Asha Bakari aanguka ghafla Dodoma

Asha Bakari aanguka ghafla Dodoma

mzenjiboy

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Posts
907
Reaction score
387
Taarifa ziliopo ni kwamba Bi Asha Bakari wa CCM ameanguka ghafla huko Dodoma akitokwa na damu za mdomo na masikio na hivyo kuwahishwa hospitali ya Muhimbili.

ImageUploadedByJamiiForums1408713699.457328.jpg


-------------------

KWA UFUPI
Habari ambazo zililifikia gazeti hili zinasema Makame alianza kuumwa usiku wa kuamkia juzi baada ya uvimbe mdogo uliokuwa umeota puani kupasuka na kuvuja damu nyingi.


Dodoma
Mjumbe wa Bunge Maalumu, Asha Bakari Makame amelazimika kuwahishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu baada ya kuzidiwa akiwa Dodoma ambako alikuwa akihudhuria vikao vya kamati.


Habari ambazo zililifikia gazeti hili zinasema Makame alianza kuumwa usiku wa kuamkia juzi baada ya uvimbe mdogo uliokuwa umeota puani kupasuka na kuvuja damu nyingi.

"Alivuja damu nyingi sana kiasi kwamba presha ilishuka na kulipokucha jana (juzi) asubuhi walipanga kumpeleka Dar es Salaam kwa ndege, lakini madaktari walishauri kwamba kwa hali yake asingeweza kuhimili usafiri huo, hivyo walimsafirisha kwa ambulance (gari la wagonjwa) saa tano asubuhi," kilisema chanzo chetu.

Mtoa habari wetu alisema Makame aliwahi kufanyiwa upasuaji hivi karibuni na kwamba mara kadhaa amekuwa akipatwa na matatizo ya kiafya. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk Nassoro Mzee alithibitisha kupokelewa kwa mjumbe huyo na kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

"Ni kweli alipokelewa jana (juzi) na tulimpa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi," alisema Dk Mzee. Hata hivyo, alikataa kutaja ugonjwa unaomsumbua mjumbe huyo.

Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alithibitisha mjumbe huyo kupelekwa Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua ghafla.

"Hatujafahamu tatizo ni nini ila ni taarifa tulizonazo ni kwamba aliwahi kufanyiwa upasuaji hivyo ana tatizo ambalo limekuwa likimfanya apelekwe hospitalini kupatiwa matibabu mara kadhaa," alisema Hamad.

CHANZO: Mwananchi
 
Mungu amsaidie apate nafuu. Ili arudi bungeni kuendelea kuwapigania watanzania.
 
Msalani. Naungana na wewe kumtakia mema. Lakini kwa kuwapigania Watanzania,hapana bwana mdogo. Huyu si ndiye yule mbibi aliyemaliza muda wake wote kwa matusi kwa Jusa, akisema serikali ya zanzibar ni ya kimapinduzi haipinduliwi kwa makaratasi, na matuisi kede kede? Anapigania watanzania gani kwa hoja ipi? Mtu asiyejua hata maana ya bunge maalum la katiba, wala hana habari kama kuna kitu kinaitwa rasimu ya katiba!. Tafadhali acha utani.

Dawa yake Dr. ampe complete bed rest ya miaka miwili ili akiruhusiwa kuinuka, akute dunia yake haipo.

La msingi, kama ni ebola, wabunge walioko dodoma wawekwe kwenye quarantine hadi mwezi mmoja upite bila kukutana na watu wa nje. Yaawezekana natural justice Mungu ameileta ili kuwastopisha hawa wahuni.

Mungu amsaidie apate nafuu. Ili arudi bungeni kuendelea kuwapigania watanzania.
 
Huyo bibi simpendi, ni mchumia tumbo na hana jipya. Uwepo wake ni janga kwa wananchi kwenye huu mchakato wa katiba mpya!...Namchukia kuliko kawaida..Nadhani kwa sasa acha nitulie ila nikijiridhisha kwamba hizi taarifa ni za kweli, nitakuwa na hafla weekend hii kuupa hadhi na heshima wakati mzuri kwangu kama huu.Kwa hilo nadhani na kwa kweli nina uhakika itakuwa faraja kubwa kwangu kuondokewa na adui kwenye ulingo wa mapambano! Kwa sasa ni muda muafaka kwangu kuongeza nguvu ili nijiridhishe na habari hii ili mambo yaanze mapema iwezekanavyo! Kila mtu ana muda ambao analazimika kuwa na majonzi na muda ambao anakuwa na furaha.Na huu ni muda wa furaha na faraja kwangu!
 
Back
Top Bottom