Asaidiwe vipi! True story

Asaidiwe vipi! True story

mimisa

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
2,511
Reaction score
1,441
ameolewa ana miaka 11 ndani ya ndoa na ana watoto wawili,wa kike na kiume..Akiwa na miaka mitatu ndani ya ndoa aligundua kua mumewe hajatulia,alikua ana mahusiano nje na wanawake wenye uwezo tu,na huko yy alikua akijinadi kua yuko single ila ana maid nyumbani anaemlelea wanae baada ya kuachana na mkewe miaka ming ilopita..tabia hii iliendelea mpaka wakazaliwa watoto wengne wawili kwa mama tofauti,na kila mama akijua kua yuko peke yake ila kuna watoto ktk ndoa ya awali ya bwana huyu..muda mrefu wamekua na migongano ya hapa na pale ndani ya ndoa yao,chanzo kikiwa na kutokutulia kwa huyu shemeji yetu..maana wakat mwngine alikua anapotea nyumbani hata wiki,akirudi anasema alikua kapata kazi ya kulinda club,wakat mwingne anarudi na na kadi za bank ambazo wamiliki wake ni wanawake na mkewe akiuliza alikua anaambiwa ni za hawara wa marafiki zake na shemeji..ss majuzi,huyu shemeji yetu alikuja akawachukua watoto nyumbani,na alisema anatoka nao anaenda kuwafanyia shopping,na siku hiyo ilikua birthday ya mtt wake wa kwanza..kumbe uko alikua ameandaa birthday party ya mwanae huyo huku akisaidiana na mwanamke wake mwingne ambae amezaa nae mtt (ana uwezo sn kifedha)..baada ya sherehe kwa kua mtt mkubwa ana miaka 10 ss alikua anaona kila kinachoendelea,alipofika nyumbani alimuhadithia dada kila kitu..apo waligombana sn na mumewe bt bado wakaendelea kua pamoja..ss majuzi amekuja kugundua kua huyu shemeji ameoa,tena amefunga ndoa ya kiislamu..na anatambulika kwa jina la kiislam kwao na mwanamke alomuoa saiv..ikumbukwe kua dada yetu ni mkristo na uyu ana shemeji yetu uku upande wetu anajulikana ni mkristo..dada aligundua hili baada ya kujiunga facebook,so kuna watu walimtumia picha za mumewe akifunga ndoa hiyo msikitini na ktk sherehe pia..na yy alipochunguza sn alikutana na copy ya cheti cha ndoa cha mumewe na jina lake jipya la uislamun..dada yetu alifunga ndoa ya kimila tu na shemeji yetu huyu..ss anataka msaada.je asaidiwe vipi?..

NB..shemej yetu aliishia std 7,dada yetu form six..kuna wakat alipata nafac ya kusoma D.I.T bt hakumaliza,maana mumewe alikua akimfungia ndani kila akigundua kua ni wakat wa kufanya mitihani..hivo akashindwa kumaliza masomo yake..

jaman kusimulia wito..nivumilien ivo ivo..
 
Kweli dunia ina mambo!! huyo dada yako inawezekana anapendwa lakini huyo shemeji ndo anatafuta fedha kwa mtindo huo ili kujikimu kimaisha.
 
ss maisha gani hayo? shemeji mtaji alipewa..na bado hua anajishughulisha na udalali wa magari..kwa mtu mwenye mapenzi na mke angeweza kutulia tu na kutafta njia nyngne ya kipato..tofauti na anchofanya..ss dada uetu ndo anaetaabika
Kweli dunia ina mambo!! huyo dada yako inawezekana anapendwa lakini huyo shemeji ndo anatafuta fedha kwa mtindo huo ili kujikimu kimaisha.
 
Kama anapata mahitaji yake ipasavyo, avumilie tu, no way. Kizuri kula na mwenzako.
 
ku run anasita.anaumia kuwaacha wanae..maana kaambiwa na mumewe uyo akitaka kuondka aondokepeke yake..
Ushauri hapo ni ku run as fast as possible
 
sasa baad ya yote hayo bado anamsikiliza mumewe kweli? ni mume huyo sasa!??:angry:
 
Duh! Hii ni ngumu, wanaume wauza sura ni shida sana, anataka kulelewa na wanawake. Huyo dada ausikilize moyo wake tu, kama ana amani, amsamehe na aendelee kuishi na mumewe. Ndoa zina siri nyingi sana. Akumbuke pia - hakuna guarantee kama akimuacha mumewe ndio atapata furaha huko aendako lol!
 
Yaani ni ngumu sana ila kwa vile anawapenda wanae basi akae hapo kwa lengo kwamba "yuko hapo kwa faida ya watoto" yaani anawasindikiza watoto wakifika mahali watakapoweza kujitegemea wenyewe basi na yeye achukue ustaarabu wake.
 
atakapopata ukimwi ndo atajua kama hapo anakaa na wanae au gumegume...dume linakutenda hivyo unalivumilia ili iweje,damn! hayo ya uvumilivu hayapo dada siku hizi,,jamani wanawake gani hadi mwingine aone hasira juu yenu!!??
 
Ausikiliza moyo wake manake waweza sema aondoke kumbe yeye hayuko radhi. Aendelee kuwatunza wanawe huku akitarajia chochote hasa maambukizi ya magonjwa toka kwa mumewe. Asisahau Huu ugonjwa wa kisasa bado hauna dawa.
 
hana kazi yyt..na mama yake saiv kastaaf..so anawaza namna ya kuwalea wanae pia..na pia ushauri huu alipewa siku nyng sn..haufanyii kazi
asimsikilize
akimbie na wanae
 
Back
Top Bottom