barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,865
Rais JPM safisha "uozo" huu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Mh.Waziri Prof.Mbarawa umekuwa msikivu,mwenye kuitikia wito na kufuatilia malalamiko ya wananchi juu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara yako.Hakika wewe ni mmoja wa mawaziri katika Serikali hii unayefanya kazi kwa kujituma na kwa busara kubwa sana.Mungu aendelee kukusimamia.
Baada ya kutembelea viwanja mbalimbali vya mikoani kama Iringa,Mbeya na Dodoma hatimaye umefika kwenye kitovu cha usafiri wa anga Tz na Uwanja wa Julius Nyerere International Airport.Mambo yote yaliyoletwa hapa umeyashuhudia na kuona kuwa si majungu bali ni hali halisi,bila shaka umeona na kusikia malalamiko ingawa waliweza kukukwepesha sana kupata muda wa kutosha kuonana faragha na wafanyakazi ambapo ungepata changamoto nyingi sana zinazokwamisha ufanisi wa uwanja huu.
Uamuzi wako wa kuunda Tume ndogo ili kuchunguza malalamiko ya wafanyakazi umepokewa kwa mikono miwili sana sana,tunaomba tume hiyo iwe huru,iundwe na watu huru na wasio na maslahi na madai yanayolalamikiwa,lakini pia tunaomba tume hii isiishie Makao Makuu tu ya TAA bali itembelee na kuhoji wafanyakazi mpaka wa kada ya chini kabisa katika Uwanja wa JNIA na baadhi ya viwanja vya huku mikoani,ni imani yetu utagundua mambo mengi sana yatakayokusaidia kujuwa wapi pa kuanzia.
Mwisho tunakuuliza,mbona kale kakibanda pale nje ujakazungumzia hadharani?Hujaona tatizo la Mgahawa kujengwa kwenye eneo la "No Parking" ambalo lilikuwa likutumika kama eneo la abiria?Hakika ujio wako umeleta tija,maana tayari watu wameanz kuachia ngazi kwa kuzikimbia nafasi zao maana wataumbuka.Utapata ushirikiano mkubwa na utagundua mambo mengi sana.