Asili ya familia ya Hayati Mzee Karume

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,750
4,958
Historia inavyosema, Marehemu MzeeKarume alikuja Zanzibar na wazazi wake wakitokea Malawi, walikuwa ni wananchi wa Malawi, lakini wakati huo Tnaganyika, Zanzibar na Maliwa zilikuwa chini ya mamlaka ya Uingereza ( ama makoloni ya UK ).

Jee Familia ya akina Karume walikuwa watu wenye asili ya kibantu, kabila la : Chewa, Nyanja, Yao, Tumbuka, Lomwe, Sena, Tonga, Ngoni au Ngonde, tukijua kuwa kabila kubwa zaidi Malawi ni kabila la Chichewa (Chewa)
 
Mimi nimepata kusikia kwamba Karume ni Mmanyema, akitokea Kigoma zamani sana.

Katika Makabila ya Wamanyema (Wabwali au Wanyakaramba) yapo majina ya Karume hasa huko Ujiji.

Wamanyema asili yao ni Congo mashariki na walitoka huko zamani sana hata kabla ya Ukoloni wa Waarabu Afrika ya mashariki, walipitia Kigoma- ujiji, Tabora hadi Dar na baadhi wakaingia Zanzibar ambao ndio hao akina Karume, hapo Dar ndio hao waliojenga Msikiti wa Manyema.

Kifupi ni kwamba Karume ni Mmanyema kutoka Magharibi ya Tanzania, kusema kwamba Karume ni Mmalawi ni ngumu sana kuwa kweli.
 
Zipo habari kwamba jina karume ni la baba wa kufikia ambae alikua mkongo, ila asili yadaiwa ni malawi, nadhani hata akina amani kuna kipindi walipelekwa Malawi.
 
Mimi nimepata kusikia kwamba Karume ni Mmanyema, akitokea Kigoma zamani sana.

Katika Makabila ya Wamanyema (Wabwali au Wanyakaramba) yapo majina ya Karume hasa huko Ujiji.

Wamanyema asili yao ni Congo mashariki na walitoka huko zamani sana hata kabla ya Ukoloni wa Waarabu Afrika ya mashariki, walipitia Kigoma- ujiji, Tabora hadi Dar na baadhi wakaingia Zanzibar ambao ndio hao akina Karume, hapo Dar ndio hao waliojenga Msikiti wa Manyema.

Kifupi ni kwamba Karume ni Mmanyema kutoka Magharibi ya Tanzania, kusema kwamba Karume ni Mmalawi ni ngumu sana kuwa kweli.
Event

Hii ndo history inayofahamika
 
Amaan ameshawahi kupelekwa Malawi akiwa mdogo
 
Amaan ameshawahi kupelekwa Malawi akiwa mdogo

Malawi kuna makabila mengi, sasa jina KARUME linapatikana katika kabila lipi katika hayo makabila ya huko??, isitoshe Malawi katika zama hizo kupata Muisilamu ilikuwa ni shida kubwa, "Abeid na Amani" hayo majina mawili yana asili kiarabu na yapo sana miongoni mwa Waisilamu.

Angalia majina (surnames) za Wamanyema (Wabwali, wanyakaramba na Wagoma):-

Kaluona, Kainuza. Kasanga, kairo,Kafungo, Kaluta, kazema,Kakolwa, Karume, kaila, nk japo yapo majina Mengine ya hayo makabila hayaanzi na silabi "Ka" lakini mengi yanaanza na "ka".

Kama nilivyosema hapo awali Wamanyema walitoka Kongo DRC zamani na wakaingia Kigoma na kiasi fulani Kagera, Rukwa na Tabora, idadi yao kubwa ilifika hadi Dar na wachache wakaingia Unguja. Ni vigumu sana kumpata mmanyema asiyekuwa Muisilamu ila wapo wasiokuwa waisilamu ila ni wachache sana, mfano Ujiji inao wamanyema wengi idadi yao kubwa ni Waisilamu na huko majina ya Karume yametamalaki hadi hii leo.

Ndiyo maana nasema, Marehemu Abeid Amani Karume ni "Mmanyema", hata nilipata kumsikia Dr Salim Ahmed Salim akihojiwa na akasema (kama nakumbuka vyema) yeye DR, anayo damu ya kimanyema katika "Geneology" yake kuna mzazi wake mmoja ni mmanyema, hii maana yake ni kwamba Wamanyema kama ilivyokuwa kwa makabila mengine kama wasukuma na Wanyamwezi waliingia Unguja zamani sana kutoka Tz Bara, kama ilivyo kwa Wadigo walivyoingia Pemba kutoka Tanga.

Au vinginevyo atakuwa na asili ya Mmanyema aliyeingia Malawi kutoka Congo DRC.

that's my take.
 
Back
Top Bottom