Arusha: Walevi tuwe makini, Konyagi feki zitatumaliza

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,396
1621500326838.png


1621500364229.png


JAMAA WANA HADI STIKA ZINAZOFANANA NA ZA TRA



23MAY 2021

Nipashe Jumapili

Ashikiliwa na Polisi kuendesha kiwanda feki cha pombe
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kuendesha kiwanda feki cha kutengeneza pombe kali inayowekwa kwenye chupa inayofanana na ya Konyagi na kuziuza katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari nchini, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Justine Masejo, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kueleza uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini mtandao wote wa watengenezaji wa Pombo hiyo.

“Tunaandaa taarifa kamili ya tukio hili na tutawapatia, ni kweli limetokea katika Mkoa wa Arusha.”

Watuhumiwa hao walikamatwa juzi baada ya wananchi kuwafikishia taarifa polisi, waliposhuhudia kwa siku kadhaa vinywaji hivyo vikitoka katika nyumba hiyo iliyopo eneo la Elerai jijini humo.

Baadhi ya majirani wa nyumba hiyo, wamesema kwa muda mrefu walikuwa wakiona magari yakifika kuchukua bidhaa hizo.

Kwa upande wake, Balozi wa mtaa wa Kware kata ya Elerai, Ngoskeki James Meirura, amesema kabla ya kukamata vinywaji hivyo, alipokea taarifa ya kuwapo kwa kiwanda bubu, ndipo alipopeleka taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa na kisha kwa Jeshi la Polisi.

Askari walifika na kumkamata mtuhumiwa mmoja na wengine kukimbia.
 
Kwani walevi lengo lenu si kulewa tu? Kama lengo unalifikia ya nini kulalamika?
 
Ndo mana mm nakunywa Valeur kwa sasa. Kuna konyagi nilikunjwa nilihis kabisa hii ni fake
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom