Asante Ali Hassan Mwinyi. Hussein Mwinyi aliandaliwa, ni mwadilifu!

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,398
1,264
WanaJF

Salaam!

Maji hufuata mkondo wake - Rais wa awamu ya pili wa JMT alijizaa mfano wake. Hussein Ally Hassan Mwinyi (Rais wa sasa wa nchi ya Zanzibar) ni kiongozi shupavu na mwadilifu sana!

Chini ya uongozi wake naiona Zanzibar inayofunguka - naiona Zanzibar inayobadilika - naiona Zanzibar inayokua.

Aidha, rekodi zake akiwa Waziri wa Serikali ktk JMT kwa nafasi ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa sikuwahi kusikia, kuona ama kupata taarifa inayomtuhumu na ufisadi wa mali na rasilimali za taifa. Hii inanisukuma kumpa "BIG Up". Mengine nayompongeza ni:-

(a). Kukubali maridhiano kati ya Serikali yake na upinzani hususan ACT Wazalendo. Kwa utamaduni wa CCM si rahisi kukubali kufanya kazi ya ujenzi wa taifa kwa kushare madaraka!

(b). Miradi ya mikakati ya utafiti na uchimbaji mafuta, ujenzi wa barabara au daraja toka Zanzibar mkp Dar, ujenzi wa barabara za mitaani, utoaji mikopo kwa Jamii ya wazanzibar, uwajibishaji viongozi wazembe - kama aliyepata ajari tz akaachwa tu nk hivi ni baadhi ya vitu vinavyovutia sana.

(c). Kutopenda kutukuzwa - wapo viongozi wanapenda utukifu uliopitiliza, wanaofumbia uovu hasa ufujaji mali za umma (rejea taarifa za CAG) zinavyofunikwa na baadhi ya viongozi.

Nasema, Hussein Ally Hassan Mwinyi hongera sana kwa kazi na utumishi uliotukuka.

Msakila Kabende
Kakonko
 
Umeongea utopolo mtupu. Mwinyi alianza vizuri lakini siku zinavyoenda anakwenda kinyume na yale anayoyahubiri.

1. Suali la maridhiano keshaanza kulivunja kwa kumchagua mkurugenzi anaepigiwa kelele na wapinzani. Kafanya jeuri kubwa kumteua. Lakini pia maridhiano makubwa huonekana wakati wa uchaguzi na kuna uchaguzi tayari zishaanza kuvurugwa kama uchaguzi wa Amani. Uchaguzi mkuu ukifika ndioo tutajua mbivu na mbichi.

2. Hio miradi ya kimkakati unayosema hakuna hata mmoja ulokua realistic. Hilo daraja la kutoka Dar mpaka znz ni ndoto za alinacha. Hizo barabara za mitaani ziko maeneo ya CCm tu, huku mjini ni vumbi tupu na mashimo. Inaonesha mji wa znz huujui. Njoo malindi kwenye mataa uone hali ya barabara ni kama somalia au Afghanistan.

3. Hilo la kutopenda kutukuzwa nalo halina mashiko kwani anasifiwa na kupigiwa debe na chawa wake kama kawaida. Tokea lini chakula kikakosa nzi
 
Pia kuna upandaji holela wa kodi na usumbufu mkubwa kwa wafanyabiashara ambao hapo nyuma haukuwepo.

Mwinyi ni kiongozi mzuri ila inaonesha hapendi kushauriwa na hapendi kusikiliza maoni
 
SIYO kosa lake sbb hakujitangaza - tutamulaumu kwa lipi?
Huwezi kumsifia Hussein Mwinyi hii Nchi sio ya Kisultani kama familia zao zinajisimika kututawala Nyerere angeweza kutuwekea Makongoro badala ya Ally Hassan Mwinyi.
 
Very humble guy namkubali sana ukimsikiliza ata anavyoongea unamuona anamaanisha anayoyasema Allah amuhifadhi Kaka yetu huyu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom