Arusha yatikiswa mgomo wa daladala kutetea mbunge Lema

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
nanyaro.jpg

Kamanda Nanyaro Ephata, Mwenyekiti wa BAVICHA Arusha


Arusha imeingia doa kubwa mara baada ykuwepo kwa mgomo wa daladala ambao umedumu kwa masaa sita kutokana na kile kinachodaiwa kuwa Chadema wamekuwa wakinyimwa haki za msingi .



Mgogoro
huo ambao umesababisha madhara makubwa kwa mkoa wa Arusha hasa Leo kwa kuwa madereva wa daladala nao walisitisha safari zao za kubeba abiria kwa muda hali ambayo ilizua tafrani kubwa sana ndani ya jiji.

Bw. Ephata Nanyaro
mwenyekiti wa vijana kwa mkoa wa Arusha ambapo alisema kuwa hali hiyo ni mfano tu lakini itadumu endapo kama serikali itaendelea kuwapuuzia masuala yao mbalimbali ambayo wanataka yatekelezwe.

Aidha Bw Nanyaro aliendelea kwa kusema kuwa mara nyingi wamekuwa wakitoa maalamiko yao lakimi yamepuuzwa kwa kiwango cha hali ya juu amba moja ya hilo ni pamoja na mgogoro baina yao na mkuu wa polisi wilaya ya Arusha bwa zuberi Mwombeji.
Nanyaro alisema kutokana na kupuuzwa kwa madai yao mbalimbali kumeasabaiusha hali ya leo ya jiji la Arusha kukosa usafiri ambapo magari ya kubebea abiria katika kona zote nayo yaligoma kufanya kazi kwa mashinikizo hayo.

Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha
Bw Mwombeji alipoulizwa juu ya tuhuma hizo ambazo zinaelekezwa kwake na chadema alikana juu ya shutuma hizo na kudai kuwa yeye hayupo hivyo “ieleweke wazi kuwa mimi ni mtu mzima na kamwe kinachosemwa na Chadema si cha kweli ila wana mpango wa kunichafulia jina tu hamna kitu kingine"alisisitiza Bw Mwombeji

Kutokana na hali hiyo

Daladala za mji wa Arusha hazikuweza kufanya kazi na kutoa huduma za usafiri ambapo mgomo huo wa kushinikiza kuonewa kwa chama hicho na mbunge wa Arusha mjini Bw Goodbless Lema ulidumu kwa zaidi ya masaa sita huku daladala ambazo zilijaribu kufanya shuguli zake ziharibiwa na kuvunjwa vibaya na baadhiya watu ambao wanashinikiza juu ya kumkataa OCD na kupinga juu ya kuonewa.

Hata hivyo taarifa mbalimbali zizlizotolewa na na baadhi vyombo vya habari zilisema Mbunge wa Arusha mjini Bw. Godbless Lema amekwenda Rumande, mara baada ya kukataa dhamana hukiu wenzake wakiachiwa kwa dhamana katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kuitisha maandamano bila kibali cha Polisi
Na Gladness Mushi
 
sasa hapo wenye daladala wameikomoa serikali au wamewaumiza wananchi wa kawaida? mi nadhani ingetumika strategy nyingine lkn sio hiyo.
 
sasa hapo wenye daladala wameikomoa serikali au wamewaumiza wananchi wa kawaida? mi nadhani ingetumika strategy nyingine lkn sio hiyo.

Hapo kwenye usafiri hakuna asiyeathirika kuanzia mkulu mwenyewe, maana kuna mengi ambayo hayataenda kutokana na tabaka la watu wa chini ambao ndio watendaji, watekelezaji na wahudumu. Mambo yakiendelea hivyo hivyo kwa kakata masaa ya misafara ya daladala patafuka moshi kama wa volkano.
 
CCM na Jeshi la Polisi, Kamanda Lema nguvu ya umma wa walalahoi wote usiotikisika kote nchini wote tukisimama pamoja nyuma yake ...
 
Back
Top Bottom