Asiyekuwa na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe. Hii imekaa vizuri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asiyekuwa na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe. Hii imekaa vizuri!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mozze, Sep 6, 2010.

 1. m

  mozze Senior Member

  #1
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii Comment nadhani imetulia, sasa tuhitimishe mijadala ya maisha binafsi na kuangalia masuala ya mustakabali wa TAIFA! Tujibu hoja za manufaa kwa wananchi!
  ------------------------------------------------------------

  Kwa watanzania wote wenye mapenzi mema na hata wale walioathirika vibaya na kimeta cha CCM wasome ujumbe huu. Ni bure, hakuna kulipia!

  Inatia huruma sana kwa vile wakati huu wa kampeni CCM wamebanwa mbavu kiasi kwamba hakuna anayethubutu kujibu hoja nzito kuhusu ufisadi. Wamebanwa sawasawa! Sasa wanatafuta pa kutokea! Wanachokifanya sasa ni kujaribu kuhadaa wananchi na hoja za maisha ya ndoa ya Dr Slaa. Hoja zenyewe, ukiziweka katika mizani moja na zile za ufisadi, utaona mwenyewe uzito unaangukia wapi.


  Kuoa na kuolewa na kuzaliana ni jambo la kawaida katika maisha ya wanadamu na wanyama, na wadudu pia. Hata panya wanaoana na kuzaliana. Na kunguni pia. Hiyo ndiyo hulka ya viumbe vyote! Na wala ngono haimuathiri panya katika uwezo wake wa kuchimba mashimo!


  Na wanadamu ni vivyo hivyo. Ngono haina madhara yoyote bali huburudisha na kuchangamsha. Historia inaonyesha kuwa wapo hata wafalme katika biblia waliokuwa na wanawake wengi. Lakini uwezo wao wa kiutawala unasifika hadi leo. Nani asiyemjua mfalme Daudi katika biblia? Huyu alikuwa wa wanawake wanane waliotajwa, na vimada kadhaa ambao hawakutajwa. Na Mfalme Solomon je? Naye hamumfahamu? Haya, huyu alikuwa na wanawake 700 na vimada 300. Dr Slaa ana mmoja!


  Baadhi ya marais mashuhuri waliokwisha kusifika duniani, walitokea kuwa na vimada! Rais Franklin Roosevert wa Marekani alikuwa na mke wa ndoa, Eleonor. Lakini kwa pembeni alikuwa na wa moyo wake, Lucy Mercer. Mwaka 1918 Eleonor alipogundua mahusiano hayo, Roosevert alimuacha Lucy. Lakini miaka michache baadaye Roosevert alipokuwa rais, Mapenzi na Lucy yakanoga kuliko hata mwanzoni. Roosevert alipofariki mwaka 1945 huko Georgia, kimada Lucy Mercer, alilia hadi akazimia. Roosevert anasifika hadi leo kwa uongozi wake uliotukuka. Ngono haikumuathiri!


  John F. Kennedy hadi leo wamarekani wanamjua kama "Ladies man"- Bwana wa mabibi. Huyu alikuwa mtaalam wa ngono! Pamoja na kwamba alikuwa na mke wake wa ndoa aliyejulikana kwa jina la Jacquiline, alikuwa pia na vimada wengine kibao akina Judith Exner na Marilyn Monroe. Na mara nyingi alitumbukia nao White House. Pamoja na ngono, anajulikana kwa utendaji wake mzuri, hadi uwanja wa ndege wa Kimataifa huko New York unajulikana kwa jina lake, J. F Kennedy International Air Port. Huyu naye, ngono haikumuathiri.


  Bill Clinton na Monica Lewinsky wanajulikana sana kwa mahusiano yao ya ngono. Lakini ni nani asiyemjua Clinton na utendaji wake wa kazi? Na huyu naye, ngono haikumzuia asifanye kazi zake.


  Jacob Zuma, rais wa Africa ya kusini, anao wanawake watatu. Na wote wanajulikana kama first ladies. Na bado kwa pembeni, anazo nyumba nyingine ndogo nne. Jumla wanawake saba. Dr Slaa ana mmoja..


  Nani asiyemjua mzee Nelson Mandela? Huyu alimwacha mke wake wa ndoa, akaoa mke wa mtu mwingine. Alimuoa mke wa Samora Mashel. Wala sifa ya Mandela haijapungua mpaka leo, mpaka kesho. Sasa sijui ninyi CCM mnatuletea utumbo gani! Hoja za kuacha mke na kuoa mwingine wala hata hazina mvuto zikilinganishwa na hoja za wizi na ufisadi! Poleni sana kwa kutapatapa!


  Watanzania ni wa kuhurumiwa. Ni rahisi kurubuniwa hata na hoja ambazo hazina kichwa wala miguu. Ukimdondoshea kuku vipande wiwili vya almasi na punje mbili za mahindi, ni wazi atashambulia punje za mahindi na kuiacha almasi. Atafanya hivyo kwa vile akili yake imeishia hapo. Hana la ziada. Hana habari na thamani ya almasi!


