Asante Mungu kwa kuniondolea kimbelembele cha kuoa mapema

Asante Mungu kwa kuniondolea kimbelembele cha kuoa mapema

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
618
Nikitazama ndoa za Vijana wenzangu daah aisee naweza ua mtu. Hapa mtaani kuna mpangaji mwenzangu amekosana na mke wake usiku wa manane.

Asubuhi ya leo jamaa kaenda kazini, mchana huu msichana kaondoka na kila kitu cha ndani nimetafakari juu ya hili nikaona sina jinsi ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya hili kwasababu bado sijaoa.

Nakumbuka kisa alichopost member mwenzetu huku siku nyingi kidogo kuhusu kijana mwingine na maswahibu ya ndoa yake.

Ngoja nizeeke zeeke kwanza pengine nitakuja elewa.
 
Maisha yenyewe mafupi,endelea kula ujana.
 
Kwa kuwa mpangaji wako katendwa na mkewe, haina maana mkeo kama ungekuwa naye angekutenda namna hiyo. Acha uoga wa kuikimbia ndoa. Unataka kuoa uzeeni? :msela:
 
Kwani mkuu kuna wanawake wangapi wamebeba vitu vya ndani na kuondoka navyo wakiwaacha waume zao solemba mpaka ufikie hitimisho hilo?
 
Bado unacopy hadimaisha yandoa looh kweli wabongo vilaza subiria ucopy Na kazi ya mumewe pia
 
!
!
I miss my bachelorhood. Ila in hardly a week lazima nicheze bonge la movie niwe bachelor one more time.
 
Waolewaji ni shida tupu na waowaji hakuna yaaani mpaka raha
Mwanamke ukipata mwanume anaetaka kukuoa usichelewe kimbilia tenda iyo nafasi ni chachee
 
Kwa hyo unaona cfa kuendelea kuwa mzinzi sio?
 
Subiri subiri watoto waje wakuite babu,

ukizaa una miaka 35 ukifikisha 60 firstbone ana 25 bado tegemezi we subiri tu na tu na tu na tu, wenye vitimbwi wanapigana huku watoto wanakua, we umekaa tu. unazani aliye ondoka na vitu vyote jamaa hapajui kwao?
 
Unakaz nyie ndo wadandiaj wake za watu co
 
Subiri subiri watoto waje wakuite babu,

ukizaa una miaka 35 ukifikisha 60 firstbone ana 25 bado tegemezi we subiri tu na tu na tu na tu, wenye vitimbwi wanapigana huku watoto wanakua, we umekaa tu. unazani aliye ondoka na vitu vyote jamaa hapajui kwao?

Watakuwa walibebana bila ndoa hao, mke wa ndoa hawezi kufanya kitu kama hicho! Atakimbilia wapi na hivyo vitu?? Ni familia gani ya kipuuzi itakayompokea mtoto wao aliyeolewa kabeba vitu namna hiyo bila taarifa??
 
Unaamini katika samaki mmoja akioza wote wameoza?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom