Asante Bashiru, tumewajua machawa Halisi

Pengine ni kwamba Makada hao wamepitwa na wakati sasa!

Nyakati za kutetea chama badala ya wananchi zimekwisha pitwa!

Leo hii ni wananchi kwanza kisha ndio Chama!

Hakuna chama bila wanachama!

Hao "makuda" wanatetea matumbo yao na sio kingine!
Hili haliwezekani kwanza tujiulize nini maana ya chama. Kuwa kwenye chama ina maana unakubaliana na sera za chama na lengo la chama ni kutawala ili utawale lazima muwe pamoja hasa mkimaliza mambo yenu ya ndani ya chama mkiyamaliza mkitoka mnamkabili mpinzani kwa sauti moja. Hili unalotaka kusema hapa hata huko majuu hutoboi ukiwa uko nje ya chama. Kila chama kina taratibu zake za kufanya maamuzi na wanakosoana tu ila mkimaliza mnatoka wamoja sasa huwezi kutoka nje ukaanza kuwakosoa wenzano wakati unajuwa lengo ni kushika dola. Sio huyu Bashiru alisema huwezi kuwa na dola halafu usitumie dola kubaki madarakani au sio yeye? Chama ni kundi la watu wenye mawazo na malengo yaliofanana na wajibu kusimamia maamuzi ya chama. ndio maana hata uwe mkubwa vipi hata Mama Samia sio raisi lakini sio lolote akitoka nje ya CCM
 
Ukiwa kada mtiifu lazima upiganie chama chako na viongozi wako.
Mbona sasa unarukaruka, nimekujibu vile baada ya wewe kusema ni kada mtiifu ndio maana nikauta wewe ni tools ya watu kufikia malengo yao. Hakuna cha ukada wala ukamanda zote ni tools tu za wanasisa kufikia malengo yao.
 
Chama ni kundi la watu wenye mawazo na malengo yaliofanana na wajibu kusimamia maamuzi ya chama
Hii tafsiri ya kiujanja ujanja tu. Chama ni kikundi kidogo cha watu waliojipanga kuwatumia wananchi wajinga kufanikisha mambo yao.
 
Mbona sasa unarukaruka, nimekujibu vile baada ya wewe kusema ni kada mtiifu ndio maana nikauta wewe ni tools ya watu kufikia malengo yao. Hakuna cha ukada wala ukamanda zote ni tools tu za wanasisa kufikia malengo yao.
Ndio maana ya siasa nashaka hujasoma mambo ya siasa ukijuwa maana yake huwezi kuandika ulichoandika, ni sehemu ya siasa kawaida kabisa
 
Ila kusifu na kuabudu si ndio alianzisha yeye?
 
Hii tafsiri ya kiujanja ujanja tu. Chama ni kikundi kidogo cha watu waliojipanga kuwatumia wananchi wajinga kufanikisha mambo yao.
Labda kuna wajinga kwentu na huko majuu utatoboa kama wewe sio Republican au Democratic au Conservation au labour hata mikopo tu hujajiunga Saccos hutoboi na kusema wanawatumia wananchi kina nani? hakuna mtu kazaliwa kiongozi wanapigana kwenye mfumo huohuo kutoka zero nakuja kuwa kiongozi. Ni system lazima upigane ili ufike juu kama huwezi una support tu ndio maisha. Hata mpira ziko team tunashangilia tu lakini sio lazima uwe kiongozi na vyama ni hivyo huwezi kupigana shangilia tu.
 
imeandikwa "Koleza kuni mbichi ndani ya shimo ..... wahuni lazima waibuke"
 
Umewaita watu machawa wakati ulichofanya ni uchawa ule ule tu. Bashiru anasumbuliwa na 'uhaya' kudhani anachojua yeye ndio sheria na ndio mipaka ya mtu mwingine ya kuelewa jambo,.

