Asante Kinana umetuokoa

Asante Kinana umetuokoa

Mpangamji

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2010
Posts
540
Reaction score
141
Namshukuru sana Kinana kwa kujitolea kufanya mdahalo na Dr. Slaa Star TV. nakushukuru kwa mambo yafuatayo
  1. umetuondolea aibu ya mgombea wetu kumuogopa mgombea wa Chadema ingawa wewe si mgombea lakini umeonyesha uwezo mkubwa wa kucheza na maneno, dhidi ya msomi huyu.
  2. nakushukuru kwa kupata muda wa kusema ukweli unaotukabili kwa sasa kuwa ushindi kwa hali iliyopo si lazima ni hivyo kufuta usemi wa uongo wa kuwa ushindi ni lazima.
  3. nakushukuru kwa kuonyesha kuwa una ujasiri mkubwa, na hivyo kuwaonyesha wanachama wa chama cha kijani na njano kuwa wewe unafaa zaidi kugombea na Dr. kuliko anayemuogopa Dr.
  4. nakushukuru kwa kuendelea kutumia akili yako na uwezo wako wa kujieleza kufunika hoja zinazotolewa na wapinzani ikiwemo ya matumizi ya ndege za serikali na magari ya serikali aliyokuwa anatumia mama na kijana wetu.
natoa pole, kwako na sisi wengine kwa kuwa haya yote unayoyafanya na kwa kuzingatia tamko lako la jana kuwa ushindi si lazima tutapata shida, kwani hawa jamaa wakiingia madarakani hawalipi fadhila kama sisi. wao wanaangalia uwajibikaji na uadilifu.
nakuhakikishia tu kwamba kura yangu mwaka huu nitampa Dr.
Hata hivyo hongera sana.:lock1:
 
Sasa CCM ilikosea kutomteua Kinana kuwa mgombea nini?
 
Unajua mwongo akisimamia uongo anaonekana jasiri.

Kinana anaposema kikwete ametekeleza ahadi kwa silimia tisini alikuja na jedwali la ahadi na kutonesha zipi zimetimizwa na zipi bado?

Wizi mtupu
 
Sasa CCM ilikosea kutomteua Kinana kuwa mgombea nini?
Hapo zamani Kinana alikuwa mbunge huko arusha ,alipotaka kugombea kwa mara ya pili akatishiwa nyau kuwa yeyey si raia kwao ni Somali,lakini pia Kinana ana mawaa kibao si msafi,pia ndie mwakilishi wa mwarabu wa Loliondo ,mwarabu anayetesa wananchi wa huko Loliondo.Nafikiri tumesahau aliyoyasema mama Sophia Simba kuwa CCM hakuna msafi
 
Mambo ya kipanga wetu hayo!!!! Ndo matatizo ya kuzoea kudesa
 
CCM hawajui side effect ya debate ya Slaa na Kinana.
 
Kinana kumpakata Kikwete - kwani amekuwa kiwete ?
 
Sasa CCM ilikosea kutomteua Kinana kuwa mgombea nini?

Unajua kwa nini aliwahi kuenguliwa kwenye kinyanganyiro cha ubunge wa Arusha miaka ya huko nyuma? "siyo mtanzania."
 
Raisi wa TZ mwaka 2015

Mzee wa Chalinze akianguka safari hii hanyanyuki na mrithi huenda akawa msomali wetu Kinana. By the way huyu si ndugu na Bashe?? sasa ilikuwaje akamtosa?:help:
 
Mzee wa Chalinze akianguka safari hii hanyanyuki na mrithi huenda akawa msomali wetu Kinana. By the way huyu si ndugu na Bashe?? sasa ilikuwaje akamtosa?:help:

Yaani huyu mzee mwezi ukiwa mchanga anashida kweli!halafu mbali na kuanguka hivi hakomi videmu
 
hiv kinana alikuwa anasemea nchi ipi? tanzania au nchi yake ya somalia. ajitaidi aksemee kule somali angali kuwe na serikali, atuache na nchi yetu
 
It is a shame kwa CCM kumleta mtu aliye na uchache wa hoja na upungufu mkubwa wa uzalendo kusimama na Dr Slaa... wapo wapi watanzania wa kweli waliojigamba kwamba wanaipenda nchi yetu kama akina Makamba? Yupo wapi rais wetu mwenye huba na bashasha na rekodi ya mafanikio kwa asilimia tisini??

Kwanini hatukumuona makamu mwenyekiti wa CCM mwenye rekodi ya uadilifu na historia ya bunge pevu?? Hivi yule katibu mwenezi wa chama vipi??

Pole sana mwanaCCM mwenye vision na upeo zaidi kwani kama mmefikia hatua ya kuleta mtu asiye na nafasi yoyote chamani wa serikali kusimama na kunadi sera na mafanikio yenu mjue mmefulia sana ..... katika wamatumbi wooooote mmeamua kumleta huyo?

Nafananisha na mwanafunzi anayekodi mamluki kumsaidia kuandika thesis

zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama chetu.... Haya yote niliyasikia jana brake point mtu akimpa kada wa chama za uso
 
Back
Top Bottom