Asanteni kwa maombi yenu

Maserati

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2014
Posts
11,602
Reaction score
20,101
Wana MMU,
Habari ya sikukuu ya Eid, natumai zimepita salama.
Kabla sijatoa shukrani zangu naomba nielezee kwa ufupi.

week 3 au mwezi uliopita, rafiki yangu kipenzi relato ilikuwa katika harakati za kutafuta riziki kama watu wengine na shuguli zao mbalimbali. Akiwa huko akapata ajari, alidondoka na kwa bahati mbaya akajigonga kichwa chini. Akapelekwa hospitali akahudumiwa na kuruhusiwa siku hiyo hiyo kwa sababu hakuwa na majeraha makubwa mwilini.

Nakumbuka siku hiyo alinipigia simu akasema tu kichwa kinamuuma lakini amepata dawa za kutuliza maumivu. siku kadhaa mbele akiwa eneo lake la kujitafutia riziki alidondoka na kupoteza fahamu. Kuanzia Hapo mpaka week kadhaa mbele hakurudisha fahamu zake.

Akahamishwa hospitali mpaka hospitali moja jirani na maeneo ya mwenge hapa dar, huko ikaonekana kuna internal breeding na kuna damu zimeganda kichwani kwake. Hapo mama yake akachukua hatua na kuanza process ya kumpeleka nje ya nchi kufanyiwa upasuaji. Alipelekwa south Africa na week iliyopita walifanikiwa kumfanyia upasuaji ambao ulifanikiwa kutoa damu zilizoganda na hatua zingine za kitabibu. Akapelekwa kwenye wodi ya uangalizi maalumu ICU, kwa siku kadhaa na hali yake kwa sasa imetengemaa. ametolewa ICU na kurudishwa wodi za kawaida, pia jambo zuri lingine na la kumshukuru Mungu siku mbili zilizopita na mpaka sasa ni amerejewa na fahamu, baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa zaidi ya week 2.

Napenda kuwashukuru wana mmu na Jf wote kwa ujumla ambao mlifahamu japokuwa si kwa undani sana, kwa kweli nilishindwa kusema au kutoa taarifa moja maana nilichanganyikiwa sana, lakini kwa namna moja au nyingine mlishirikiana nami na familia ya relato kwa ujumla, katika kumuombea mwenzetu katika kipindi kigumu alichopitia.

Wengine mlisaidiana na vikundi vya maombi kumuombea mpendwa wetu, na wengine mlimuombea sana ili MwenyeziMungu aweze kutenda jambo na kumponyesha relato haraka. Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana na naomba msiache kumuombea mpaka pale atakapotoka hospitali na kupona kabisa.
Nawashukuru sana.
Mungu awabariki wote..
_______________________________
_______________________________
UPTADES KUHUSU HALI YA RELATO
kama ambavyo niliahidi kuwaletea taarifa, jana alifanyiwa vipimo CT scan na vingine, bado ametakiwa kubaki nchini south Africa kwa ajili ya kuendelea na matibabu.
Mpaka mwisho wa mwezi huu, au katikati inaweza isifikie mwisho wa mwezi akawa ameruhusiwa, lakini bado ametakiwa kubaki huko.
Asanteni kwa maombi yenu, tuzidi kumuombea bado anahitaji maombi yetu..
 
Mungu ampe unafuu na apate kupona kabisa. Mwenyenzi Mungu ni mwema, naye atamjalia nguvu aweze kurudi katika hali take ya kawaida.

"So do not fear, for I am with you; do not be dismayed, for I am your God. I will strengthen you and help you; I will uphold you with my righteous right hand."

Isaiah 41:10.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…