stujadiliane
Member
- Jun 2, 2017
- 66
- 84
Napenda kuwashukru kwa dhati benki ya NMB makao makuu wa kusiliza kilio changu. Baada ya kuposti usiku wa kuamkia leo kuwa benk ya NMB wamenifanya kuwa ombaomba, NMB makao makuu wamenipigia simu.
Rejea >>> Benki ya NMB wamenifanya ombaomba baada ya kuibiwa pesa zangu nilizolimbikiza kwa miaka kadhaa
Nawashukru kwa ushirikiano ambao wamenionesha naamini kuwa suala hilo watalishughulikia mapema iwezekanavyo.
Kwa sababu hiyo nasitisha kwa muda taratibu zote ambazo nilikuwa nimepanga kuzifanya ili kuwapa muda wa kushughulikia suala langu.
(1)Nakumbuka nilikuwa najiandaa kuweka vielelezo vyote hapa JamiiForums. (2) Nilikuwa najiandaa kusafiri mpaka Dodoma ili kuonana na Waziri wa Fedha. (3) Nilikuwa najiandaa kumuandikia Mh. Rais Magufuli. (4) Na mwisho nilikuwa najiandaa kufungua kesi mahakamani ikiwa hatua yangu ya mwisho.
Nashukuru sana JamiiForums pia wadau wote mliochangia na zaidi nawashukuru NMB Bank makao makuu kwa kujali kilio changu na kuahidi kulishughulikia upesi.
Mungu awabariki sana