Asilimia 3 ya TRA kiini macho?

Daniel Mjema

Member
Jul 23, 2007
77
84
20160414_135819-1.jpg

TRA inahamasisha raia wema kutoa taarifa za wakwepa kodi kwa ahadi watapewa 3% ya pesa inayokombolewa lkn kumbe nyuma ya pazia mtu hawezi kulipwa zaidi ya sh20 milioni hata kama atafichua mabilioni.

Sasa kwanini wanatangaza wanatoa 3%? Naomba tujadili hili tukirejea na attachment niliyoiambatanisha ya majibu ya TRA
 
Ni kiini macho kwakuwa ni mchakato mrefu unaojumuisha mambo ya kisheria mpaka upate hiyo asilimia 3 yaani mpaka ithibitike kiwango alichokwepa na aadhibiwe ndio nawe upewe chako
 
TRA inahamasisha raia wema kutoa taarifa za wakwepa kodi kwa ahadi watapewa 3% ya pesa inayokombolewa lkn kumbe nyuma ya pazia mtu hawezi kulipwa zaidi ya sh20 milioni hata kama atafichua mabilioni. Sasa kwanini wanatangaza wanatoa 3%? Naomba tujadili hili tukirejea na attachment niliyoiambatanisha ya majibu ya TRA
Nilisoma jamaa mmoja alitoa taarifa kwa tra hakupewa chochote matokeo yake aliishia kupelekwa polisi osterbey.
Hii nchi ndio maana watu wanakosa uzalendo kwa upuuzi huu,
Mtu amejitolea muhanga kutoa taarifa zenye maslahi ya nchi lakini mchango wake unapuuzwa
 
Mkweli alikuwa mzee wa kirachacha tuu yeye aliahidi 10% na alitoa bila figisu
 
Back
Top Bottom