Asante kondomu, hakika sio kwa ujanja wangu..!!

alexmahone

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
482
405
Salamuuuu..!!

Inafika muda unajaribu kuhesabu idadi yao unakuta unafika 300+, unaogopaaa unajishangaaa unajisema hawa ni watu etiii, unakumbuka zile takwimu zao kuwa wakiwa 10 basi mmoja wao kaathirika.Ukiweka uwiano kwa ulipopita unagundua hakuna namna unaweza kuwa hujakutana na walioathirika.

Ila niseme tu Kondomu imenibeba sana, ashukuriwe aliyegundua hii kitu.Laa sivyo Mafisi wengi tusingeweza kutoboa miaka hii tukiwa kifua mbele na ujasiri wa kuweza kwenda kupimwa HIV.

Ingawa matukio machache ya kupasuka yanatokea , lakini Dunia imekuwa rahisi siku hizi.Nakumbuka siku nipo Dom nakula whisky Pestana, mfukoni nina Pakti za Rough rider, shetani sio kiumbe mwema anatokea binti mmoja mzuriii, ana rangi ya mtume.Nikamfuata mezani, piga naye stori mbili tatu na kumchombeza akawa anatabasamu akaagiza wine nikamwambia kuwa huru mrembo twende tuburudike pamoja, nikagundua huyu baharia tuu, stori zikanoga daaaah kumbe kazunguka sehemu nyingi tuu keshadangaa mpaka Tunduma huko, kavuka na boda akatokea South Africa ila saizi nipo naye mezani kudadeq.

Muda ukayoyoma vinywaji vikakoleaa, saa sita kasoro usiku mkali tukatoka pamoja mpaka Lodge nilipofikia.Tukaingia bafuni kuoga, kisha tukaanza mtanange.Kidume nina Mpira wangu madhubutii nimeshauvaa hapo nina jiamini kwa asilimia zote kama Superman vilee.

Show inaendeleaa kwa kasi, nina spidi kama zote utadhani nimekutana na kigoriii, mara binti ananiambia kuwa anahisi mpira umepasukaa.
Nikamwambia hiyo brand haijawahi kuniangusha.Daaah baada ya kushusha waarabu, ile nachomoa nakuta kweli aisee kitu ilishapasuka kitambo...!!
Hapo akili ikanirudi, pombe ikaniisha nikajionaa nimepotezaa haraka nikakumbuka theory ya Zuma, kwa haraka nikakimbilia bafuni nikaoga tena awamu hii nika concetrate eneo moja zaidi, huku nikipaka sabuni nyingi daah kufa kunauma jamanii, ile narudi chumbani naona binti amejilaza kitandani ananiambia kuwa yeye alishajua alishangaa kwanini mimi sikutambua kuwa nishapasua.Anasema yeye hana shida maana amemaliza period soon so habari ya mimba sio rahisi kihivyo kwake.
Hapo nikajua nipo na kiumbe tofautii ambaye kwake hofu namba moja ni mimba tuu, vingine ni vya kawaida..!!

Nikaamua kumlipa chake, nikamwambia aende mimi nikabaki na mawazo kibao.Sikuwa na namna maana hata usingizi sikuwa nao tenaa, ikabidi nitoke hapo Lodge niende Rainbow, awamu hii nikaagiza maji tuu na slice za limao.Nikawa nimepoteza matumaini, mara jamaa ananishtua kwa bashasha kumbe ni rafiki angu kitambo anaishi Dom ni daktari anagundua sina furaha ananidadisi naamua kufunguka kwa uchungu kwa kilichotokea.Anasikitika ila ananipa moyo kuwa hilo tatizo dogo kwa miaka ya sasa, anasema nicheki kesho nikuunganishe na watu wa hicho kitengo kwenye hospitali anapofanyia ila itabidi usiseme ukweli huo inatakiwa kutengeza hadithi tofauti ili angalau waelewe kuwa sio kwa uzembe.

Nikamshukuru baada ya kunipa tumaini jipya la kuona mwanga kisha tukaagana nikarudi Lodge.
Kesho yake mapema nikafanya kama alivyonielekeza nikaenda mpaka hospitali nikajieleza nikapatiwa dawa zinaitwa PEP, baada ya wao kunipima HIV na kunikuta niko safi.Then nikaanza dozi ni dawa nyingi na nzito lakini nilifanikiwa kuzimaliza.
Hakika ni tukio zito lililowahi kunitokea lakini bado naziheshimu Kondomu na nilihesabu kama ajali kazini bado nazipa asilimia za juu kwa namna inavyo save maisha yetu sisi mabaharia wa nchi kavu.

Kila kherii wakali wa hizi mambo, KONDOMU ziheshimiwe na watu woteee..!!
 
Na kama yupo exposed na virus kiwango ambacho hakijafikia kuwa detectable?
Mm Sio mshabiki wa ndomu na nikiitumia lazma niivue...natembea na vipimo kwa emergency mnapima kwanza akigoma unamuacha aende...
 
Back
Top Bottom