Asante serikali ya CCM kutokuingiza mahakama ya kadhi kwenye katiba mpya

mmaranguoriginal.

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
4,060
459
Nawasalimu sana.

Nataka kutoa pongezi zangu za dhati kwa serikali yangu ya CCM kwa tukio La Jana la uzinduzi Wa katiba mpya itayokwenda kupigiwa kura ya maoni pindi daftari la wapiga kura likiboreshwa na kulitakia zoezi zima mafanikio mema.

Mara baada ya kusema hayo nimefurahi sana kwa tendo la rasimu ya katiba mpya hii kukata kipengele cha mahakama ya kadhi kutokuingizwa kabisa mosi ni changamoto za kuindesha mahakama hiyo kwa kutumia Pesa na kodi zetu wananchi na huku ikitoa huduma kwa waislamu peke yao ambapo naona ni kitu ambacho hakiingii akilini.

Mathalani utafiti uliofanywa na baadhi Ya watu imebainika kwamba wanaopinga mahakama hii idadi kubwa ni waislamu wenyewe haswa bakwata na kuonyesha kwamba kuwa kuna shida kubwa kwenye hii mahakama hata kwa upande wao waislamu mfano matatizo ya nchi kama somalia,Nigeria,Kenya, sudani n.k kwa uchache ni baadhi Ya nchi ambazo zimeonja joto ya jiwe kuhusu mahakama ya kadhi ambapo kuiruhusu hapa tanzania ni kuleta machafuko haswa.

Mahakama hii kutumia kodi yangu na wasio waslamu ni uonevu mkubwa sana na nitalipinga mpaka mwisho Wa dunia.napenda kutoa nasaha kwa serikali yangu Ya CCM kukaza Uzi huo huo kutokuingiza hii mahakama kadhi kabisa.

Nawasilisha.
 
We kanywe mbege pale marangu mtoni, hukumsikia Pinda bunge la katiba?
 
We kanywe mbege pale marangu mtoni, hukumsikia Pinda bunge la katiba?

zile ndo zinaitwa siasa mkuu...hata kikwete wakati anaomba kura aliwaambia waislam kua atalishughulikia suala la mahakama ya kadhi.... binafsi..siitaki..na nadhani kwa wenye kuipenda sana hii mahakama wahamie somalia,sudan na nchi zote zinazojiendesha kwa mahakama hii...ambazo nyingi ziko kwenye machafuko.
 
We kanywe mbege pale marangu mtoni, hukumsikia Pinda bunge la katiba?

Ndio ile hadithi ya Jini ambalo mtu alilifungulia, likataka kumla, akaliambia lirudi kwenye chupa ili aone lilikuwa limekaa namna gani, baada ya kuingia kwenye chupa, akafunga kifuniko na kuendelea na maisha yake, aidha, hiyo ndio imewakumba UKAWA baada ya kuambia BMK litasitishwa, wakaweka chini mikoba wakati wenzao wanamilisha Katiba Pendekezwa kwa Kasi, Standard and Speed.
 
Asante serikali ya CCM kutokuingiza mahakama ya kadhi kwenye katiba mpya
Hilo ndilo lililomuumiza moyo JK jana. Aliwaahidi waisilamu wenzake mwaka 2005 na wakamchagua. Ilipofika 2010 akashauriwa kwamba hiyo kitu haitekelezeki, akaiacha. Amebanwabanwa hapo kati, akaamua kuanzisha mchakato wa katiba mpya ili mahakama ya kadhi iingie kwa mlango mwingine ili aondokane na lawama kutoka pande zote (NEC ya CCM vs waisilamu). Sasa anaondoka madarakani bila ya mahakama ya Kadhi, na wataalamu wa sheria wameshasema hakuna sheria inayoruhusiwa kutungwa ambayo inapingana na ibara yoyote ya katiba, kwa hiyo hata hiyo sheria waliyoahidiwa kutungiwa mwezi januari, imeelezwa kwamba mtu yoyote akienda mahakamani kuizuia atashinda kesi, na sheria itafutwa!
 
wajanja tulishaona mbali ile ya Pinda ni janja ya kupata za NDIYO wameshafanikiwa hakuna mahakama ya kadhi tena hapo
 
kwa diplomasia ya hali ya juu kabisa, Mheshimiwa Rais aliongea jana kua, wakati wake bado, watu bado wanahofu. Do you need more from this guy. He is exceptional politician. Sasa tunasubiri tu aondoke Madrakani ili Makanisa ya anze kufundisha waumini wake kua hakufanya lolote katika nchi hii. Kama walivyo fanya kwa Ali hassan Mwinyi na Kumruka Mkapa aliefilisi Mali zote za Nchi.
 
Tusiwe na haraka, wakati wake bado, Watanzania bado wana mashaka na hiyo kitu, wakati wake ukifka itaingia tu.
 
kwa diplomasia ya hali ya juu kabisa, Mheshimiwa Rais aliongea jana kua, wakati wake bado, watu bado wanahofu. Do you need more from this guy. He is exceptional politician. Sasa tunasubiri tu aondoke Madrakani ili Makanisa ya anze kufundisha waumini wake kua hakufanya lolote katika nchi hii. Kama walivyo fanya kwa Ali hassan Mwinyi na Kumruka Mkapa aliefilisi Mali zote za Nchi.

Kitufe cha "Like" kiko wapi, hata kama sikioni pokea Like kutoka kwangu.
 
Si kwel kwamba mahakama ya kadhi inaleta machafuko, na si kwel kwamba bakwata hawaitaki, bali waislam hawaitki kwa sababu ya kuchaguliwa sheria za kuhukumu, tusilete propaganda kwenye ukwel, mbona ktk utawala wa nyerere ilikuwepo, ilileta machafuko gani?
 
kwa diplomasia ya hali ya juu kabisa, Mheshimiwa Rais aliongea jana kua, wakati wake bado, watu bado wanahofu. Do you need more from this guy. He is exceptional politician. Sasa tunasubiri tu aondoke Madrakani ili Makanisa ya anze kufundisha waumini wake kua hakufanya lolote katika nchi hii. Kama walivyo fanya kwa Ali hassan Mwinyi na Kumruka Mkapa aliefilisi Mali zote za Nchi.

Katiba hii ni nzuri isipokuwa jambo moja halikukaa vizuri.kwa nini kuwanyima uraia watanzania wenzetu ambao kwa ajili ya maslahi muhimu wamechukua uraia wa nchi nyingine.Hii imedhihirisha watanzania tuwanafiki au tumejawa na wivu.Tunajidai tunawapenda ndugu wezetu walio nje ili tufaidi kutoka kwao lakini hatutaki wao wafaidi.

Pia ni jambo la baraka kubwa kuachana na mahakama ya kadhi.Kimsingi hii ni mahakama ya kiislamu au ya waislamu.sasa tutakuwa na mihiimili mingapi.Halafu ni kwa nini inataka kujikita katika masuala ya mirathi,ndoa na talaka.tujiulize muislamu aliyefunga ndoa katika uislamu alafu akabadili dini atalindwa na mahakama ipi?Au muislamu huyo akawa na watoto wakristo watoto hao watalindwa na mahakama ipi ya nchi?Hata hao wanawake watapata haki zao kweli?
 
Juzi tulimsikia balozi Mahiga akisema kuna wa TZ-AL SHABAB.na wengine wanaenda ISIS hofu yangu watakaporudi
 
Juzi tulimsikia balozi Mahiga akisema kuna wa TZ-AL SHABAB.na wengine wanaenda ISIS hofu yangu watakaporudi

Atoe Ushahidi. Kwetu sisi Waislamu, Hao Alshabab, ISIS, ALQAEDA, BOKO HARAM na Wengineo ni Makafiri wakubwa kabisa. Uislamu hauja ruhusu hayo wanayo yafanya. Hufanya hao kwa Maslahi ya Mabwana zao na Political agenda zao. Mpaka sasa ni watu wachache sana wasiojua kua BOKO HARAM, ALQAEDA na ISIS wameanzishwa na Marekani kwa ajili ya sababu za kisiasa na Kuuchafua Uislamu.

Wanatumia Bunduki za Kimarekani na Vifaru na Magari ya kijeshi ya Marekani.
 
Back
Top Bottom