Ni utaahira tu utaisha. Hapa ni sawa na pahala pengine popote. Watu wanauza na kununua magari humu itakuwa kumpata rafiki au mwenza? Watu wanapata sponsors humu itakuwa rafiki au mwenza? Watu wanapata guarantors humu itakuwa mke?....n.k.
Watazoea tu. Miaka ya nyuma kwa ushamba wetu tuliamini kumuoa/ kuolewa na mtu ni mpaka ukoo wako uufahamu ukoo wa mtarajiwa. Imeenda hivyo kwa miaka sasa si takwa/sharti muhimu tena. Unakutana na mwenza kijiweni/sokoni/daladala/msibani/harusini/kisimani huku hamjuani kabisa mnakubaliana mnaanza kuishi na mwishowe wazaz watataarifiwa. Jamii imezoea na ndivyo hivyo ilivyo sasa.
Kwahiyo ni imani yangu kuwa hata humu ni ushamba na uhafidhina vinasumbua watu ndo maana wanaona kama hili si jukwaa sahihi. Big up kwa waleta uzi woote ktk jukwa hili.
Siyo kila mtu anaenda kijiweji ama anazurura mitaani ama anashobokea harusi kama wewe. Si kila mtu anafanya mambo yasiyoendana na mila na desturi misibani. Eti wenzio wanalia wewe unatongoza. Watu wako bize kinyama, wanyama nyie. Hapa ni saw a na pahala pengine popote.
. Nawasilisha