WILLIAM NGELEJA NGUZO YA MAFANIKIO SERIKALI YA AWAMU YA NNE,SEKTA YA NISHATI
Willium Ngeleja ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa,mbali na kuwa mbunge kwa kipind cha pili sasa, Ngeleja amewah kuwa naibu na hatimaye wazir wizara ya nishati na Madini kwa takriban miaka mitano na nusu kuanzia Januari 2007 hadi mei 2012 alipojiuzulu kwa kuwajibika kisiasa kutokana na shinikizo la bunge.
Ni ukweli ulio wazi kwamba mafanikio makubwa tunayoyaona sasa kwenye sekta ya nishati na madini, ni matokeo ya akili inayochemka,maono,mipango mizur na ubunifu mkubwa wa Ngeleja alipokuwa wazir wa nishati kwa kipind chake hicho.
Hata utafutaji wa gesi asilia na mafuta ulianza kushika kasi zaid Ngeleja akiwa waziri, ukiwemo mradi mkubwa wa ujenz wa bomba la gesi kutoka mtwara hadi Dar es salaam, eneo la kinyerezi kunakojengwa kituo kikubwa cha kupokelea gesi hiyo baada ya kuchakatwa katika vinu vyake vilivyoko Mtwara na songosongo.
Jambo moja kubwa na nuhimu kwa ustawi wa taifa letu,lililofanywa na serikali ya raisi kikwete wakat Ngeleja akiwa wazir ni ubunifu wa bomba hilo la gesi asili lenye urefu wa km 500.
Ngeleja kwa kushirikiana na TPDC mwaka 2009 walibuni mradi huo wa bomba la kusafirishia gesi asili na kuanza utekelezaji kabla hajajiuzulu uwaziri mei 2012.
Nawataja Ngeleja na TPDC katika ubunifu huo kwa sababu mradi huo haukuwa kwenye ilani ya CCM ya mwaka 2005-2010, kwa hiyo bila maono na ubunifu wao mradi huo usingekuwa hapo ulipofikia leo.
Walichofanya Ngeleja na TPDC, kinafananishwa na maono na ubunifu alioufanya mh.Kikwete mara tuu baada ya kuingia madarakan kwa kubuni na kuanza ujenzi wa chuo kikuu cha dodoma(Udom) mwaka 2006 kwani ujenz wa chuo hiki haukuwa kwenye ilani ya chama ya mwaka 2005-2009.
Mpango kabambe wa umeme vijijini kupitia REA, mpango huu ulibuniwa katika mwaka wa fedha wa 2010 /2011.
Mpango huo ni mojawapo ya mambo mengi makubwa mazuri ambayo raisi Kikwete amefanya katika utawala wake na kusimamiwa kwa umahiri mkubwa na Ngeleja na sasa Prof. Muhongo ambaye alimrithi Ngeleja.
Mpango huo wa umeme vijijini, ni muhimu sana kutokana na ukweli kwamba hakuna nchi yeyote duniani iliyopiga hatua ya maendeleo bila Kuwa na nishat ya umeme wa uhakika kwa wananchi wake.
Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mpango huo imeiwezesha serikali kuwafikishia umeme asilimia 36 ya wananchi vijijini had sasa, Hii ni zaid ya lengo lililokuwa limepangwa na serikali la kuwafikishia umeme asilimia 30 ya wananchi ifikapo mwaka 2015,hivyo serikali imevuka lengo ililokuwa imejiwekea kupitia REA,Tanesco na washirika wa maendeleo.
JUA KWA UFUPI SABABU ZA KUMFANYA NGELEJA KUWA RAISI 2015 AMBAYE SISI VIJANA TUTAHAKIKISHA ANAFANIKIWA