachukua ni Prof. Mohamed Bakari nimemsikia akiyasema kwenye kongamano Kampala mwaka wa 2003 akisema, ‘’Ikiwa sisi hatutoandika historia yetu watakuja watu kutuandikia na huenda tusipendezewe na hayo waliyoandika.’’

Mimi ninapofanya rejea ya maneno hayo humtaja Prof. Mohamed Bakari.

Prof. Mohamed Bakari ofisini kwake Fatih University Istanbul 2015

Yericko angekuwa mjuzi kweli wa historia ya mapinduzi angemtaja kwanza Ali Mwinyi Tambwe aliyetumikia ''Intelligence.'' toka ukoloni hadi uhuru unapatikana 1961 tena akisafiri kueneza TANU na Nyerere bila ya Baba wa Taifa kujua kuwa taarifa zake zote zinafika kwa Gavana.

Yericko anamwaga majina ya kina Mzena ambao wakijulikana sana si mara moja katajwa katika mikasa ya akina Hashil Seif na John Okello.

Ali Mwinyi ndiye kiongozi wa Kambi ya Kipumbwi na ndiye aliyemtia Mohamed

Omari Mkwawa
katika njama ya mapinduzi na kumpa kazi ya kuvusha askari mamluki akifanyakazi chini ya Victor Mkello.

Victor Mkello akiwa nyumbani kwake Nguvumali, Tanga

Vitabu vyote vya historia ya mapinduzi hakuna mwandishi aliyelijua hili.

Yeye Yericko kazi ni yake kukopi tu.

Ghassany kazungumza na Victor Mkello si mara moja au mbili ilikuwa kazi ya kwenda Tanga na kurudi Muscat, Mkello hakufungua kinywa chake hadi nadhani alipohisi hana siku nyingi za kuishi na hapo alikuwa tayari mguu mmoja ushakatwa.

Mimi nilikuwapo kwenye vikao vyote isipokuwa cha mwisho Mkello alipoamua kueleza ukweli mbele ya mkewe kikao hiki mimi nilitoka nje kuwapa faragha na kumtoa Mkello wasiwasi kwa kuwa Dr. Ghassany yeye mgeni mimi naishi na yeye mji mmoja.

Yericko hana moja alijualo.

Na Dr. Ghassany nyumbani kwake Muscat 1999 alipomfahamisha Mwandishi mradi wa kutafiti historia ya mapinduzi ya Zanzibar ya 1964

Dr. Ghassany na Mzee Mkwawa, Tanga 2003
 
Pamoja na ukweli wa hoja zako lkn unaonekana ww ni mbinafsi, mchoyo na mwenye wivu wa dhahiri. Na unanisononesha zaidi kwa kuwa umri umeshakwenda; laiti ungelikuwa kijana ningesema maneno mabaya zaidi.

Mara nyingi unapoteza nguvu nyingi kubishana na kazi za Yericko kwa nukta nukta za ukweli unaoujua.

Ombi langu kwako kusanya kila unachokijua halafu tuandikie kitabu ukisambaze na tukisome kama alivyofanya Yericko kuliko hili povu lako la kila mara.

Mm binafsi nimesoma historia ya mapinduzi ya Zanzibar ktk vitabu vitatu tofauti na vyote vina vitu vinakinzana na kingine lkn pia nimesoma historia ya Zanzibar kupitia makala za Joseph Mihangwa ktk gazeti la RAI.

Na kwa kutumia akili yangu nimekubaliana na aliyoandika Mihangwa kwa 65% zaidi ya kwenye vitabu nilivyosoma.

Sasa baba ANDIKA. ANDIKA baba tusome.

HUU UNAFIKI WA KUJUA VITU HALAFU UNAA NAVYO MPAKA UFE NAVYO UTATUSAIDIA NINI SISI WA KIZAZI HIKI.
BILA YERICKO KUANDIKA UNGELIBISHANIA WAPI.
 
Hizo picha unazocopy kwa msisitizo wa hoja zako zitapendezesha kitabu chako kuliko hivi unavyofanya...Na kubwa zaidi Yericko hajaandika ya Zanzibar peke yake.Ameandika na mengine mengi kuhusu Tanganyika na maeneo mengine na huo ndio muundo wa kitabu chake.

WATU WEUSI TUNA TABU SANA AISEE!!
 
Mi hata sikuelewi,
Ungeweka reference au hata link kwanza ya Yericko Nyerere alisema nini hapo awali ili ukianza kumkosoa tujue unamkosoa kwa kitu gani.

Yaani hapa sielewi kua kuna Kitabu Yericko Nyerere amekitunga maalum kwa ajili ya Mapinduzi ndio unachokikosoa au amezungumzia Mapinduzi kwenye kilekitabu chake maarufu cha UJASUSI WA DOLA NA WA KIUCHUMI?? Jaribu kwanza kufafanua hili ndo tutaelewa uaandika nini.
 
Pamoja na ukweli wa hoja zako lkn unaonekana ww ni mbinafsi,mchoyo na mwenye wivu wa dhahiri...na unanisononesha zaidi kwa kua umri umeshakwenda,laiti ungelikua kijana ningesema maneno mabaya zaidi.

Mara nyingi unapoteza nguvu nyingi kubishana na kazi za Yericko kwa nukta nukta za ukweli unaoujua. Ombi langu kwako kusanya kila unachokijua halafu tuandikie kitabu ukisambaze na tukisome kama alivyofanya Yericko kuliko hili povu lako la kila mara.

Mm binafsi nimesoma historia ya mapinduzi ya Zanzibar ktk vitabu vitatu tofauti na vyote vina vitu vinakinzana na kingine..Lkn pia nimesoma historia ya Zanzibar kupitia makala za Joseph Mihangwa ktk gazeti la RAI .Na kwa kutumia akili yangu nimekubaliana na aliyoandika MihaTangwa kwa 65% zaidi ya kwenye vitabu nilivyosoma.

Sasa baba ANDIKA ..ANDIKA baba tusome.

HUU UNAFIKI WA KUJUA VITU HALAFU UNAA NAVYO MPAKA UFE NAVYO UTATUSAIDIA NINI SISI WA KIZAZI HIKI.
BILA YERICKO KUANDIKA UNGELIBISHANIA WAPI.
Ridhwani...
Una jina zuri sana na naamini unajua maana yake.

Huna sababu ya kunitishia kutukana.

Ikiwa hiyo ndiyo hulka yako usijuzuie fanya lile linalokupendeza usijali uzee wangu.

Ikiwa umelelewa katika nyumba isiyo na adabu nani wa kukubadili katika umri huo uliofika?

Mimi sijaandika historia ya Mapinduzi ya Zanzibar lakini nilikuwa Mtafiti msaidizi wa Dr. Harith Ghassany wakati anatafiti kitabu chake maarufu, ''Kwaheri Uhuru Ukoloni Kwaheri Uhuru.''

Inaelekea hukijui kitabu hiki kutokana na jinsi ulivyotoa fikra zako hapa Majlis na kusema unaiamini historia iliyoandikwa na Mihangwa.

Kwa taarifa yako Mihangwa anaandika makala kuhusu Zanzibar hana kitabu alichoandika kuhusu Zanzibar.

Kuandika kitabu hili ni jambo lingine kabisa.

Hiyo mosi.

Pili nimeandika na kuzungumza kuhusu historia ya Mapinduzi na naweza kukuwekea link hapa zikusaidie.

Tatu sina khiyana dhidi ya Yericko ila naandika kusahihisha yake ambayo mimi naona yamekosewa na hii ni kawaida katika duru za uandishi na duru za kisomi.

Nne nakushauri tufanya mjadala wenye adabu na ustaarabu hizi lugha za ''povu,'' zitumie kwa watu wengine kwangu si mahali pake.

Kwa kuhitimisha nakuomba urejee tena katika post yangu na angalia zile picha za Mzee Mkwawa na Victor Mkello.

Katika vitabu ulivyosoma vya historia ya Zanzibar umepatapo kuona mahali popote wametajwa?

Wale na wengine sikuwaeleza ndiyo waliokuwana funguo za Mapinduzi
ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

Hata Mihangwa hakuwa anawajua hawa.
Kwa mara ya kwanza kawasikia kwa Dr. Harith Ghassany.
 
Namkumbuka yule Profesa aliyesema "siwezi kukiamini kitabu cha historia kilichoandikwa kwa ligha ya kiswahili" sasa naanza kumuamini huyu Professa wangu.
 
Mi hata sikuelewi,
Ungeweka reference au hata link kwanza ya Yericko Nyerere alisema nini hapo awali ili ukianza kumkosoa tujue unamkosoa kwa kitu gani.

Yaani hapa sielewi kua kuna Kitabu Yericko Nyerere amekitunga maalum kwa ajili ya Mapinduzi ndio unachokikosoa au amezungumzia Mapinduzi kwenye kilekitabu chake maarufu cha UJASUSI WA DOLA NA WA KIUCHUMI?? Jaribu kwanza kufafanua hili ndo tutaelewa uaandika nini.
Shark,
Umeingia katikati ya mjadala wa Yericko.
Yericko
hapa Majlis ni mwenyeji na anafahamika sana na wengi.

Bahati mbaya ni wewe ndiyo hujui huu mjadala unahusu nini.

Soma alichoandika na nimeweka katika post yangu utaelewa nini ninasema.
 
Hizo picha unazocopy kwa msisitizo wa hoja zako zitapendezesha kitabu chako kuliko hivi unavyofanya...Na kubwa zaidi Yericko hajaandika ya Zanzibar peke yake.Ameandika na mengine mengi kuhusu Tanganyika na maeneo mengine na huo ndio muundo wa kitabu chake.

WATU WEUSI TUNA TABU SANA AISEE!!
Ridhwani,
Kitabu cha Yericko ni ''potpourri,'' yaani mchanganyiko
wa mambo mengi huwezi kufanya kitu kinachoitwa,
''demarcation,'' yaani mipaka.
potpourri
pəʊˈpʊəri,pəʊpʊəˈriː,pɒtˈpʊəri/
noun
  1. a mixture of dried petals and spices placed in a bowl to perfume a room.
    • a mixture or medley of things.
      plural noun: potpourris; plural noun: pot-pourris
      "he played a potpourri of tunes from Gilbert and Sullivan"
      synonyms: mixture, assortment, collection, selection, assemblage, medley, miscellany, melange, mix, variety, motley collection, mixed bag, patchwork, pastiche, blend; More
demarcation
diːmɑːˈkeɪʃ(ə)n/
noun
  1. the action of fixing the boundary or limits of something.
    "the demarcation of the maritime border"
    synonyms: separation, distinction, differentiation, division; More
    • a dividing line.
      plural noun: demarcations
      "a horizontal band that produces a distinct demarcation two inches from the top"
      synonyms: boundary, border, borderline, frontier, bound, limit; More

jimmy...
Maalim Faiza
ni mdogo wangu.

Mimi ni umri wa baba yako mjukuu wangu ndiyo kwanza
yuko chekechea unaweza kuniita baba badala ya babu ila
kama utapenda kuniita babu pia ni sawa.

Nimekueleza haya kukusaidia kunipima katika majadiliano.

Napenda san nikuite babu.

Huwa napita sana kwenye website yako kule kujaza ubongo.

Sasa babu fanya hivi niwekee vitabu vizuri vya historia za Zanzibari hapa.
 
Ridhwani...
Una jina zuri sana na naamini unajua maana yake.

Huba sababu ya kunitishia kutukana.

Ikiwa hiyo ndiyo hulka yako usijuzuie fanya lile linalokupendeza
usijali uzee wangu.

Ikiwa umelelewa katika nyumba isiyo na adabu nani wa kukubadili
katika umri huo uliofika?

Mimi sijaandika historia ya Mapinduzi ya Zanzibar lakini nilikuwa Mtafiti msaidizi wa Dr. Harith Ghassany wakati anatafiti kitabu chake maarufu, ''Kwaheri Uhuru Ukoloni Kwaheri Uhuru.''

Inaelekea hukijui kitabu hiki kutokana na jinsi ulivyotoa fikra zako hapa Majlis na kusema unaiamini historia iliyoandikwa na Mihangwa.

Kwa taarifa yako Mihangwa anaandika makala kuhusu Zanzibar hana kitabu alichoandika kuhusu Zanzibar.

Kuandika kitabu hili ni jambo lingine kabisa.

Hiyo mosi.

Pili nimeandika na kuzungumza kuhusu historia ya Mapinduzi na naweza kukuwekea link hapa zikusaidie.

Tatu sina khiyana dhidi ya Yericko ila naandika kusahihisha yake ambayo mimi naona yamekosewa na hii ni kawaida katika duru za uandishi na duru za kisomi.

Nne nakushauri tufanya mjadala wenye adabu na ustaarabu hizi lugha za ''povu,'' zitumie kwa watu wengine kwangu si mahali pake.

Kwa kuhitimisha nakuomba urejee tena katika post yangu na angalia zile picha za Mzee Mkwawa na Victor Mkello.

Katika vitabu ulivyosoma vya historia ya Zanzibar umepatapo kuona mahali popote wametajwa?

Wale na wengine sikuwaeleza ndiyo waliokuwana funguo za mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

Hata Mihangwa hakuwa anawajua hawa.
Kwa mara ya kwanza kawasikia kwa Dr. Harith Ghassany.
Mzee wangu inaonesha unapenda sana wazungusha vijana vijiwe vya kahawa na kuwapa utam wa historia nusunusu.(utani )..nadhan ungekua kwe sehemu mzuri zaidi kama ungetupa link tusome hiyo historia unayoijua kwani kwa jinsi unavyojitanabaisha ni kama weye ulishushiwa hiyo historia toka mbinguni...kama ulipata bahati ya kusimuliwa kujisifu tu bila kuiweka kama ilivyo unatuchanganya sis vijana ambao hatukupata bahati ya kuiona no bora basi hata huyo yericko nyerere alijaribu kutuonjesha hata kama haikuiva kisawasawa kama unavyojaribu kutuaminisha.

Nawasilisha.
 
Namkumbuka yule Profesa aliyesema "siwezi kukiamini kitabu cha historia kilichoandikwa kwa ligha ya kiswahili" sasa naanza kumuamini huyu Professa wangu.
Mgeni...
Huyu ni profesa gani anaefungwa na lugha?

Moja ya kitabu muhimu sana katika historia ua Urusi kabla na
baada ya WWII kimendikwa kwa Kirusi na Nikita Khrushchev.

Hiki kitabu kinaitwa, ''Khrushchev Remembers.''
Lakini wapo maprofesa na maprofesa.

Ushauri wangu ni kuwa wewe bado kijana na unahitaji kusoma
ili uelimike.

Soma chochote kwa lugha yoyote unayoijua kwani si maprofesa
wote wanajua Kiingereza.
 
Shark,
Umeingia katikati ya mjadala wa Yericko.
Yericko
hapa Majlis ni mwenyeji na anafahamika sana na wengi.

Bahati mbaya ni wewe ndiyo hujui huu mjadala unahusu nini.

Soma alichoandika na nimeweka katika post yangu utaelewa nini
ninasema.
Ni kweli nimeingilia Mjadala, siujui umeanzaje,
Ndio maana nikakushauri kua kwa faida ya wengine kama mimi ungegweka Link tuone Yeye alisemaje.

Sijakiona hicho kitu kwenye Red.
 
Back
Top Bottom