Zapa RadioFm
Senior Member
- Feb 12, 2016
- 112
- 171
Kufuatia kufungwa kwa Chuo kikuu cha saint Joseph Kampasi ya songea wanafunzi wa chuo hicho kampasi ya Arusha wameanzisha mgomo wa kutoingia darasani wakidai kuwathibitishiwa endapo chuo hicho hakitafungwa kama ilivyotokea kwenye kampasi ya songea.
Madai ya wanafunzi hao ambao wameshuhudiwa wakiwa wamekusanyika nje ya majengo ya chuo hicho wakisubiri kujua hatma yao kuhusu uhalali wa chuo hicho kuendelea kutoa mafunzo hayo wakati chuo cha songea kikiwa kimefungwa.
wakiongozwa na viongozi wao ikiwa ni sehemu ya kushikiza kupewa taarifa rasmi ya ufumbuzi wa suala lao wanachuo hao wanaelezea hofu yao kuhusu hatma yao.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa chuo hicho Siles Balasingh amesema madai ya wanafunzi hao ni kutokana na hofu tu kwani tayari timu ya wakaguzi kutoka tume ya vyuo vikuu imeshafika chuoni hapo na kutoa taarifa kuwa kampasi zingine za chuo hicho zitaendelea na kutoa mafunzo kama kawaida huku akiwasihi kusitisha mgomo wao.
Chuo kikuu cha mtakatifu Joseph kiko nje kidogo ya jiji la Arusha na kinatoa program za ualimu katika ngazi mbalimbali.