  Ndivyo watanzania wengi wanavofanywa na CCM. Uwezo wao wa mang'amuzi ya mambo umedumaa. Na CCM inatumia mwanya huo kuwarubuni. Waakati tunahangaika kujaribu kutupa macho huku na kule ili kujaribu kupeana mawazo juu ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu, na ni nani mzalendo wa kweli atakayetuvusha katika lindi la umaskini, CCM wanatupotezea lengo na kutuletea habari ya maisha ya mtu binafsi. Hawataki tuongelee almasi na dhahabu zetu zinazokwapuliwa . Wanataka uwezo wetu wa kufikiri uishie kwenye ngono.


  CCM wamekuwa wakimtuhumu Dr Slaa kwamba ana kimada. Hii ni hoja finyu sasa ukiilinganisha na hoja za ufisadi zinazotolewa, ambazo zinahitaji majibu. Wanachokifanya ni kujaribu kukwepa kujibu maswali na hoja za msingi kuhusu ufisadi. Baadala ya wananchi kufikiri na kujadili mambo yanayohusu uchumi wa taifa lao, waanze kufikiri na kujadili juu ya maisha ya mtu binafsi.


  Iwapo Dr Slaa ana mwanamke, shida iko wapi? Mbona ni ishara nzuri kwamba, walau ni mwanamme, tena dume la mbegu! Na hata ukimtazama Dr. Slaa usoni, unaona ana sura ya kiume! Anao uwezo wa kuoa! Na hilo haliwezi kuathiri uwezo wake wa utendaji kazi. Rais wa Afrika ya kusini anao saba. Dr Slaa anaye mmoja! Sijui iwapo Makamba ulikwishafika Swaziland. Kama hajafika namshauri ufunge safari ukajionee mfalme Muswati ana wanawake wangapi. Yeye binafsi, hatuna sababu ya kumchunguza, anajijua mwenyewe!


  Sasa tukianza kuchunguza maisha ya ndoa ya kila mtu, ni mwanamme gani atasimama? Wenye vimada ni wengi, hadi wanatia kinyaa. Viongozi wakuu wa CCM ndio wenyeviti wa ngono! Tuongelee dira na mwelekeo wa kiuchumi wa nchi yetu. Maswali muhimu yajibiwe, kuliko kukurupukia maisha binafsi ya mtu.


  Tunataka mtu wa kutuonyesha dira za kimaendeleo. CCM isituyumbishe na hoja za ngono ambazo hazimjengi mtanzania. Baadala ya kujibu maswali ya msingi kuhusu ufisadi, mnatupachika tongotongo za ngono ili kutupotezea lengo. Tunataka kupata majibu ya kufaa juu ya maswali kuhusu ufisadi unaofanywa na watu wachache, huku mamilioni ya watanzania wakihangaika kila kukicha. Ee Mungu inasue nchi yetu katika mikono ya mafisadi!


  Wewe mtanzania uliyeathiriwa na aina hii ya kimeta cha CCM, amka kumepambazuka! Achana na longolongo za CCM. Achana na akili za kuku kuishia katika punje za mahindi. Kura yako mpe Dr Slaa! Mwambie na mke wako, kura yake Chadema inaihitaji.


  Usisahau kumpasha habari na mama yako kule kijijini. Mwambie kura yake ni muhimu sana kwa Chadema. Kila la heri. Ubarikiwe sana!


  Mwenye maoni awasiliane nami kwa e-mail hii: mak.ralph[​IMG]yahoo.com

  Source: Coment in Mwananchi, 2010-9-6
   
 2. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapo suala si kuwa na vimada wengi kwani ingekuwa hivyo basi mapdri wa RC wangeongoza kwa kuwa masista wote waliopo parokiani ni vimada wao na ndio maana wakaamua kuunda vituo vya kulelea watoto 'yatima' kama vile msimbazi centre n.k.Ebu Jiulize hapa TZ kuna watoto wangapi wa mitaani wanazurura ovyo na hao mapadri wanawaona lakini hawawachukui na kwenda kuwalea(jibu kichwani mwako).Watoto wanaolelewa katika vituo hivyo ni wale wanaotokana na uzinzi wa mapdri na masista(watawa).Kwa kulijua hilo ndio maana makanisa mengine kama KKKT,EAGT,nk wachungaji wetu wote wameliona hilo na kuepusha hiyo dhambi ya uzinifu wakaamua kuoa.

