Asante benki ya NMB kwa kusikia kilio changu

stujadiliane

Member
Jun 2, 2017
66
84
Napenda kuwashukru kwa dhati benki ya NMB makao makuu wa kusiliza kilio changu. Baada ya kuposti usiku wa kuamkia leo kuwa benk ya NMB wamenifanya kuwa ombaomba, NMB makao makuu wamenipigia simu.

Rejea >>> Benki ya NMB wamenifanya ombaomba baada ya kuibiwa pesa zangu nilizolimbikiza kwa miaka kadhaa

Nawashukru kwa ushirikiano ambao wamenionesha naamini kuwa suala hilo watalishughulikia mapema iwezekanavyo.

Kwa sababu hiyo nasitisha kwa muda taratibu zote ambazo nilikuwa nimepanga kuzifanya ili kuwapa muda wa kushughulikia suala langu.

(1)Nakumbuka nilikuwa najiandaa kuweka vielelezo vyote hapa JamiiForums. (2) Nilikuwa najiandaa kusafiri mpaka Dodoma ili kuonana na Waziri wa Fedha. (3) Nilikuwa najiandaa kumuandikia Mh. Rais Magufuli. (4) Na mwisho nilikuwa najiandaa kufungua kesi mahakamani ikiwa hatua yangu ya mwisho.

Nashukuru sana JamiiForums pia wadau wote mliochangia na zaidi nawashukuru NMB Bank makao makuu kwa kujali kilio changu na kuahidi kulishughulikia upesi.

Mungu awabariki sana
 
Hivi mpaka waandikwe vibaya kwenye mitandao ya kijamii ndo washughulike na matatizo ya watu??? Tena kwa kitishiiwa
 
bank teller kazi ya kidwazi sana nilikuwa naa dream nayo lakin na wao ni wapigaji mungu ana waona
 
Ndugu stujadiliane
Kama ni miaka kadhaa sasa imepita toka upoteze pesa zako basi nakushauri ufungue kesi mahakamani, weka na wakili Mkuu upate stahiki zako pamoja na usumbufu wote. Hawezi kukupotezea milioni hamsini halafu waje kukurudishia milioni hamsini baada ya miaka mitatu, no way...pesa haiko hivyo, ndiyo maana wao ukikaa na pesa yao wanahesabu ziada kila unapobaki nayo. Ongea na mwanasheria, mwoneshe vielelezo vyote, usiogope gharama zitarudi tu.
 
Napenda kuwashukru kwa dhati benki ya NMB makao makuu wa kusiliza kilio changu. Baada ya kuposti usiku wa kuamkia leo kuwa benk ya NMB wamenifanya kuwa ombaomba, NMB makao makuu wamenipigia simu.

Rejea >>> Benki ya NMB wamenifanya ombaomba baada ya kuibiwa pesa zangu nilizolimbikiza kwa miaka kadhaa

Nawashukru kwa ushirikiano ambao wamenionesha naamini kuwa suala hilo watalishughulikia mapema iwezekanavyo.

Kwa sababu hiyo nasitisha kwa muda taratibu zote ambazo nilikuwa nimepanga kuzifanya ili kuwapa muda wa kushughulikia suala langu.

(1)Nakumbuka nilikuwa najiandaa kuweka vielelezo vyote hapa JamiiForums. (2) Nilikuwa najiandaa kusafiri mpaka Dodoma ili kuonana na Waziri wa Fedha. (3) Nilikuwa najiandaa kumuandikia Mh. Rais Magufuli. (4) Na mwisho nilikuwa najiandaa kufungua kesi mahakamani ikiwa hatua yangu ya mwisho.

Nashukuru sana JamiiForums pia wadau wote mliochangia na zaidi nawashukuru NMB Bank makao makuu kwa kujali kilio changu na kuahidi kulishughulikia upesi.

Mungu awabariki sana

Umeahidiwa wasipotekeleza uje tena.
 
Hivi mpaka waandikwe vibaya kwenye mitandao ya kijamii ndo washughulike na matatizo ya watu??? Tena kwa kitishiiwa
Ila kwa bahati mbaya mabwana wale ukiwaandika tu wasivyotaka wao utaamkia posta
 
Niko makini sana na hili kwani pesa zangu zina miaka zaidi ya mitatu.wasipo timiza ahadi yao nitarudi hapa na makrabasha yangu yote. Na nitaendelea na tua zangu muhimu. Ni kweli ni mepoteza muda mrefu biashara yangu imesimama familia yangu imeangaika sana
Kusema kweli naitaji kudai fidia.kama nitalazimika kufika mahakamani basi nitadai fidia tena kubwa.ila wakinilipa pesa zangu mapema kabla ya week mbili nitawasamehe
 
Mkuu yaan mtu anahamisha pesa zako bila ridhaa yako yaan anakuona kama vile bashite...walaaniwe hao wez
 
Kaza hapo hapo hadi wakulipe.., washenzi sana hawa, ina maana usingeandika humu wangeendelea kukuzungusha, si ndio maana yake?!
 
stemcell
Fafanua zaid kuhusu kufilikisa kwa benk then mim niliye kuwa na million 100 nipate 250,000/- .Mkuu tafadhal maana hii hali ya Mh. ngumu unaweza sikia benk fulan imefirisika ghafla
 
Jambo likishindikana jf basi tena.

Ona sasa kumbe wamo humu. Usingelalamika wanazitafuna
 
Safi sana NMB kwa kusikiliza kilio hiki, endeleeni kufanya kazi kwa juhudi kubwa zaidi
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom