Asimulia zawadi feki za Dk. Bilal

Asimulia zawadi feki za Dk. Bilal

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Egbert Mtui

Toleo la 355 | 28 May 2014

SIKU chache baada ya kuripotiwa kwa habari za wanafunzi kumi bora waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana kupatiwa zawadi feki, mmoja wa wanafunzi waliokumbwa na mkasa huo ameelezea kilichojiri siku hiyo.

Akizungumza na Raia Mwema, mwanafunzi huyo (jina tunalo) alisema siku hiyo (Mei 10/2014) wakiwa katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, walikabidhiwa bahasha ambazo zilikuwa na kipande cha karatasi ndani kilichokuwa na namba ya simu pamoja na maelezo ya jinsi ya kupewa zawadi hiyo ya pesa taslimu.

Alieleza kwamba baada ya kupiga namba ya simu iliyokuwa kwenye bahasha, waliitwa pembeni ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kulikofanyika hafla hiyo.

"Kulikuwa na kibanda ambapo ndani yake kulikuwa na wanawake wawili ambao walikuwa wakifanya malipo," alisema.

Alisema ya kuwa wanafunzi hao ambao waliambatana na wazazi na walezi wao, walilipwa shilingi 90,000 kila mmoja ikiwa ni pesa ya matumizi ya siku mbili, nauli ya kwenda na kurudi kulingana na kila mtu alikotoka na shilingi 250,000 kama sehemu ya zawadi waliyotakiwa kupewa.

Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, pamoja na vyanzo vingine vya habari, kiwango hicho cha fedha kilikuwa kinyume cha utaratibu uliokuwa umetangazwa hapo awali.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Elimu nchini, Profesa Eustella Bhalalusesa iliyosomwa mbele ya Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Ghalib Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, ilisema ya kuwa zawadi zitakazotolewa ni halisi na kwamba zimelenga kutekeleza kikamilifu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Taarifa hiyo ilieleza ya kuwa zawadi za shilingi 250,000 kila mmoja zingekwenda kwa washindi 10 wa sekondari na shilingi 150,000 kwa washindi wa shule ya msingi.

Aidha, Serikali ya China ilitoa shilingi milioni 25 ambapo kwa wanafunzi 100 waliofanya vizuri wangepata shilingi 250,000 kila mmoja. Halikadhalika kulikuwa na zawadi ya shilingi 500,000 zilizotolewa kama vocha ya vitabu na Mfuko wa Elimu Tanzania. (TEA).

Baada ya wazazi na walezi wa watoto kuona mambo yamekwenda ndivyo sivyo, walikuja juu na kuhoji juu ya tukio hilo na kutakiwa kuandika barua.

"Baada ya wazazi na walezi wa watoto hao kuja juu walitakiwa kuandika barua Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi juu ya mvutano huo, jambo ambalo lilifanyika, lakini ukweli ni kwamba mpaka sasa hivi hakuna chochote ambacho kimejibiwa, japokuwa nimesoma kwenye baadhi ya magazeti ya kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wamekwishapewa pesa hizo na hasa wa Dar es Salaam.
"Kama wameweza kuwalipa wa Dar es Salaam watashindwaje kuwalipa wa mikoani wakati madai ni yale yale? Siku hizi dunia ni kama kijiji. Mimi naona hapa kuna mchezo unafanyika. Mama yangu alijaribu kufuatilia lakini anasema ya kuwa kuna mlolongo mrefu," alisema mwanafunzi huyo katika mazungumzo yake hayo na Raia Mwema.

Hivi karibuni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alikiri kutokea kwa utoaji wa zawadi feki kwa wanafunzi hao, lakini pia akaomba radhi akiahidi kuchukua hatua kali za kinidhamu dhidi ya watendaji wote waliohusika katika tukio hilo.
 
kila anayepata nafasi ya kupiga anapiga tuu, almradi usile peke yako mengine yatajisolve mbele ya safari
 
alijiimbia muumini mwinjuma ''zawadi ni zawadi hata ukipewa jiwe chukuaaaaaa''
 
Zawadi haiwezi kuwa genuine huku ikiwa imetolewa na serikali feki. Nasema ni serikali feki kwa sababu kwa mwenendo wake, ni wazi imekosa uhalali wa kuongoza. Hasa tukizingatia hiyo elimu yenyewe ilivyo kwa sasa, sidhani kama ni halali serikali kumpongeza yeyote, wakati inajua wazi kuwa elimu inachukuliwa kisiasa zaidi na kwa sasa hata tofauti kati ya kufeli na kufaulu hakuna.

Vinginevyo sioni tofauti ni ipi, wakati waliofeli hawawezi kusoma wala kuandika na waliofaulu hawajui hata majina yao! Halafu katika mazingira ya serikali ya aina hiyo mtegemee zawadi genuine. Zawadi genuine zitatolewa na serikali genuine. Serikali feki itaendelea kutoa zawadi feki kwa matokeo feki.
 
I like it.kitufe tu kisingetosha kukupongeza kwa ulichoandika.u are genuine
 
Ikienda BUNGENI hiyo mtaambiwa hamjenda shule au elimu yenu itabidi kuhojiwa.
 
Hakika usanii umsezidi mno kwenye elimu ya nchi hii. Yaani hata Makamu wa Rais anaingizwa chaka na huu upepo utapita tu !
 
hata hivyo zawad ya fedha sio nzuri sana kwa wanafunz walitakiwa kupewa vitu kama laptops,nk ambavyo vingeonekana on the spot kuzuia uharifu na utapeli wa serikali sikivu.
 
daaah mzee wa utepe kashikishwa zawadi hewaaa...
Bilal bwana!!!
 
hata hivyo zawad ya fedha sio nzuri sana kwa wanafunz walitakiwa kupewa vitu kama laptops,nk ambavyo vingeonekana on the spot kuzuia uharifu na utapeli wa serikali sikivu.

Wangewapa chakavu
 
Zawadi haiwezi kuwa genuine huku ikiwa imetolewa na serikali feki. Nasema ni serikali feki kwa sababu kwa mwenendo wake, ni wazi imekosa uhalali wa kuongoza. Hasa tukizingatia hiyo elimu yenyewe ilivyo kwa sasa, sidhani kama ni halali serikali kumpongeza yeyote, wakati inajua wazi kuwa elimu inachukuliwa kisiasa zaidi na kwa sasa hata tofauti kati ya kufeli na kufaulu hakuna.

Vinginevyo sioni tofauti ni ipi, wakati waliofeli hawawezi kusoma wala kuandika na waliofaulu hawajui hata majina yao! Halafu katika mazingira ya serikali ya aina hiyo mtegemee zawadi genuine. Zawadi genuine zitatolewa na serikali genuine. Serikali feki itaendelea kutoa zawadi feki kwa matokeo feki.
Based on reality.
Good dude!
 
Daaaah kweli bongo noma, watu hawa ridhiki tu hadi za wanafunzi wanatafuna tu.
 
Wizara na watendaji wake wengi Ni walewale wapigaji na wakubebana. Nani atamfunga paka Kengele? Isha toka hiyo
 
Back
Top Bottom