  Nikirudi katika mada yako,huyo Padri anashutumiwa kwa kupora mke halali wa mwenzie(ushahidi soma magazeti ya leo) na si kuzini kwani ameshazoea kuzini kabla hajaliasi kanisa.Nakushauri uwe unatoa mada yenye kueleweka na si kudandia kama vile wadandia kipanya cha ubungo -migomigo,we unaujua uchungu wa mke?
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli hata umtetee vipi Dr Slaa mimi na wengi tulio na wake hatutakuelewa. Fikiria kama Josephini Mushumbusi angekuwa ni mkeo halafu Dr Slaa akamchukua. Viongozi hao wa Marekani uliowataja walichukua vimada ambao hawakuwa na ndoa. Kama uliangalia taarifa ya habari ya C10 jana jioni ungemhurumia yule bwana aliyeporwa mke na Dr Slaa. Mwambie tu Dr Slaa aje humu atueleze kilichotokea. Vinginevyo anayo kesi ya kujibu. Wanawake mabarabarani wako wengi tu.
   
 4. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Yule anayesema ameporwa mke na Dr. Slaa alikuwa wapi sikuzote asiseme hebu jiulizeni mtu keshatambulishwa na wazazi wake wamempokea mbona hakupinga toka mwanzo, eleweni huo ni mchezo mchafu wa CCM na huyo baba hakufikiria mara 2 kwenda kujilalidhisha mbele ya kadamnasi kisa vijisenti alivyopewa. Kama kweli ni Mkeo tangu aanze kuishi na Dr.Slaa mbona hukumfuata ulikuwa wapi siku zote???? Watu wameishi muda tu unasubiri kampeni zimepamba moto CCM imekaliwa kooni ndipo unajitokeza eti Josephine ni mke wangu halali, unajiabisha wee baba hela hatakupeleka popote ulizaliwa ukaikuta na utakufa unaicha, mlishatengana na mkeo sasa kapata mwingine unatapatapa ulimpomtenda ulimwona wa nini wenzio wakamsamini sasa roho inakuuma pole zako
   
 5. Mwanamosi

  Mwanamosi Member

  #5
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mke wa mtu Sumu...kama umeoa basi unajua inakuwaje hata pale unapoona njemba inamsololea mama watoto...hoja za ufisadi nadhani ziko kesi ambazo hazifai kuzizungumzia majukwaani so isitumike sana kama ndio mtaji wa kujitafutia kura...nadhani umefika wakati wa wagombea kuacha mambo binafsi na kujikita kwenye sera na ilani za vyama vyao...binafsi sifurahishwi na kuchafuana kunakofanywa na wagombea na wapambe wao...
   
 6. P

  Paul S.S Verified User

  #6
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  daah watu wamagazeti nao wameweka hadi picha ya harusi
  kweli dr ameshikwa pabaya
   
 7. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hizi zote ni jitahada za mafisadi kumchafua jemedari wetu. Kwa nini Rostam anatumia rasilimali zake kumchafua Dr Slaa?
  • Je lengo ni kuhakikisha kuwa watanzania wanachagua rais anayeheshimu ndoa yake? Kama ndivyo, mbona hatujasikia akigusia juu ya maisha binafsi ya Kikwete ambaye kwa hakika ameviona vitovu vya akina mama vingi kuliko madaktari bingwa wa akina mama wa Muhimbili?
  • Je lengo ni kuhakikisha CCM inabaki madarakani? Kama ndivyo, wengi tunajua kwa sababu gani. CCM na Kikwete wakiendelea kuwa madarakani Rostam na mafisadi wengine waendelee kutuibia bila ya wasiwasi wa kushitakiwa
  Yeyote atakayeingia kwenye mtego huu mchafu na kuamua kumuasi Dr Slaa kwa sababu ya maisha yake binafsi atakuwa ameridhia kuendelea kuibiwa na kudhalilishwa. Huu wote ni mchezo mchafu na hauna tofauti na zile propaganda zilizotumika kumchafua Dr Salm Ahmed Salm.

  Nina amini mtu yule aliyejitokeza kudai Josephine ni mke wake amelipwa hela nzuri sana kufanya hivyo na ataendelea kutumiwa ili kuendelea kuwahadaa watanzania, tuzikatae hila hizi za kishenzi
   
 8. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  CCM imefeli ndio maana imeanza kuingilia maisha ya watu badala ya kunadi sera zake
   
 9. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Katika hili Dr. Slaa amejichafua mwenyewe na anawajibika kwa matendo yake!!
   
 10. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45

  tunajua wote mnaoshabikia mada hii ya josephine ni walewaleeeeeee,
  Huyo baba alikuwa wapi siku zote?kwani ndoa inasuruhishwa kwenye vyombo vya habari au magazeti?acha hizo tumeolewa na wameoa.angeenda mahakamani kwanza na waandishi wazipate toka mahakamani.Tunajua mtumiieni akija shtuka kwenda mahakamani ndiyo mwisho .Hatudanganyiki mke haibiwi bwana kwani josephine ni mtoo mdogo......acheni ushabiki.
   
Loading...