Kiwera Mikaeli
Senior Member
- Aug 11, 2012
- 121
- 40
Ndugu Wanajamvi
Kwa heshima kubwa naomba nitoe shukrani kwa niaba yangu binafsi, familia yangu na watu wangu wa Kijiweni kwa Ujasiri wa Kuendesha mijadala yenye tija kwa taifa letu bila kujali risk ambayo ungeweza kupata katika biashara zenu.
Tulifarijika sana kwa midahalo iliyorushwa na vyombo vyenu. Hakika tumepata Ujasiri wa aina yake, tumepata kujua vizuri zaidi wanasiasa wetu haswa walioko madarakani.
Tunaomba upuuze Mkwara wa Spika Sitta na muendelee na Ujasiri huo. Heri kufa au kufisilika kwa ajili ya kupigania taifa letu kuwa bora kwa Kizazi Kijacho.
Asante sana IPP Media - ITV, Capital Radio na Radio One pamoja na management na staff wote. Hakika Mungu yu Nanyi.
Nitakuwa si uungwana kama sitamshukuru ndugu A. Mbowe na team yako nzima ya Ukawa. Bila kukataa kuburuzwa na CCM tusingejua mambo yote yaliyozungumzwa kwa mijadala kadhaa iliyoendeshwa siku za karibuni. Nilishangazwa na umoja wenu mlionyesha katika jambo hili lenye maslahi kwa kizazi chetu na Kijacho. Kura yangu, Kura za Familia Yangu na Kura za Wanakijiwe Wenzangu unazo 100%.
Asante sana - IPP na UKAWA