Namshukuru sana Kinana kwa kujitolea kufanya mdahalo na Dr. Slaa Star TV. nakushukuru kwa mambo yafuatayo
- umetuondolea aibu ya mgombea wetu kumuogopa mgombea wa Chadema ingawa wewe si mgombea lakini umeonyesha uwezo mkubwa wa kucheza na maneno, dhidi ya msomi huyu.
- nakushukuru kwa kupata muda wa kusema ukweli unaotukabili kwa sasa kuwa ushindi kwa hali iliyopo si lazima ni hivyo kufuta usemi wa uongo wa kuwa ushindi ni lazima.
- nakushukuru kwa kuonyesha kuwa una ujasiri mkubwa, na hivyo kuwaonyesha wanachama wa chama cha kijani na njano kuwa wewe unafaa zaidi kugombea na Dr. kuliko anayemuogopa Dr.
- nakushukuru kwa kuendelea kutumia akili yako na uwezo wako wa kujieleza kufunika hoja zinazotolewa na wapinzani ikiwemo ya matumizi ya ndege za serikali na magari ya serikali aliyokuwa anatumia mama na kijana wetu.
natoa pole, kwako na sisi wengine kwa kuwa haya yote unayoyafanya na kwa kuzingatia tamko lako la jana kuwa ushindi si lazima tutapata shida, kwani hawa jamaa wakiingia madarakani hawalipi fadhila kama sisi. wao wanaangalia uwajibikaji na uadilifu.
nakuhakikishia tu kwamba kura yangu mwaka huu nitampa Dr.
Hata hivyo hongera sana.:lock1: