ASILIMIA 90% YA WAHITIMU WALIOFANYA VIZURI (TOP PERFORMERS) SHAHADA YA KWANZA NI JOBLESS

mtulivuu

Member
Dec 18, 2015
60
24
Hii imethibitishwa na wanafunzi wenyewe katika sherehe iliyoandaliwa na jumuiya ya wanafunzi tanzania iliyokuwa na takriban ya wanafunzi 60 waliofanya vzur katka vyuo vyao.Sherehe hyo ilifanywa Dodoma ambapo Mnamo tar 20 ,Apr walikaribishwa bungeni na tar 23 ndio sherehe hyo ilifanyika na kuvishwa majoho na kupewa vyeti mgeni rasmi alikuwa NAIBU WAZIRI.....wahitimu hao waliwasilisha malalamiko yao kwa mgen rasm kwamba asilimia 90% kati yao hawana kazi(jobless)......je n nn maoni yako katka hli?????
 
...hahaahaaa "asilimia 90 ya walio perform vizuri wanalalamika ma jobless!", huku ma PhD nao wanalia wakumbukwe!, hii elimu ya Tanzania sijui ililaaniwa na nani!
 
Tatizo Tanzania ni nchi isiyo na mipango. Ni nchi pekee Duniani isiyojua kwanini inasomesha watu wake. Hakuna Kiongozi wa Tanzania anayetambua hasa faida za kuwa na Taifa la watu walioelimika ni nini.

Kila mtu anadhani kusoma na kupata vyeti ni kufanya siasa. taifa litaendelea kwa kutambua michango ya wataalamu mbalimbali siyo wanasiasa. Bado tuna safari ndefu sana ya kwenda ili kupata maendeleo ya kweli.
 
Hii inatokana na kua Mungu aliwapa akili za kukariri na kujibia mitihani. "Walipewa akili za darasani" hawakupewa akili za Maisha.

Kuna tofauti kubwa kati ya akili za darasani na zile za maisha. Wengine wanatafuta degree hizi kwa ajili ya kupanua uelewa tu. Kingine kibaya ni sisi watanzania kukaa darasan tukiwa na Imani kua tukimaliza shule tukaajiriwe.

Cha msingi sana tupige makelele vyuoni wawawekee vijana wetu elimu au kozi maalumu ya kujitegemea au ujasiriamali.
 
Hii inatokana na kua Mungu aliwapa akili za kukariri na kujibia mitihani. "Walipewa akili za darasani" hawakupewa akili za Maisha.

Kuna tofauti kubwa kati ya akili za darasani na zile za maisha. Wengine wanatafuta degree hizi kwa ajili ya kupanua uelewa tu. Kingine kibaya ni sisi watanzania kukaa darasan tukiwa na Imani kua tukimaliza shule tukaajiriwe.

Cha msingi sana tupige makelele vyuoni wawawekee vijana wetu elimu au kozi maalumu ya kujitegemea au ujasiriamali.
Mfumo wa kujitegemea utajengwa na jamii kuanzia ngazi ya familia na sio shuleni pale mtu huenda kuongeza maarifa baada ya kupata mengine kwenye jamii.
 
Mimi na GPA yangu 2.5 nipo shamba nalima,na kibiashara kanasogea vizuri tu ..........soon naagiza corolla ya kutembelea .....,nikisubiri tgsd wakati GPA yangu michoso nitaishii kwa Shemeji mpaka lini
Mali inapatikana shambani
 
Mtu mnamaliza chuo karibia darasa zima mna GPAya 4.6..... kichwani hamna kitu... kwanini usikose kazi
 
Ndiyo maana nimekataa kusoma masters mpka niitumie kwanza hii degree yangu niridhike wanawaza kuwezeshwa kweli hao ni zero mind.Vyakufanya vyoteeeeee wao wanawaza kupewa ajira dah!Haya majipu
 
just go and read the book of robert kiyosaki;why A student work for C student and B student work for the government
 
huo ni uongo.... labda kama gpa zao za kununua..

watu wanaowahi kupata kazi ni best student..

kwanza wanabakizwa vyuoni kufundisha...

kama una gpa za kukariri darasani interview unaonekana mweupe lazima ukose kazi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom