Asilimia 100% Leo mke wangu kanisaliti

Asilimia 100% Leo mke wangu kanisaliti

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
2,255
Reaction score
1,565
Heshima kwenu wakuuu,

Naandika hapa na maumivu ya moyo makubwa sana mke wangu kipenzi yuko Dar es salaam mimi niko mkoani.

Leo toka mchana mke wangu kanambia simu yake haina charge umeme umekatika lakini kitu cha kushangaza simu zake zote mbili zimezima kwa wakati mmoja toka huo mchana mpaka saizi.

Na kibaya zaidi anaishi Kinondoni kwa Manyanya na kila nikiulizia majirani naambiwa umeme upo toka asubuhi na nimetuma mtu mpaka hapo nyumbani kuna umeme.

Kibaya zaidi nimeingia kwa page yake Fb nimekuta mwanamke anamshambulia mke wangu kuwa aachane na bwana wake.

Iam passing through hell right now na bado simpati mke kwa simu.Maumivu niliyonayo is only God knows.
 
matatizo ya distance relationships ndo haya, kila wakati kuhisi hisi tu!!
 
Polee ngoja atapopatikana atakupa sabbu ya msingi.. Usianze kujipa majbu mwenyew, presha itakusumbua bure
 
Heshima kwenu wakuuu
Naandika hapa na maumivu ya moyo makubwa sana..mke wangu kipenzi yuko Dar me Niko mkoani..Leo toka mchana mke wangu kanambia simu yake haina charge umeme umekatika lakini kitu cha kushangaza simu zake zote mbili zimezima kwa wakati mmoja toka huo mchana mpaka saizi...na kibaya zaidi anaishi kinondoni kwa manyanya na kila nikiulizia majirani naambiwa umeme upo toka asubuhi na nimetuma mtu mpaka hapo nyumbani kuna umeme..
Kibaya zaidi nimeingia kwa page yake fb nimekuta mwanamke anamshambulia mke wangu kuwa aachane na bwana wake...am passing through hell right now.. Na bado simpati mke kwa simu..
..Maumivu niliyonayo is only God knows...

Umenikumbusha miaka kama nane iliyopita jamaa wawili walikuwa Dar Es Salaam, mmoja akamtuma mwingine(akisema
Jamaa 1: Naomba unichukulie mzigo fulani unipitishie nyumbani maana niko safari Nairobi narudi kesho.

Jamaa 2(Nate akamjibu): Dah! Huku ' bongo' Kuna bonge la mvua sasa hivi imenyesha toka asubuhi, na hailekei kukatika leo.

Funny thing is, wajamaa wote walikuwa hapo hapo Kijitonyama!

Back to the topic sasa:
Pole, lakini mbona waja huku badala ya kum_confront mkeo? Yuko Dar kikazi au? Pengine ndipo wamekuwa wakikutania huku!

I think it is, 'Only GOD knows'.
 
Wewe kimaumbile ni mwembamba sana lakini mtu akikuangalia una mwili wakunenepa ila umegoma.

Halafu vimifupa juu ya mashavu vimekutoka. Pia macho yako yapo kama unakerwa na moshi.

Bisha kama haupo hivyo! !

Huo ndio muonekano wa Mtu mwe wivu wa kimapenzi uliopitiliza. Wengi hawanenepi sababu ya hisia tu.
 
Aisee mmh hapa ni pagumu sana aisee...pole sana jaribu kumeza pain killer ili ulale utayajua kesho japo najua ni ngumu hiyo yaani now unakua unawaza yale mautundu yote anapeewa mtu na huenda wanaenda mbali zaidi ya mnapoishiaga nyie c unajua muibaji anavyotaka kukomesha. Ndugu yangu pole sana na usiku mwema
 
Pole kijana ni changamoto tu za maisha hamna namna inabidi upambane nazo tu
 
Wewe kimaumbile ni mwembamba sana lakini mtu akikuangalia una mwili wakunenepa ila umegoma.

Halafu vimifupa juu ya mashavu vimekutoka. Pia macho yako yapo kama unakerwa na moshi.

Bisha kama haupo hivyo! !

Huo ndio muonekano wa Mtu mwe wivu wa kimapenzi uliopitiliza. Wengi hawanenepi sababu ya hisia tu.

Mkuu me na kg 98 ...imagine mwenyewe nilivyo
 
Ndugu ebu tuliza nafsi yako..wanawake wanamitihani sana...piga moyo konde kama unajiskia kuachana nae fanya hvyo soon...wala usisikilize maneno ya mtu wala usisikilize maneno matamu atayokupa...ni ukweli kwamba inauma sana kuishi na mtu alafu anakua msaliti...kaka utaamua kumsamehe basi msamehe kiroho safi tu maana hapa tunashauri tu lakin maamuzi ya mwisho unayo mwenyewe.....jaribu kutulia na kupoza moyo akwambie nini tatzo lakin hapo inabidi uwe makin na ikiwezekana kaa na mke wako karibu ndugu..
 
Umenikumbusha miaka kama nane iliyopita jamaa wawili walikuwa Dar Es Salaam, mmoja akamtuma mwingine(akisema
Jamaa 1: Naomba unichukulie mzigo fulani unipitishie nyumbani maana niko safari Nairobi narudi kesho.

Jamaa 2(Nate akamjibu): Dah! Huku ' bongo' Kuna bonge la mvua sasa hivi imenyesha toka asubuhi, na hailekei kukatika leo.

Funny thing is, wajamaa wote walikuwa hapo hapo Kijitonyama!

Back to the topic sasa:
Pole, lakini mbona waja huku badala ya kum_confront mkeo? Yuko Dar kikazi au? Pengine ndipo wamekuwa wakikutania huku!

I think it is, 'Only GOD knows'.

Mkuuu mke anauma sana..jf no sehemu ambayo watu wanaweza wakakufariji au ukapokea maumivu..but pia naweza kutana na comment ikanambia umeme kweli haukwepo japo vyanzo vyangu vyote vimenambia kuna umeme..me nimekuja kikazi mkoa
 
Mazingira yameshajitengeneza kuwa umesalitiwa, haijalishi kama ni kweli au lah.....
I think you are going through all kinds of emotions right now and it is difficult to even think straight na nafikiri hadi kuna some reaction physically.....
I mean, mfano maumivu kifuani ikiendana na mapigo ya moyo ya kasi, tumbo linakusokota labda, kama hujakwenda msalani hadi sasa, sijui.
Kama una hali niliyoelezea ni vizuri kuhangaikia your well being kuliko vitu ambavyo hauna uwezo navyo.
Take care of yourself, kama una mtu wako wa karibu mpigie for support halafu mengine yatajulikana tu.
 
Hapo nadhani tayari kichwani una movie yote jinsi anavyobanjuliwa kitandani, aisee pole sana jikaze fanya utafiti halafu ufanye maamuzi magumu kiongozi halafu kinondoni sio mahala pa kuacha mke

Your advice noted mkuu
 
tafuta mchepuko wewe acha ujinga dawa ya mwanamke ni mwanamke mwenzake na dawa ya moto ni motoo
 
Back
Top Bottom