Mji karibu wote wa Arusha kwa sasa habari kuu ni tukio la kukamatwa kwa Lema na jeshi la Polisi.
Makundi mbalimbali ya watu yamekuwa yakitafuta kwa udi na Uvumba kutaka kuona video inayomwonyesha Lema akiongea na Wanachuo wa IAA kwa nia ya kuwatuliza hasira baada ya mwanafunzi mwenzao kuuwawa kwa kuchoma visu na vibaka.
Video hiyo kwa sasa iko mitandaoni na CHADEMA mkoa wa Arusha wameahidi kuanza kusambaza DVD ya tukio hilo zaidi ya 3000 kwa wananchi wa Arusha kabla ya jumatatu ili waweze kujionea wenyewe namna Mbunge wao anavyopenda Amani na Busara katika kutatua migogoro ya kijamii bahati mbaya watawala wamemgeuzia kibao na kutaka kumwonea.
Hali hii inatabiriwa kuvuta watu wengi sana siku ya Jumatatu mahakamani ambako Lema atasomewa mashtaka, wengi wa watu wakitaka kuonyesha wanamuunga mkono mbunge wao na wanachuo kadhaa waliokamatwa.