ASILI YA JINA LA KAWE

ASILI YA JINA LA KAWE

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
19,151
Reaction score
43,102
IMG_20240615_153320_774.jpg

Ng’ombe wakiwa wamewasili katika kiwanda cha Tanganyika Packers Kawe tayari kwa kuchinjwa na baadaye nyama kusindikwa na ngozi kuandaliwa kwa matumizi mengine.

Kisha baadaye mambo yakaw yale yaleeeee...kiwanda kikajifia zake tu, sababu hazijatajwa.....😃

Mji wa Kawe ulianza tangu miaka ya 1908. Kipindi hicho mji ulikuwa lilipo eneo la Makaburi ya Mzimuni (Mwai Kibaki road). Kufikia miaka ya 1960 baada ya kuanzishwa kwa kiwanda cha Tanganyika Packers palikuwa na njia ya kupeleka ng'ombe kiwandani, ambayo wazungu waliita "cow way" wakimaanisha njia ya ng'ombe. Wamatumbi wakashindwa kulitamka neno hilo na badala yake wakatamka KAWE.

Vitongoji vilivyokuwa vinapakana na Kawe kwa kipindi hicho vingi vilitokana na wakazi mashuhuri wa maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na Kwa Mussa Hassan ambako ni Msasani, Michael Chain ambako sasa ni Mikocheni. Umbwelani ambako sasa ni pahala ilipo hosteli ya JWTZ, pia kwa Wakwama ambako sasa ni Ukwamani na upande wa Kaskazini walipakana na mashamba ya mkonge ya Asamali ambako sasa ni Mbezi Beach.
 
View attachment 3018014

Ng’ombe wakiwa wamewasili katika kiwanda cha Tanganyika Packers Kawe tayari kwa kuchinjwa na baadaye nyama kusindikwa na ngozi kuandaliwa kwa matumizi mengine.

Kisha baadaye mambo yakaw yale yaleeeee...kiwanda kikajifia zake tu, sababu hazijatajwa.....

Mji wa Kawe ulianza tangu miaka ya 1908. Kipindi hicho mji ulikuwa lilipo eneo la Makaburi ya Mzimuni (Mwai Kibaki road). Kufikia miaka ya 1960 baada ya kuanzishwa kwa kiwanda cha Tanganyika Packers palikuwa na njia ya kupeleka ng'ombe kiwandani, ambayo wazungu waliita "cow way" wakimaanisha njia ya ng'ombe. Wamatumbi wakashindwa kulitamka neno hilo na badala yake wakatamka KAWE.

Vitongoji vilivyokuwa vinapakana na Kawe kwa kipindi hicho vingi vilitokana na wakazi mashuhuri wa maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na Kwa Mussa Hassan ambako ni Msasani, Michael Chain ambako sasa ni Mikocheni. Umbwelani ambako sasa ni pahala ilipo hosteli ya JWTZ, pia kwa Wakwama ambako sasa ni Ukwamani na upande wa Kaskazini walipakana na mashamba ya mkonge ya Asamali ambako sasa ni Mbezi Beach.
Kabla ya hivyo cow way palikua panaitwa je. Au palikua hapana majina kabisa?
 
Back
Top Bottom