Asanteni NBC Bank mmetutumia na sasa mmetu-dump

Asanteni NBC Bank mmetutumia na sasa mmetu-dump

Kigoma 2015

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2011
Posts
371
Reaction score
93
Kwanza tulianza tukiwa chini ya Erolink ndani ya NBC toka mwaka 2011, huku tukipewa mikataba ya miezi sitasita mpaka ilipofikia mwaka 2013 September mkasema hakuna staff atakaekua chini ya Erolink tena.. hivyo wote tukawa chini ya NBC kwa mikataba ya mwezi mmoja, miwili, mitatu......

tulifanya kazi kwa weredi na nguvu zetu zote tena bila ya hata malipo ya overtime... tukiamini mtaziona juhudi zetu na kutufikiria katika ajira.....
bahati mbaya sana hata nafasi nyingi ambazo zilikua zikitangazwa tuliomba ila hatukua hata tukiitwa kwenye interview ila tlikua tukiona sura mpya kabisa zikiajiriwa hali nasi tukiwa bado benchi.....

... bado hatukufa moyo kwani pamoja na kufanya kazi kwa weredi mkubwa hata kwenye idara nyeti kabisa.. tuliendelea kupiga kazi huku tukiamini maneno ya MD mama Mizinga Melu kuwa hakuna atakakosa nafasi.... masikini ya Mungu kumbe tulikua tukidanganywa....

Tukaanza kuona baadhi ya wenzetu wakipunguzwa kuanzia mwezi wa 12 mwaka jana hatukuamini..... sasa ilipofikia 31.03.2014 ndipo tukaamini kua halaaaaa kumbe nasi hatuitajiki tena?
ni zaidi ya vijana tupatao 2000 tupo mitaani sasa baada ya kuitumikia benki kwa muda wa miaka miwili wengine mwaka na zaidi.....

Sawa mmeamua kutu dump.... lakini mbona mafao yetu ya PPF nayo mnazungusha??
kuna vijana wapo nje ya bank toka mwezi wa 12 mwaka jana lakini mpaka sasa wanasotea hela zao za mafao ya PPF.... wakienda NBC HQ wanaambiwa check zenu bado hazijafika.... kweli?? toka mwezi wa 12??
mbaya zaidi na zaidi..... pesa zetu za "leave allowance". nazo tunaambiwa hatupaswi kulipwa??, kweli??
tuna ushahidi wa baadhi ya watu waliofanya kazi na erolink kwa muda wa miezi sita lakini pesa zao za leave walipewa..... kwanini iwe tofauti na NBC??

Sawa mmetu dump tunakubali... basi tukamilishieni tunachostahili tuende kwa amani... napo mnatupiga danadana.... hii ni haki??

ni hayo tu...
 
Mi nashindwa kuelewa mambo yanavyoendeshwa nchi hi, kama nyie mmeanzakufukuzwa toka mwaka jana december sasa mbona tena hawa raia wanaendelea kuwafanyisha watu mainterview huo mwezi wa 12 ilifanyika interview ya maana tu pale piccock hotel kijitonyama, na watu waliokua wanawafanyia ni fresh graduate sasa kama kuna watu bado hawajawaajili na wanaexperience na ni hao 2000 kama mkuu alivyo tutonya kwa nini wasiwape ajira hao waliopo kwao wanaofanya kazi tayari, sidhani kama wote hao 2000 hamna watu wachapa kazi mpaka waanze kuajiri watu wengine toka njee, hebu mliopo kwenye hio bank mtusaidie kutuelewesha nn tatizo
 
Tatizo wabongo waoga sana. Jaribu kusoma sheria za ajira. Kama huwezi basi omba msaada wa sheria. Musiishie kulalamika kama vile sio wasomi. Sheria zote zipo wazi. Tafuta mtu aliyesoma HR au sheria akupe maajuzi
 
nyie wabongo mnaongea sana na ni watu wa maneno bila vitendo. Kabla ya kukurupukia kazi, someni makubaliano au mikataba mliyopewa, huo ndio muongozo wenu.
 
Mi nashindwa kuelewa mambo yanavyoendeshwa nchi hi, kama nyie mmeanzakufukuzwa toka mwaka jana december sasa mbona tena hawa raia wanaendelea kuwafanyisha watu mainterview huo mwezi wa 12 ilifanyika interview ya maana tu pale piccock hotel kijitonyama, na watu waliokua wanawafanyia ni fresh graduate sasa kama kuna watu bado hawajawaajili na wanaexperience na ni hao 2000 kama mkuu alivyo tutonya kwa nini wasiwape ajira hao waliopo kwao wanaofanya kazi tayari, sidhani kama wote hao 2000 hamna watu wachapa kazi mpaka waanze kuajiri watu wengine toka njee, hebu mliopo kwenye hio bank mtusaidie kutuelewesha nn tatizo

ni kawaida yao.... na hata tulipokua tukiomba hizo nafas hatuitwi hata kwenye interview....
na ukiitwa kwenye interviw unaambiwa huja qualify...
mwaka jana walitangaza nafasi za tellers.... watu tumefanya kazi hiyo zaidi ya mwaka sasa.... tuliomba... tukafanyishwa interview majibu kutoka ati hatujafaulu na mpaka leo hakuna alieajiriwa.....
 
Jikusanyeni wapeleke mahakamani hao makaburu.
 
Kuna mshua wa rafiki anafanya kaz hapo tena senior position ana declare kuwa hiyo benk nw going worse almost to die, poor management, ila ni serikali tu inaishikikia haitaki kuona inakufa though makaburu wameshashindwa na kinachofanyika xaxa ni kupunguza wafanyakazi kwa kas cz they need to reduce the cost of operation. In each single day wana vikao agenda ni hw to secure NBC and conclusion is to reduce an employees as much they can, u cn get today job at NBC and after few days u get suprise of being terminate. In short NBC nw is not safe place.Almost to die.
 
Jamani poleni sana. Kubalini kwamba mmefukuzwa kazi lakini msikubali kudhurumiwa chochote. Nawashaurini mwende PPF yoyote mkaulizie hayo mafao yenu kama yapo coz mwaweza kuta hakuna kilichokuwa kinapelekwa huko then hatua ndo zinaanzia hapo. Jambo nililogundua ni kwamba watu wengi wakisha ajiriwa wanabweteka kabisa, wakijua watafanya kazi mpaka kufa ilhali wakiwa bize kufanya kazi tu pasi na kufuatilia sheria za kazi, mafao yao n.k. Wakishafukuzwa ndo wanashtuka toka usingizini. HUO NI UJINGA, I TELL YOU
 
Duh! Woga unazidi.

Sasaa kama nyie mlioko ndani mnakosa tunaokuja ndo itakuaje. Mpaka napata uoga wa hizo internship ila Mungu ajua. Bahati ya mtu hailaliwi mlango wazi. Labda haikupangwa mkuu. Piga moyo konde mapambano yaendelee. Sasa ninaposema mambo hayaeleweki na ni kweli. Hapo bahati imegoma na koneksheni zimegoma. Sasa watu watumie uchawi? Maana sielewi kipi kinahitajika kama nyie mlio na uzoefu mmekosa na 'freshers' wakazama. Mi ntapambana mpaka mwisho kieleweke. Food aint gonna buy itself kabisa. Nawasilisha
 
Back
Top Bottom