Asante JF kwa kutunza kumbukumbu. Hii ndiyo ilikuwa post yangu ya kwanza kabisa toka nijiunge na JF tarehe 31/5/2008!

Mkuu heshima kwako. Unasomeka vyema.
Hili la kutopiga kura limeniuma. Yawezekana kuna wengi kama wewe ambao hatupigi kura.
"Don't boo, vote." Alisisitiza Obama.
Pamoja na yote, tusikate tamaa na kuwaachia kina Mbowe vita hivi peke yao.
Ndugu yangu, kwa Katiba na mfumo wa sasa, kweli unaamini kura yako ina maana yoyote? Wanapojisahau hawa viongozi wetu, wanajikuta wakitoa kauli ambazo zinaweza kutolewa tu na walevi wa madaraka...
  • Msipigie kura kwa Chama Kingine kwa sababu hata mkipigia kule, Chama Cha Mapinduzi kinaenda kuunda serikali.
  • CCM hata akibaki mtu mmoja tutashinda tu na hatutaachia dola hata iweje
  • Mkuu wa polisi Mkoa akimfokea kiongozi wa upinzani, "Hushindi, nakuambia hushindi wewe"
  • Nikulipe mshahara halafu umtangaze mshindi mpinzani, thubutu!
Kauli kama hizo zinaashiria nini ndugu yangu brazaj? Kura yako haina umuhimu wowote ni bora hata usipige. Kama sote tungesusia uchaguzi lazima tu mabadiliko yangewezekana.
 
2008 ndo nipo advance dah kitambo sana
Miaka 4 baadae 2012 ndo najiunga rasmi JF na simu yangu ya kwanza Nokia C2-00
Live long
JF
 
Hongera sana mkuu
 
Hongera sana mkuu
 
Mkuu respect. Nyie ndo wazee/ makaka zetu humu
 
Maandishi yanaishi
Toka najiunga na Jamii Forums nilisema na kusisitiza kuwa adui nambari wani wa taifa letu, Tanzania, ni CCM. Huu msimamo nimekuwa nao hadi leo haujabadilika na kila nikipata nafasi ya kuchangia nakazia hapo hapo.

Nikisema sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa wachache sana wataamini kwani kulingana na mawazo ya wengi mkosoaji mkuu kama mimi lazima ni Chadema...Chadema hata ofisi yao sijaikanyaga, nasikia tu iko UFIPA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…