niseme kuwa nimeona hii post yake katika ukurasa wake wa facebook
kama ukisoma vizuri utaona kuwa kunajambo la msingi analo.
katika kipindi cha malumbano ya hoja ITV Jana alhamisi, hawakumpa MUDA WA KUTOSHA ASENGA na bwana Marcusy wakati anafunga hakumuelewa, sana sana alipita kule asenga alipokuwa anamaanisha.
kanuni ya 76 aliyosema asenga ipo sawa lakini Marcus na Mtatilo walivyoisoma awali walimaanisha kwa upande mmoja tu kuwa;
'kanuni zilimtaka spika kuhairisha bunge kwa sababu ya vurugu" na asenga aolichokisema ni kuwa ni kweli kanuni ipo hivyo lakini kuna neno la kisheria (anaweza) kusitisha hoja ya kikao cha bunge au kuhairisha kikao
alichosema asenga ndio hicho,kuwa naibu spika alisitisha kikao(ingieni kwenye kamusi ya kiswahili muone maana ya neno kusitisha au someni vizuri kanuni za bunge,
sasa hoja ije kupinga je ? ni kweli Ndugai alisitisha kikao na baadae akasema kabisa dakika zilizotumika na akaomba Lukuvi atoe hoja ya kuongeza muda.
kwa walioona bunge ni kweli alifanya hivyo.
chadema nawashauri msiwe mnatukana na kukashifu tu kila asemacho kijana wa CCM,JARIBUNI KUSOMA KWA MAKINI.
asenga posti yake inaanza hapa;
TUMIA MUDA WAKO KUSIOMA YOTE;
Malumbano ya hoja Itv na upotoshaji wa dk Lwaitama,Mtatiro na Marcus na taasisi ya yake kufatilia bunge.
Nawaomba muisome yote na mfatilie kwa makini.
Upo mkakati makusudi kabisa ya watu wazima kupotosha mambo kwa kuwa wanahasira na CCM, walishindwa kwenye kura za maoni za ubunge Mfano, Marcus, kidogo mzee Masako na Lwaitama ambae anamsongo wa mawazo wa kukosa mkataba mpya wa kazi serikalini, hali inayomfanya atembee kwa mguu au kupanda daladala akiamini kuwa eti kununua gari ni ubepari.
.Naamini wanafunzi wake wa UDSM mnamjua mzee huyu anaefikiria dunia ya kusadikika
Marcus anasema Itv pale aliposema mwanzo ijapo badae aligeuka na kuelewa somo MWISHONI, eti kanuni ya 76 inamtaka spika kuhairisha bunge zinapotokea vurugu na Mtatiro pia karudia vilevile.
Sasa wanatumia nafasi yao wao kuzungumza mwisho kudanganya na kukashifu juu ya multiple choice ahaaaaa aisee kama kashfa tunaziweza sana la kini hapa ni hoja tu, watu wazima wanapaniki.
Sasa na anza...
Kila mtu asome kanuni ya bunge au agoogle.
Ibara ya 76(1) inasema;
"Kwa madhumuni ya kudhibiti fujo endapo itatokea ndani ya ukumbi wa bunge na spika ATAONA kuwa kuna haja ya kutumia nguvu, basi ANAWEZA(may) kuhairisha shughuli za bunge bila ya hoja yeyote kutolewa au kusitisha kikao kwa muda atakaoutaja ili fujo hiyo iweze kudhibitiwa na mpambe wa bunge.)
Ata mtoto wa shule ya msingi anajua kuwa si lazima kuhairisha bunge na ni sawa naibu spika alivyositisha hoja ya kikao na kusimama kushughulikia fujo na alipomaliza alielezea muda uliopotea na kuomba kuongeza nusu saa
Hiyo moja; pia kwa mujibu wa kanuni hii tunajifunza kuwa kumbe spika anaweza kutumia nguvu kama alivyofanya kuita askari maalumu wa bunge chini ya mpambe wa bunge.
Sasa wanaosema Ndugai kakosea kumtoa Mbowe wamechemka
Ingewezekana wakati mpambe wa bunge anaongea na Mbowe ili atoke nje, naibu spika akamwambia mzee Mrema aendelee kuchangia`, lakini kwa kufata kanuni alisitisha ajenda ya kikao na Mrema kunyamaza kama kanuni ilivyomtaka.
Mbowe amevunja kanuni nyingi sana za bunge kwa kitendo chake
Soma kanuni hii;ya 59 alioitoa Michael Aweda mkurugenzi wa jimbo chadema anaejificha kichaka cha uanaharakati, jana alipotosha ITV kwakusema kuwa eti kanuni hiyo inamruhusu Mbowe kusimama na kutoa hoja bila kufata kiti cha spika.
twende kwenye kanuni;
Ya 59 inasema;
(kwa idhini ya spika, mbunge yeyote anaweza kusimama na kuchangia bungeni ktk nyakati tofauti (a) hadi (I) lakini (b) inamhusu Mbowe mana inasema (wakati anatoa hoja ili ijadiliwe) anapaswa kusimama na kuruhusiwa kusema na kiti cha spika".
maana Mbowe alisikika akisema kuwa "alikuwa na hoja"
Sasa jiulize Mbowe aliposimama alipata idhini ya spika? Hakupata na naibu spika alimwambia akae ili
Mrema amalizie, Mbowe hakutii sheria bila shuruti.
So Aweda jipange vizuri unaitia aibu chadema.
Twende kwenye kanuni ya bunge sehemu ya pili ibara ya 5 ambayo eti wanaitumia kwa kigezo, kama jambo alipo ktk kanuni naibu spika alitakiwa afate utaratibu wa mabunge mengine ya jumuiya ya madola,nisawa lakini kabla ya kufanya hivyo anapaswa kuona jambo hilo liliamuliwaje na waliomtangulia?
Watu wazima wanasahau kufata kanuni kamili, kuwa kabla ya kufata taratibu za mabunge hayo anatakiwa kutazama kanuni nyingine zilizopo na maamuzi ya awali ya maspika wa bunge letu waliomtangulia
ukiachiliambali kuwa Mbowe aliandika siku hiyo kwa naibu spika KIMEMO (rejea ushahidi alioutoa Ndugai juzi star TV) kuwa hatosema chochote bungeni siku hiyo.
Sasa wao wanakimbilia tu mabunge ya Madola na kuruka mstari Wasioutaka, kwa kuwa wanajua kuna spika aliepita aliwahi kuwatoa nje wa bunge ata kwa kuita askari wa bunge na ata Mnyika alipokataa kutii kiti cha spika.
Twende kwenye kanuni;
Hiyo ya 5
Inasema:
(katika kutekeleza majukumu yake yaliyotajwa ktk ibara ya 84 ya katiba, spika ataongozwa na kanuni hizi na pale ambapo kanuni hazikutoa muongozo, basi spika atafanya kazi kwa kuzingatia katiba, sheria nyingine za nchi, kanuni nyingine zilizopo? Maamuzi ya awali ya spika wa bunge pamoja(zingatia hapa juu) na mila na desturi za mabunge mengine yenye utaratibu wa kibunge unaofanana na utaratibu wa bunge la Tanzania )
Kanuni ipo wazi hapo na kama Mbowe hakuridhika na maamuzi ka kiti baada ya kutii maamuzi ya kiti ambayo ni ya mwisho alipaswa kufata fasili ya 4 hapo chini kuwa (mbunge ambae hajaridhika na uamuzi wa spika awasilishe sababu zake kwa kamati ya bunge ya kanuni)
Mbowe kavunja kanuni hii.
Na ni upuuzi kuamini kuwa eti ni sahihi bunge letu wabunge kupigana kwa kuwa yapo mabunge mengine yanafanya hivyo.
Tatizo ni kuwa watu hawakupitia ata debate primary, sec na vyuo.
Tuje kwenye hoja nyingine ya wana chadema wanaojificha kwenye unaharakati wakati mpaka kadi zao za za chadema ni no 56739.
Huyu kijana Mastawill Kahami ;
huyu ambae ktk mkutano wa mwisho wa CDM jangwan Dsm, akiwa na kombati zake za kaki alipewa kazi ya kuuza kadi za CDM (apinge hapa) ijapo anajificha ficha eti mwanaharakati wa vyuo, teeeeee
Aliasema pale ITV jana, eti anaushahidi kuwa rais Kikwete hakuteua mjumbe toka walemavu kama walivyopendekeza.
Uongo mkubwa na hoja hii ilitoka kwa Lisu na waziri Lukuvi alijibu bungeni lisu akawa mpole.
Ni hivi Tz inavyama vya kiraia zaidi ya elfu 14 vikiwamo vingi vya walemavu na wasiojiweza, sasa si kila asasi itapata uwakilishi ktk bunge la katiba, mana basi bunge litakuwa na wajumbe elfu kumi, kitu ambacho hakiwezekani.
LUKUVI alikuja na ushahidi kuwa, mbunge Sheimaa ambae ni mlemavu wa ngozi alipendekezwa na chama cha kiraia kama ambavyo CDM walipendekeza Lisu na Baregu, na Baregu kwa kuwa ana elimu,ufahamu,hekima na uzoefu kuliko Tundu, akateuliwa.
So ata hoja za Lisu juu ya wajumbe wa Bakwata na Kanisa si kweli, na lukuvi alitoa barua zao kuwa rais aliteua miongoni mwamapendekezo yao na Lisu hakupinga,BALI ALISHIKA TAMA.
Sasa hapa hoja ya kusema eti rais asiteue wajumbe wa bunge la katiba kwa hoja nyepesi kiasi hicho eti atapendelea CCM, basi kama hivyo ata chadema haijiamini mana inaweza kupendekeza mwana CCM.
Twende kwenye hoja ya kutaka wabunge wasiwe kwenye bunge la katiba eti kisa tu wengi ni wa CCM
Wangekuwa wengi ni wenu mngepinga?
Kuteua wajumbe wengi wa bunge la katiba toka vyama vya kiraia ni kuwapa mchakato wa katiba wa fadhili wa Marcus na wenzake kama wale wa jerumani.
Nani anafadhili taasisi ya familia ya Marcus?
(Ntakwambia siku ingine)
Wabunge ni wajumbe halali kubaki kwenye bunge la katiba mana huwezi kumuacha MBOWE kuwakilisha jimbo la Hai, mana ndio kachaguliwa na wananchi wa jimbo la hai kama mwakilishi wao kwenye mambo yote nyeti ya wananchi wa jimbo hilo.
Kama seuze Mbowe kwanini utake kumuacha mzee Chenge na utaalamu wake wa sheria kisa eti anatoka CCM? Hofu tu ya kutofikiri sana.
Hoja ya Znz kutoshirikishwa
mara zote nimekuwa nasema kuwa hawa jamaa wanakimbia wanasahau ata jana walisema nini?
Lisu aliwahi kusema "Zanzibar wasipewe nafasi sawa na bara katika uwakilishi wa mambo kwakuwa wao hawazidi miliono 2 na bara kuna zaidi ya milioni 35.Lisu kesha sahau
leo anakuja na kusema waznz hawakushirikishwa vya kutosha,uwakilishi wao ni mchache.
Kama Lisu ni mjumbe wa kamati ya bunge anaechukua posho za kamati kila kikao na ni mjenga hoja mzuri, ameshindwaje kujenga hoja kwenye kamati kushawishi washirikishwe hadi atege mtego wakuja kusema eti bungeni, akidhani itasaidia kutekeleza ahadi yake jimboni kuwapa madawati wanafunzi wasikae chini??
Nimepita jimboni kwa Lisu ,ni aibu na kama anajitambua baada ya CCM kushinda urais, alipaswa kujiuzuru maana ilani yake haiwezi kutekelezwa, ama aungane kutekeleza ilani ya CCM kama Mbowe na Zito kwenye majimbo yao, mana michango aliyozuia lissu jimboni kwake,kule kwa Mbowe na Zito inaendeleaa, yeye karupuka kuzuia.
Mbunge wa miaka 5.
NITAKUJA NA HOJA SIKUINGINE KUWA HAYA WAFANYAYO CHADEMA WANAONGWA NA MABEBERU,TUSIPOANGALIA WATAIVURUGA NCHI YETU.soma gazeti la JAMBO LEO LA JANA.
Ndugu zangu kumbukeni tabia za UKWELI
1.HUWA UNADHARAULIWA
2.MSEMAJI AU ANAEUSIMAMIA MWANZONI UPUUZWA NA ATA KIKIMBIWA NA RAFIKI ZAKE NA ATA KUUMIZWA.
3.UKWELI LAZIMA IDHIHIRI, IJAPOKUWA UWA UNACHELEWA NA KUKUTA UONGO UMESHA SAMBAA
MAANA WAKATI UONGO UNAPANDA GHOROFA KWA LIFTI, UKWELI UNAPANDA GHOROFA KWA KUTUMIA NGAZI,IJAPO
UTAFIKA TU SIKU MOJA GHOROFANI.
NAWASHUKURUNI KWA KUSOMA YOTE