Hata bosi wake wa zamani hayati JPM alikuwa anasumbuliwa na matatizo haya haya tu, anaelezwa kitu na mtaalam fulani na ghafla anamkatiza katikati kabla hata hajafikia mwisho wa maelezo yake, ni ugonjwa wa ujuaji ule ule tu!.
 
muulize mwalimu wangu Bashiru wale waliounga mkono juhudi kama mwita waitara na wengine wengiii kisha nchi ikagharamia chaguzi kwa kuwarudisha kwenye majimbo yale yale kisiasa INAITWAJE?
Mlikemea uchawa ule tena uliokuwa na gharama kwa walipa kodi kwa kiasi gani?
Bwana Bashiru alishawahi kuwambia wananchi wahoji na lile?
acheni unafiki wenu nyinyi
KAMFUFUE UZIKWE WEWE
 
Kuna mtu alitembea pale ikulu kutoka getini mpaka karibu na mlango wa kuingia ndani akiwa na kitambaa mkononi akifuta jasho. Sidhani kama msomi Bashiru anakumbuka kero ile pamoja na ile ya kurekodi maongezi ya viongozi wenzake wa CCM na kuiweka nchi katika hali ya uoga.

Malipo ni hapa hapa chini ya jua.
 
huyu ni msomi mnafiki aliyetupwa nje ya mfumo tu. hana kipya
 
Hivyo vibonzo vimenifanya nicheke huku moyoni nahuzunika!
 
Wajinga watasema kwasababu yeye ni ccm,ama kwasababu alikuwa anamsifia Magu basi hana uhalali wa kusema ukweli.

Hata Magu alipokuwa anapambana na ufisadi na uzembe kazini walisema kwakuwa nayeye ni ccm kwamba angekuwa mzalendo angejiuzulu zamani ilikuonyesha hapendezwi na ufisadi.
 
Hali inazidi kuwa mbaya kwa wahuni na mafisadi.
 
Leo hii Bashiru anaonekana mwamba haha
Yaani ndomaana nasema waafrica tunalaana ya asili. Eti watu wameshupaza shingo kuwa bashiru ni mwamba . Kwa lipi haswa. Huyu alooshindwa kutetea maslahi ya wafanyakazi kwa miaka 5 ya magufuli eti Leo hii anahuruma na wakulima? Afu watu walivyo wajinga washamuona ni mtu wa maana. Mimi npo na Mama Samia kwa sababu naona yanayofanyika ni makubwa Kama ni changamoto zitata tuliwa kadili uwezi utakapokuwa unapatikana. Wakulima matatizo yao miaka dahali.
 
Asante mkuu napenda watu wenye uelewa wa Mambo. Bashiru Hana sababu ya kulaumu utawala wa mama samia
 
Asanteeee mkuu . Baelezeee wajinga wakubwa hawa.
 
Na sisi wananchi ndio tunawaendekeza, kwasababu wakija na propaganda zao hazina kichwa wala miguu tuna washangilia, na ndio wanachukulia kama advantage kutu dalali.
Ndugu, Wanaibua kura. Wananchi Si wajinga.

Wamekata tamaa, kama UVCCM viongozi wanaonunua uongozi Kwa pesa, lifuatalo ni kutafuta mbinu za kuiba kura baas.

Tuungane kuhakikisha, Haufanyiki uchaguzi wowote bila kupata kwanza TUME HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Ameeeen.
 
Ni sahihi unachokisema, lakini kuna haka kamtindo wanakuja sehemu, mfano wanawakusanja wakulima au boda boda wanawapanga wasifie ujinga.
Nyerere alisema TUWAZOMEE viongozi wa namna hiyo, utendaji duni hafu watafute kusifiwa!! naona Utaratibu huo umeanza kuasahaulika.
 
BTW uchawa uliasisiwa rasmi awamu ya tano tena ile ilikua mbaya kuliko ya sasa maana ole wako upinge mamb yao, ukosoe mambo yao na kibaya zaid umkosoe mkuu 😂😂 hakuna rangi utaacha ona mkuu na unapelekwa kuzimu mazima!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…