Asante JK kwa kutuvutia gesi kutoka Mtwara hadi Ubungo! kwa ukame huu mgawo wa umeme usingeepukika. Uliona mbali sana mzee wetu. Gesi hii ya kutoka Mtwara ndo inayoendesha mtambo wa Ubungo II wenye uwezo wa kuzalisha MW 105, mitambo ya Symbion MW 112 na Kinyerezi I, MW 150. Kwa niaba ya watanzania nakushukuru sana Mzee JK umetuacha pazuri! huenda tungekuwa tunaambiwa kwani ukame umeletwa na serikali au na CCM? na tusingekuwa na cha kujibu!
TUJIKUMBUSHE HABARI HII CHINI
............................................................................................................
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Felchismi Mramba, amesema shirika hilo lipo kwenye hatua za mwisho za majaribio ya kuwasha mitambo ya gesi asilia kupitia mitambo ya Kinyerezi I na baadhi ya maeneo ya nchi wameanza kupata umeme wa uhakika tangu jana.
Amesema mafundi wamefanikiwa kuwasha jenereta 10 za Ubungo no.1, hivyo mpaka kuanzia leo uzalishaji umeme utakuwa umeongezeka.
Amesema sehemu kubwa ya kazi hiyo imekamilika na kwamba leo wataanza kufungulia gesi hiyo kwa presha kubwa kwa ajili ya kutoa uchafu wote ambao unaweza kuwa umebaki katika kipande kidogo cha bomba linalounganisha mitambo ya Ubungo.
Aidha, amesema kazi hiyo itachukua muda mfupi na leo asubuhi wataanza kuwasha mitambo hiyo na kuwa kazi ya kuwasha mitambo mingine itaendelea kwa sababu mabomba mapya kama hayo na mitambo inayopokea gesi hiyo kwa mara ya kwanza hawawezi kuifungulia yote kwa wakati mmoja.
Hata hivyo, ameeleza kuwa wanachokifanya nikuingiza mtambo mmoja baada ya mwingine huku wakifuatilia presha kwenye bomba kuwa inaingia vipi na pia mitambo mipya itaanza kuingia na wataanza na baadhi ya mitambo iliyopo Ubungo na katika mitambo mingine kutegemeana na presha yake itakavyokuwa.
Gesi ya kutoka Mtwara inategemewa kuendesha mtambo wa Ubungo II wenye uwezo wa kuzalisha MW 105, mitambo ya Symbion MW 112 na Kinyerezi I, MW 150.
Kwa mujibu wa Mramba, Mtambo wa Ubungo I utaendelea kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ya Songosongo na kwamba Ubungo II ndiyo utumia gesi ya Mtwara kwa kuwa inatosha kuendesha mitambo hiyo. Uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi utaisaidia serikali kuokoa takribani dola za Marekani bilioni 1 kwa mwaka, ambazo zilikuwa zinatumiwa kununua mafuta mazito ya kuzalisha umeme.
Hali ya umeme inatarajia kurejea katika hali yake ya kawaida nchini kote Ijumaa wiki hii.
Meneja Mawasiliano wa Shirika hilo Adrian Severin amesema zoezi la kuunganisha bomba la gesi kutoka Mtwara na kufikisha Kinyerezi hatimaye Ubungo jijini DSM lililoanza tarehe 7 hadi 14 mwezi huu limekamilika.

- Sehemu ya habari iliyonukuliwa kutoka FikraPevu.com - Mitambo ya Umeme wa gesi yawashwa, baadhi ya maeneo yaanza kupata Umeme wa uhakika