Asemavyo Dokta Lweitama kuhusu magamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asemavyo Dokta Lweitama kuhusu magamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanangwa, Apr 2, 2012.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
 2. n

  nketi JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mara zote huyu mzee hujiita mwana ccm aliyekufa. Huwa simwelewi.
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,783
  Likes Received: 36,779
  Trophy Points: 280
  [h=1]Arumeru: Dr Lwaitama Ana Haya Ya Kusema…[/h] By admin on April 2, 2012 in home
  [​IMG]
  Ndugu Mjengwa,

  Ushauri wako kwa CCM hii ya makuadi wa soko huria na wapenda kusifiwa hata wanapokuwa hawana walilolifanya linalostahili kusifiwa si sahihi kwa maoni yangu. CCM ya leo wala haistahili kupewa ushauri wako wa eti: "CCM ya sasa inapaswa kupanga mikakati ya kuendelea kuongoza dola huku ikishirikiana hata na wapinzani. Ingawa hata huo ni mtihani mgumu wenye kukihitaji chama hicho kuwa na watu makini zaidi badala ya waendekeza fitina na majungu.  " Hii CCM ya leo ni CCM ya viongozi wanaofikiria kujilimbikizia mali kupita kiasi kwa kutumia mgongo wa kushika dola pekee au na wapinzania walio walafi kama wao na ambao watakubali kutawaliwa na CCM milele. Ushauri unatoa ni hatari kwani si ushauri wa kidemokrasia. Wananchi ndio wanapaswa kupanga nani awatawale si eti "CCM ya sasa inapaswa kupanga mikakati ya kuendelea kuongoza dola huku ikishirikiana hata na wapinzani."


  Yale yale yaliyopangwa gizani Zanzibar na watu wawili ya kugawana madaraka viongozi chama tawala na cha upinzani na kuzalisha vyeo lukuki vya umakamu wa Rais na gharama zake zinabebwa na watu masikini...Kwani cheo cha Waziri Kiongozi na Naibu Waziri Kiongozi vingekuwa na ubaya gani? Leo Tanzania ina Rais 2 na Makamu wa Rais wa 3 na ikianzishwa serikali ya Tanganyika basi tunaweza tukajikuta tunao labda wa Rais 3 na Makamu wa Rais 5 eti? Natumaini huo sio mmoja wa "mikakati ya kuendelea kuongoza dola huku ikishirikiana hata na wapinzani"!!!!


  Hapana!!! CCM kinaitaji kuondolewa madarakani haraka iwezekanavyo kama walivyoonyesha njia watu wa Arumeru. Kikae upinzani nachenyewe na pale wakifurunda Chadema basi Watanzania wawapunzishe na wao na wawarudishe CCM. Huo ndi mfumo wa vyama vingi, Ndugu Mjengwa!. Wanasiasa wanakuwa wanyenyekevu kwa wapinga kura kwa vile wanajua watapunzishwa mara moja wakizembea katika uongozi. CCM iliyoongozwa na kauli za Mheshimiwa Mkapa na Mbunge Lusinde kule Arumeru ilistahili kubwagwa na kuangukia pua na wapiga kura makini maana ilijaa majigambo ya kijinga na kauli za kipuuzi za watu waliolewa madaraka kutokana na chama chao kutawala kwa nusu karne.Tusaidiane


  Mjengwa. Mimi siku hiyo CCM itakapoondolewa madarakani na kuwa chama cha upinzani nitafufua uanachama wangu wa chama hiki kilichokuwa chenye mwelekeo wa kijamaa na kizalendo enzi za Mwalimu Nyerere pamoja na mapungufu yake ya enzi hizo katika nyanja za haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari. Tanzania inaitaji vyama vikuu viwili makini na vya kizalendo, kimoja chenye kuegemea ujamaa ( CCM) na kingine kuegemea ubepari ( Chadema), lakini vyote vya vikiogozwa na watu wanyenyekevu walio tayari kuwa kwenye upinzani kura za wananchi zikiitaji hivyo.
  Mwl. Lwaitama
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  wewe angalia tu, kulia kwake kuna chupa ya maji ya uhai, bei sh. 400. hakuna glass, anabwia kama dafu. kushoto kuna kiti cha plastiki hakina hata sponji. bado humuelewi tu?
   
 5. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mwanaccm aliyekufa inamaanisha kuwa ni mwanachama mwenye kadi ya uanachama asiyelipa ada za kila mwaka za uanachama, siku akilipa anakuwa mwanachama hai
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,783
  Likes Received: 36,779
  Trophy Points: 280
  Yani ni mwana CCM asiyeshiriki jambo lolote la kujenga chama chake kwa kuamini kuwa chama hichi ni chama kinachostahili kuadhibiwa kwa kuondoshwa madarakani. Umeelewa??
   
 7. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ni msema kweli huyu bwana!
   
 8. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  namkubali sana huyu mzee ni mzee mwenye maono kwa nini huyu bwana BWM hataki kujifunza kutoka kwa hawa wazee?
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  anawaita 'wasomi uchwara'
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Hebu wampe kipindi kwenye TV wiki hii atupe raha ya uchambuzi.
   
 11. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Dr. AL umenena, laiti na wenzako kama Bana wangekuwa na mtizamo huo ndani ya CCM basi tungefikia kile kilele cha demokrasia tunayoitaka hapa Tanzania kwa kasi sana.

  Lakin kutokana na ugumu wao wa kukubali mabadiliko na ufinyu wao wa mawazo au kujipendeza kwa watawala ndio maana hali ipo kama ilivyo sasa. Hata hivyo pamoja na hayo bado tumejaaliwa viongozi makini, wabunifu na wanyenyevu ndani ya chadema wanaojua kucheza na hali hii hii mpaka kieleweke na kwa sasa wamekuja na program ya M4C. Kama program hii itafanikiwa vizuri, na lazima ifanikiwe basi tutegemee mabadiliko kwa kasi ya tsunami kwan tunachotaka kwa sasa ni elimu ya uraia ili wananchi wajue nguvu sahihi waliyonayo. Wengi tulishachoka zamani sana
   
 12. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  sasa usichoelewa ni nini?? manake ye si mwana ccm..we nawe ujinga umekutawala kama lusinde..mpssxxyyy
   
 13. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Rweitama ninavyo
  mfaham c mwana
  ccm, anajua mambo
  sana ya siasa
  kwa kweli ni
  mwana chadema
  asiyependa kujio
  nyesha. Nampenda
  sana ni mchambuzi
  mahiri sana.
   
 14. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  huyu mzee namkubali..ana bichwa baya lakini lina akili..sio wandengereko mlio wapa nchi wenye vichwa vya duara lakini wanakenua kuonyesha dentition zao kwakua kijiji na familia yote wana minjino mibaya..hovyooo..
   
 15. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Na si ada tu...hata michango ya hoja,uhudhuriaji mikutano na upigaji kura
   
 16. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Siamini kama
  kuna msomi
  anaweza kuipenda
  ccm kwa moyo
  wake wote.
  Labda awe na akili
  ya ''MAITI''
   
 17. YanguHaki

  YanguHaki Senior Member

  #17
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio rahisi kujua kama ana glass kwa sababu ya kukingwa na maua ya hao Wairani! Dr. Lwaitama ana hoja hapo. Achana na mapungufu yake kama binadamu!
   
 18. fanson

  fanson Senior Member

  #18
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 181
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ni moja ya wazee wachache wanaotakia mema watoto,vijana wao na wao wenyewe,we mfano mzuri L..
   
 19. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #19
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nina hakika hata Mwl Nyerere angekua hai angekua mfuasi wa C.D.M
   
Loading...