Asante Mungu Kwakunipa Ajira

Asante Mungu Kwakunipa Ajira

lazima ukae

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2013
Posts
791
Reaction score
417
Habari zenu wadau,
Napenda kutumia fursa hii kumshukuru Muumba mbingu na nchi kwakunipatia ajira hatimaye na mimi sasa natoka asubuhi na kurudi jioni.Vilevile napenda kuwakumbusha vijana wenzangu kwamba kukata tamaa ni mwiko na mjitahidi kutuma maombi ya kazi pindi zinapotangazwa na ipo siku Mungu atawajaria.
 
Kuwa mtumishi mzur na zingatia ethics za kazi yako.

Mungu akuongoze na akulinde mi bado nahangaika..
 
Nianze kwa kukupa Pole hasa wakati ule uliposota na kutafuta Kazi,Hata mie hiyo Hali ilinipata Ndani ya mwaka mzima nasaka Kazi,Ilifikia hatua napata mlo mmoja tu kwa kuwa sikuwa na hela ya kujikimu,Ila Leo nami naungana Nawe kumshukuru MUNGU kwa wema alionitendea,Vijana wenzangu tukipata Kazi tumkumbuke sana MUNGU na kuwasaidia wenzetu.
 
Shukran kaka Mungu atakubariki
 
Umepata kazi sasa fanya kazi. All the best.
 
Hongera sana, kumbuka kutimiza wajibu wako na umuombe sana Mungu maana huko makazini majungu hayaishi
 
Hongera sana mkuu!as for me now naingia mwaka wa 3 wa utafutaji wa ajira all the best mkuu!
 
Jenga kwanza halafu oa halafu boresha familia achana na stare he ikiwezekana hata soda usinywe utafanikiwa
 
Hongera sana.
........ Usisahau ile sentensi ya mwisho kwenye maombi yako ya kazi
(Yours faithfully).......... keep it.
 
Back
Top Bottom