Asilimia 15 ya Bodi ya Mikopo kuanza kukatwa kwenye mshahara ghafi(basic) kuanzia mwezi Januari

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Ni baada ya Rais Magufuli kusaini mabadiliko ya Sheria mwezi Novemba 2016.

IMG_2360.JPG
 
Weekend yangu ime haribika baada yakukutana na hii kitu jamani,
1484325304673.jpg


Baba , mkuu wetu wengine tulishaa anza kulipa deni mwaka watano huu, tunakaribia kumaliza , nakuomba Baba makato yamekua mengi na asilimia kubwa kubwa mpaka tunachanganyikiwa sisi watumishi wako!!!

Molari ya kazi Baba inashuka kila kukikucha, tunaamini wewe nikiongozi wa wanyonge, bas tunaomba huruma yako kuu Baba itufikie sie tusio pandishwa madaraja Baba, tusio na posho Baba, tusio na semina wala warsha,

Mbaya zaid tuka kopa ili tujenge vibanda, maana kwa necha ya kazi yetu ni ngumu kujenga mpaka ustaaafu,

Baba, misongo ya mawazo sasa inaanza kuwa mikubwa baba, tunakatwa bima, matibabu ovyo baba, tunakatwa mifuko ya jamii baba, tunakatwa vyama vya wafanyakazi baba, umaskini wetu na familia zetu kusoma kwa kutumia hii mikopo baba ndo utuponze kweli???

Mi naamini basi sio mbaya ukikata hiyo asilimia 15lakini tunaomba bas utuongezee increment ili tuwe vizuri eee baba!!! Kwa hali hii nawaza nirudi saloon kusuka nywele baba, maaana ni wazi kazi itanishinda, maaana mume ninae ILA na yeye ni kama Mimi TU, msururu wa ndugu na matatizo kama uzijuavyo familia za kiafrika!!!

Sijawai kuwa mpiga dili niliridhika na kamshahara kangu, sasa kukakata ten Baba kanabaki kadogo mpaka aibu kujiita mtumishi, nafwa baba, nafwaaaaaaa, najua siko Mimi TU, tupo wengi baba, twafaaaaaa! Uruma yako ni muhimu baba tunakuomba kupitia utukufu wako!!!

Wako katika kazi, mtumishi wako mtiifu baba,

MARIETHA JOHN!!!!
 
We binti yoga , acha porojo, huyu hapana. Kama anaweza kuwakebehi, kuwasimanga wafiwa, acha tu. Mtu analala nje unamdhihaki
Sio porojo, mi najua atatuskia hakuna asiye taka kulipa sema kiasi cha pesa kinacho taka kukatwa nikikubwa kulingana na kipato tunacho pokea so ni kumuoba atusikie. Atutatulie hili jamni!!!
 
Sio porojo, mi najua atatuskia hakuna asiye taka kulipa sema kiasi cha pesa kinacho taka kukatwa nikikubwa kulingana na kipato tunacho pokea so ni kumuoba atusikie. Atutatulie hili jamni!!!
Endelea kuomba sana!
 
Ila kusema kweli, 15% ni kubwa sana sana, na wabunge wa CCM sio watu kabisa, mm ni CCM, ila hili wameshindwa hata kujua ni hatari kwa maisha ya mtumishi, sbb sasa hv tu makato ya mshahara almost yanafikia 36%...

Sasa ukichukua 36% + 15% = 51% ya basic salary

Na wabunge wanaona tu, sbb wao haiwahusu, na wakapitisha..!!

Watumishi waliosoma kwa mikopo watumia sana saanaa..!! Sbb utakuwa unakatwa karibia nusu mshahara baada ya makato yako yote..!!

Hili ni janga kuu kwa walio na mkopo, labda Mh. Rais aguswe na nani moyoni ashtuke na aombe irekebishwe, of which sioni kama hilo lipo, atleast wangeeka 8% kama awali..
 
Back
Top Bottom