ARUSHA: Viongozi wa CHADEMA wakamatwa kwa Amri ya Mkuu wa Mkoa

Hapo inaleta picha kwamba saa hizi sheria haina nguvu tena.
mie naona wanaosomea sheria ni kwa ajili ya wanyonge na sio kwa serikali, kwani hawako fair kabisa, na wanapata amri kutoka juu kwani hao wako juu ya sheria, wanajua kabisa hapa sheria itafanya hivi lakini kutoka na kauli za wanasiasa wanakuwa hawana la kusema, wanatii tu kwani wanalinda ugali wao, ila mtazamo wangu wanasheria na mawakili hawako fair na hasa pale wanaopingiza siasa, sasa sijui wamepoteza muda wao kwenda kusomea mambo ambayo baadae yanapigwa na wanasiasa
 
Hivi huyo kijana anaijua kesho yake? A nadhani atakuwa na mamlaka hayo milele? Mpaka u mauti umkute akiwa amekikalia hicho kiti? Haya. Ila mambo yote kwa Mr God tu
 
Kwa hiyo jamaa wameharabu machine za maji!!!!! ili iweje? wanamkomoa nani?? yaani hii Nchi maaajabu yataisha lini? wacha wachuane tu
 
Mh.Gambo huruma imemzidi mno, Hao walitakiwa siyo kukamatwa tu, wapigwe na viboko na kuteswa sana hadi waache hizo tabia za kichochezi.

Na kweli huruma imemzidi. Wangekuwa wa ccm na kutoka kanda ya ziwa ; Gambo angewapa mkate wa blue band na chai ya maziwa waburudike
 
Sasa na watu wachukue sheria mikononi kama hawa wateule nao hawaheshimu sheria na katiba. Mbona kosa hilo ni la kijinai ambalo polisi ndio wanapaswa kuchukua hatua za kisheria na kiuchunguzi badala ya amri za RC za kisiasa?
Upole huu (ambao nadhani umeletwa na Lowassa kwa nia njema) sasa unatumika vibaya na hawa watawala kwa kuwaona viongozi na wanachama wa vyama nje ya ccm ni mafala.
Nadhani wakipigwa mawe na mayai viza watajielewa. Huwezi kuagiza kijumlajumla bila ushahidi viongozi kukamatwa na watu wakakubali Kikondoo kondoo tuu. Arusha mmekuwaje tena? Mbona hayo hayatokei Mkoa wa Mara?
Amkeni nyie watu ebo! Au kwa vile Lema hayupo?
 
Tatizo la upinzani wa hapa ni kupinga kila kitu, kama kweli wameharib u miundo mbinu na umwagiliaji na kuhamasisha maandamano wafungwe kabisa.

Mkuu kuharibu miundo mbinu ni kosa, na linahitaji kushughulikiwa, na polisi wapongezwe wamefanya kazi yao kuwakamata wote wanaodhaniwa ni wahalifu,, maana hatuwezi kusema ni wahalifu mpaka mahakama itakapodhibitisha.

Watu wanachopinga order kutoka kwamba hakuna dhamana mpaka uchunguzi ukamilike? Nilitegemea mahakama ndo itoe mwongozo kisheria wa kutokuachiwa mpaka uchunguzi kukamilika na siyo kutoka kiongozi wa kisiasa.

Au katiba siku hizi haitumiki, na kama muongozo wa nchi ni katiba na haifuatwi basi tunaelekea pabaya.
 
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alitoa amri Jana kwa jeshi la polisi kuwakamata viongozi wa CHADEMA ambaye ni mwenyekiti wa wilaya ya Arumeru na viongozi wengine wa mkoa wa Arusha CHADEMA kwa kudhaniwa kuhamasisha wananchi kuharibu mashine za kilimo cha umwagiliaji zenye gharama ya tsh.million 16, na kuwatuhumu viongozi hao kuitisha maandamano mpaka sasa hivi wapo mikononi mwa polisi na upelelezi unaendelea mpaka sasa ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Mkoa huyo wa mkoa wa Arusha Gambo amesema wasipewe dhamana wakae polisi mpaka kesi itakapoisha.

Chanzo:Waandishi wa habari Arusha
Hivi kumbe dhamana ni Mtu tu anaamua huyu apewe, huyu asipewe??
Sio kwamba dhamana mtu akitimiza vigezo ndio anapewa??
Si ajabu hata Lema kuzungushwa Dhamana miezi miwili sasa kuna "Mtu" tu kaamua asipewe.
 
Mh.Gambo huruma imemzidi mno, Hao walitakiwa siyo kukamatwa tu, wapigwe na viboko na kuteswa sana hadi waache hizo tabia za kichochezi.
Umeona mkuu kabisa....nasisi huku hatuna huruma maana akijisahau akaja huku huyu alie kula rambi2 tutampiga mawe
 
Alexism kwani huko mnatumia mnatekeleza Ilani gani? Kama mnatekeleza ilani yake kumbe mnamkubali na hamtaweza kumpiga mawe. Vinginevyo tuamini kuwa umeropoka tu kwa bahati mbaya.
 
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alitoa amri Jana kwa jeshi la polisi kuwakamata viongozi wa CHADEMA ambaye ni mwenyekiti wa wilaya ya Arumeru na viongozi wengine wa mkoa wa Arusha CHADEMA kwa kudhaniwa kuhamasisha wananchi kuharibu mashine za kilimo cha umwagiliaji zenye gharama ya tsh.million 16, na kuwatuhumu viongozi hao kuitisha maandamano mpaka sasa hivi wapo mikononi mwa polisi na upelelezi unaendelea mpaka sasa ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Mkoa huyo wa mkoa wa Arusha Gambo amesema wasipewe dhamana wakae polisi mpaka kesi itakapoisha.

Chanzo:Waandishi wa habari Arusha
tatizo Ni jpm kuteua watu kwa nyadhifa wasizoziweza. Huyu rc ni janga na anatumia vibaya madaraka na kupenda misifa kama boss wake
 
Tatizo la upinchair niwa hapa ni kupinga kila kitu, kama kweli wameharib u miundo mbinu na umwagiliaji na kuhamasisha maandamano wafungwe kabisa.
Mkuu tuwekeni siasa pembeni. Vurugu zilizotokea Mang'ola chanzo chake ni mkuu wa mkoa ameenda kutengua amri halali ya PM aliyekuwa ameagiza mashine za kuvuta MAJI zikae umbali wa mita 500 kutoka chanzo cha MAJI. Sasa yeye kutokana na rushiwa nono alizovuta kutoka kwa wakulima wakubwa akalazimika kuwabeba na kuagiza mashine zikae mita 60.
 
Back
Top Bottom