Asha Rose Migiro Kutemwa UN? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asha Rose Migiro Kutemwa UN?

Discussion in 'International Forum' started by Amosam, Aug 21, 2009.

 1. Amosam

  Amosam Senior Member

  #1
  Aug 21, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ban Kim-Moon kumtema Asha Rose Migiro?  [​IMG]
  Dr. Asha Rose Migiro​
  Mwanadiplomasia na balozi wa Norway kwenye Umoja wa Mataifa, Bi. Mona Juul ameiandikia wizara ya mambo ya nchi za nje ya Norway, taarifa ya siri jinsi katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Kim-Moon alivyoshindwa kufanya kazi. Hayo yaliandikwa jana na gazeti la hapa la kila siku, Aftenposten kuwa Ban Kim-Moon hajui kufanya kazi, haelewani na wafanyakazi walio chini yake na ana hasira za mkizi. Kwenye taarifa hiyo, inaonyesha kuwa Ban Kim-Moon haelewani kabisa na msaidizi wake, Bi. Asha Rose Migiro na tetesi kuwa huenda Ba Kim Moon akamtema Bi. Migiro kama msaidizi wake.
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duh ngoja ziendelee kuwa tetesi
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kashughuli kapo!!! Ila kama ilivyo tetesi nasikia B-K hapendi waafrika?? Ila mbona alimsifia sana alipoulizwa!!!! Dunia ina mambo, lukumba lukumba!!!!
   
 4. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Ni vigumu kuamini hili! After all alipomteua alijua ni African..
   
 5. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2009
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Je, nini kitatufanya tusiamini kuwa huu ni umbeya tu??? Vinginevyo shusha ushahidi wako hapa.
   
 6. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyu Mama ni mchapa kazi hodari. Ni mwiba kwa wale wasiopenda maendeleo hapo UN.
   
 7. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  ila sio tatizo hata akitemwa bado watanzania tunamuihitaji sana hapa nyumbani aje kusukuma gurudumu la maendeleo
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Tetesi, tetesi, tetesi.....tetesi
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Najua baadhi ya wazungu hawapendi watu wengine wasio wazungu waongoze UN kwa hiyo lazima wanakuwa na fitna za hapa na pale kama hivi
   
 10. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ila yaliyosemwa na huyu balozi wa Norway kuhusu katibu mkuu wa UN sio mara ya kwanza kuyasikia. Wafanyakazi waandamizi wa UN wasema hawajapata kuwa na bosi "docile" kama Ban Ki-Moon. Sasa Asha Rose hata kama unajua kazi kwa vile Bosi wake yuko vile hata Asha Rose anakuwa -affected. Of course akitemwa (baada ya muhula wake wa kwanza kuisha) Ban Ki Moon na Asha itakuwa bye bye!
   
 11. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Lisemwalo lipo............
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  naona wikend imechelewa sana leo
  sitaki kuamini hiyo ishu mpaka ushahidi uje hapa.
   
 13. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ambalo alishindwa kulisukuma alipopata nafasi hapo nyuma sio????
   
 14. Van Walter

  Van Walter Senior Member

  #14
  Aug 21, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  aje hapa bi asha tumpe urais
   
 15. araway

  araway JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2009
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 498
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45

  kwa sifa zipi?
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Aug 21, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  U Rais wa nchi au uoi mkuu? huyu si ndio yuko kile chana kilichoema kupitia mkuu wao wa propaganda kuwa kwa uwa waislamu wameambiwa waanzishe mahakama ya kadhi bila kuihusisha serikali ,then mwakani watasema mahakama ya kadhi imeanzishwa nahivyo ilani imeekelezwa....... pole Tanzania japo nakupenda kwa moyo wote
   
 17. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,081
  Likes Received: 1,727
  Trophy Points: 280
  Kidatu nadhani, pamoja na wewe waswahili wengi hamjui kinachojiri UN. Asha-Rose Migiro aliishaonyesha uwezo mdogo kiutendaji nadani ya UN. Rejea post yangu ya March mwaka huu (2009):

  Migiro is very weak in terms of leadership capacity. She was about to be dropped and sent home from the UN post last year if not pleaded by the Government of URT, supported by UK Government on condition that MIGIRO's term be extend for one year only (2009) instead of 2 years. So she will be back on her early retirement to Dar next year.
  She has failed the UN and Tanzania.
  Please do not count on her.
  Like Kikwete, Migiro is another 'uchochoro' and the fertile facility for Mafisadis, period.
   
  Last edited: Aug 21, 2009
 18. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..hiyo barua aliyoandika na Balozi wa Norway iko wapi?

  ..OK, tusubiri Migiro arudi nyumbani hiyo 2010.

  ..kama amefanya kazi nzuri or not sitarajii atumikie nafasi hiyo kwa vipindi viwili.

  ..UN siyo sawa na CCM.
   
 20. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani hapa mama yetu hatumtendei haki. Ok..assume huyo balozi wa Norway kaandika..lakini si kasema kwamba Ban Ki-moon ndo incompetent? sasa mama anaingiaje jamani? boss ndo mwenye matatizo..au mnafikiri kwamba mama akitoka pale yule bwana atakuwa successful? Well I dont know much..ila nimeshasoma somehwere kwamba BAN KWELI HAYUKO AGGRESSIVE katika utendaji wa kazi. Ila ningependa Ban ahukumiwe kama yeye siyo huyu mama. Ni kitu gani mama angefanya na hakufanya? What was the expectations? Jamani Africa yetu matatizo hayakuanza leo. Infact mimi na wewe tuna nafasi kubwa ya kuibadilisha nchi yetu kuliko kutegemea watu kama akina Migiro.

  Kikubwa ninachoona hapa..ni kwamba binadamu tumezoea status quo..tukiona mtu ambaye siyo mwenzetu anaingia kwenye "inner circle" tunajiuliza maswali mengi. Kikubwa wengi wetu/wao wanaosema kwamba mama ni incompetent ni kwasababu wanaona hakustahili kuwa alipo. Maana kuna mabureacrats wengi wamekaa UN miaka kibao mpaka leo wanapiga marktime tuu! SASA wanashangaa mama hana "experience" harafu ni second in command.

  Well, simhukumu wala kumtetea mama, lakini nadhani with all fairness...Migiro is just a international civil servants kama wengine. Ban akiamua kumdrop ni uamuzi wake after all ndo alimpa kazi. Jamani kwani leo kikwete akimfukuza kazi Pinda..who will complain? Ila tusitafute visingizio. Mimi kwa kweli sikuwa na expectation yoyote kwa mama Migiro. Let her do her job. Mda wake ukiisha aje tuijenge nchi yetu-kama bado inajengeka! Infact nadhani Hasheem Thabeet anaweza kuwa balozi wetu mzuri kuliko Migiro. Maana Hashim anadeal na michezo ambayo wa-US wanapenda..na wale ndo wenye hela za utalii. I dont think if there is any serious American (save few politicians with their national interests) who care about UN as a body.
   
Loading...