streat Anthem
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 395
- 476
Natanguliza shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kunipa uhai na nafasi ya kipekee ili niweze kushare na ninyi mawili matatu
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza hapo juu, kwa utafiti wangu nilioufanya nimegundua asilimia 80 ya Watanzania hawako serious kwenye mambo mengi sana na ndio maana nchi yetu inaendelea kwa mwendo wa kinyonga kwa kuwa watu wake wamekosa usiriasi
Tukianza mashuleni wanafunzi wengi wa hapa Tz hawako siriasi kabisa, hawajui hata shule inataka nini, unakuta mtu hata hajui hata lengo lake la kua shule na mwisho wa siku wanaishia kufanya zinaa na kupeana mimba huku wengine wakiishia kwenye pombe, bangi na sigara
Bila kuwasahau walimu wao pia hawako siriasi kabisa na wengi hawajui majukumu yao. Wanafundisha kwa ubabaishaji wa hali ya juu na kuzifanya akili za wanafunzi kudumaa sana
Pia malezi katika familia zetu ni taabu tupu. Wazazi hawako siriasi katika malezi kabisa, hakuna ushirikiano kati ya Baba na Mama, mfano Baba akimkanya mtoto Mama anakua upande wa mtoto hii inaishia kutengeneza chuki tu kwa upande mmoja. Pia wazazi hawawaandai watoto kujitegemea kifikra na kujitambua yani huku mtaani ni balaa, watoto hawana maadili kabisa na wazazi wanashangaa shangaa tu. Sijui wanaandaa watu wa namna gani?
Bila kusahau Serikali nayo haiko siriasi katika utendaji wake kwa kiwango kikubwa, sijui wanahusi wanaongoza watu wa namna gani. Siasa ya uongo, chuki na matabaka yanazidi kuchukua nafasi kubwa, Serikali haiko siriasi na rasilimali zetu, haiko siriasi na mipango ya maendeleo, hawako siriasi na hali ya maisha ya wananchi na pia hawako siriasi na demokrasia. Sijui wanafikiria nini hasa?
Nimalizie na Wananchi wa Tanzania nao hawako siriasi kwa kiwango kikubwa, watu hawafanyi kazi wala kujituma na kuhakikisha wanapata maendeleo yao binafsi wanasubiria wawekewe matonge midomoni
Maafa na matatizo yakitokea huchukua kama fursa za kufanya mizaha ya ajabu kwa mfano mauaji yanayoendelea Kibiti badala ya wananchi kulaana vitendo ivyo na kuhakikisha wanashirikiana na serikali ili kumaliza matatizo basi ndo mizaha inachukua nafasi ya kutosha.
Sijui wanahisi nchi itaendelea kwa mizaha?
NB: katika suala la mapenzi na mahusiano watu hawako siriasi kabisa! Watu hawathamini ndoa zao,kuzini nje ya ndoa imekua sifa, wasichana hawathamini wala kujua thamani zao, watu wanadanganyana na kuchezeana mpaka basi, ngono inafanywa kua lengo kuu la maisha! Sijui tatizo ni nini?