Asante sana Shekhe wa Dar es Salaam! Mokiwa Umenishtua.

Asante sana Shekhe wa Dar es Salaam! Mokiwa Umenishtua.

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
19,493
Reaction score
18,387
Wakuu, nimemkubali sana Huyu Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati akitoa salamu na kuwasihi wakristo wote kusherehekea kwa Amani sikukuu za Christmas.
Nadhani ni mwenyekiti pia wa Baraza la Muunganiko wa dini zote kubwa kwa mkoa huo.

Shekhe alianza na salamu moja mujarabu sana..Shalom!! Akimaanisha "peace". Hii ni salamu yenye nguvu sana.

This man is a real peace maker! Big up Shekhe Alhad Mussa Salum...

Hakuzungumza yeye peke yake, na Valerio Mokiwa wa kanisa la Angilican alizungumza pia, Huyu Askofu yeye alisema hawezi kukemea ulevi simply kwa sababu atakuwa anaharibu biashara za watu...
Hii ni hatari kwa upande mwingine kiimani.

Gwajima yeye kasema anaridhika sana na hali inavyokwenda na wanaolalamika kukosa pesa ni wale waliokuwa wanapiga pesa zisizo za halali.
Anadai wale waliozea kutumia pesa halali maisha yanaenda na hawakosi pesa...

Hongereni kwa kujaribu kuitetea amani ya nchi.
Shalom kwa wana Dar wote!
Shalom kwa Watanzania wote.
 
Sheikh ndio kaongea kitu cha maana sana, hao wengine(Mokiwa na Gwajima) ni waganga njaa watupu, wamegeuza dini kama kichaka cha kufichia watu maovu na kupiga Pesa za wajinga.
Ni kweli, nimependa sana Mazungumzo ya huyu Shehe.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
UOTE="kiwatengu, post: 18972909, member: 103490"]Wakuu, nimemkubali sana Huyu Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati akitoa salamu na kuwasihi wakristo wote kusherehekea kwa Amani sikukuu za Christmas.
Nadhani ni mwenyekiti pia wa Baraza la Muunganiko wa dini zote kubwa kwa mkoa huo.

Shekhe alianza na salamu moja mujarabu sana..Shalom!! Akimaanisha "peace". Hii ni salamu yenye nguvu sana.

This man is a real peace maker! Big up Shekhe Alhad Mussa Salum...

Hakuzungumza yeye peke yake, na Valerio Mokiwa wa kanisa la Angilican alizungumza pia, Huyu Askofu yeye alisema hawezi kukemea ulevi simply kwa sababu atakuwa anaharibu biashara za watu...
Hii ni hatari kwa upande mwingine kiimani.

Gwajima yeye kasema anaridhika sana na hali inavyokwenda na wanaolalamika kukosa pesa ni wale waliokuwa wanapiga pesa zisizo za halali.
Anadai wale waliozea kutumia pesa halali maisha yanaenda na hawakosi pesa...

Hongereni kwa kujaribu kuitetea amani ya nchi.
Shalom kwa wana Dar wote!
Shalom kwa Watanzania wote.[/QUOTE]
Namkubali ana huyu Sheikh maana amekuwa chachu ya umoja wa Madhehebu hasa kuonesha UMA Uislamu halisi ulivyo.. Sheikh huyu amekuwa mbegu njema sana ya amani , umoja na furaha katika imani mbili za Kikristo na Kiislamu.. Nimeupenda sana Uislamu kupitia Sheikh huyu..
 
Huyu ni sheikh ambaye bila shaka Elimu Akhera na Dunia zote zipo
 
Huyo anayejiita Sheikh wa mkoa ni njaa tupu
Kutwa kwenye maduka ya wahindi na shughuli za kiserekali

Sasa anatafuta chumo jipya kwa wafuasi wa Kristo
 
Niseme tu watu huwa wanabadilika badilika kama vinyonga kwa sababu tofauti tofauti huyo anayeridhishwa sasa na mwenendo wa nchi ni haki yake na anazo sababu za kutosha. Ila nachelea kusema wengine mazingira, woga au ukabila nk. Hulazimisha mtu kubadilisha mtazamo
 
"Hawatokuwa radhi nanyi mayahudi na manasara mpaka mfuate milazao" quran
Aloandika haya maneno alikosa maono...dunia ya sasa hiko kifungu kama kweli kipo ktk kitabu hayawezi ku-apply popote duniani may be Allepo,Saud Arabia,kidoogo kwenye baadhi ya nchi zisizokuwa na wakristo japo siamini kama zipo.kuna wakati huwa nahisi kuna tatizo somewhere kwa baadhi yetu sie tuliokuwa na imani khasa linapokuja suala la kutafasiri baadhi ya aya ktk vitabu vyetu.
 
Back
Top Bottom