Asili ya Msemo 'kula bata'

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,900
Reaction score
37,675
Wakati msemo huu unaanza kutumika, watu walikuwa wanasema " Tunakula Bata ". Sasa hivi wameongeza na msemo mwingine, wanasema " Tunakula bata mpaka kuku wanaona wivu. Hawa hawajui asili na neno tunakula bata. Tunakula " Bata'. Maana yake ni tunakula "butter" yaani " Siagi " na sio bata ndege.
 
Unapajua Ubatani?? Mabaharia wa zamani nchi inayoitwa Turkey walikuwa wanaiita ubatani. Turkey ni bata mzinga ambae Ulaya hususani UK analiwa siku ya Christmas. Kwa maana ingine ndio chakula cha sherehe kubwa, kwahio kula starehe/sherehe kubwa ndio kula Bata
 

US wanakula bata mzinga on Thanks Giving Day.

Dah, nimepata pata picha kwa mbali maana ya kula bata
 
Msemo ulianza na Kula Kuku kwa Mrija, Watu wakabadili ikawa kula bata...
 
Matokeo ya kuchanganya lugha hayo. Kwanini wasingesema siagi? Na siagi au butter inawakilisha nini hasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…