Asante Rais Samia kwa hotuba nzuri Siku ya Wanawake Duniani

ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,417
1,829
Mimi binafsi namshukuru sana Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania kutokana na yale yaliyojiri jana tarehe 8.3.2023 alipokuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa kina mama wa Chadema (BAWACHA).

1. Kwanza kabisa namshukuru sana kwa kusema HATA YEYE anasoma Jamii Forums. Hii ni tofauti sana na mtangulizi wake aliyetaka kuwafunga wakurugenzi wa JF kwa kuwafungulia kesi za ajabu ajabu. Kama Rais anasoma JF maana yake ni kwamba anawajali wananchi wake hivyo anataka kusikia maoni ya wananchi wake moja kwa moja na sio kupitia wanaojiita "chawa" wake ambao mara nyingi wanampa ripoti za uongo.

2. Jambo la pili nalomshukuru Rais ni jinsi katika hotuba yake ALIONYESHA WAZI kwamba anaitakia mema nchi yetu, na ana mpango wa kuondoa uonevu wote uliofanywa na awamu iliyotangulia. Ushahidi wa jambo hili ni jinsi alivyohakikisha kwamba kesi zote zilizokuwa zimefunguliwa kisiasa kugandamiza wapinzani zimefutwa.

Naamini wanaJF wenzangu tutashirikiana kumpa support Rais. Kama ni kukosoa mambo yanayofanywa na viongozi wa serikali yake, tukosoe lakini sio kwa matusi bali tumpe ushauri wa namna ya kuondoa hayo matatizo.

Nawaomba WaTz wenzangu tutambue kwamba SIO RAHISI (hata ungekuwa wewe), kuondoa kwa siku moja, mapungufu yaliyojikusanya kwa miaka 62 tangu tupate uhuru.

Tumpe Mama Yetu muda wa kufanya marekebisho na tum-support
 
Back
Top Bottom